Familia nyingine ni za ajabu sana

Nadharia ila tambua dunia hapa mambo mengi ya kimaisha hayana uhakika 100% kaka yanaendana na karma .

Hii ipo sana kwa vile wewe unakuwa na una watoto utakuja kuona ,dunia ina adhibu kwa kosa ambalo hukufanya mfano wewe unaweza kuwa msomi ukazaa watoto wote vilaza na hawataki hata shule tena wezi na wahuni kabisa.

Mambo mengi katika dunia yanasikitisha kwa ujumla ni suala la kuomba Mungu,babu yangu mimi ni imamu wa msikiti tena mtu mkubwa kijijini ila mwanae mmoja ndo mlevi mkubwa na mzinzi hapo kijijini mkubwa ana watoto kila kona wanaletwa tu hapo kwa bib ni chapombe kila kona kazalisha na kakimbia.

Mwalimu wetu mmoja msingi miaka hiyo alikuwa na mumewe anafanya kazi TRA ,walipata mtoto wa kwanza zombi kabisa yaani tahira hata lipelekwe shule za kulipia halielewi na mtoto wao wa pili ni wakiume ni mwizi kabisa na shule hataki ,ni vile wazazi wake ni wachaga so wana wanabars pale town ila watoto waliozaa wote hawana akili.wanazunguka tu kweny biashara za wazazi wao
 
Polee sana kwa changamoto. Familia nyingi zinapitia changamoto mbalimbali. Unaweza kulea watoto katika maadili mazuri wakaishia kuwa watoto wabaya.

Lkn huwa wanasema ubaya unaishi na mazuri ya watu huwa yanaishi kizazi hadi kizazi. Ndo maana huwa tunaambiwa wazazi tuwe tunatenda mema haijalishi nini tupande wema kwa ajili ya kizazi chetu.

Nina ndugu yangu mmoja ni mtu wa kusali sana. Na anamaisha mazuri watoto wake wanasoma shule nzuri na watoto wake wote wanapata mahitaji. Lkn ikatokea mtoto mmoja akawa na tabia ya wizi,,,akienda shule ataiba vitabu. Hela za wenzake

.Akienda kutembea nyumbani kwa watoto wenzake akikuta kuna hela anabeba. Ukijiuliza anakosa nini hamna.

Baadae ikabi aingie kwenye maombi na kufunga. Mungu akamuonyesha kuna uzao nyuma kaka mkubwa alimuibia hela mdogo wake hela alizozitunza kwa ajili ya mambo yake. Mdogo mtu akaja kujua kuwa kaka yake ndo aliiba. Kwa hiyo yule mdogo mtu akaweka kinyongo. Kwa hiyo na huyo mtoto ile roho ikawa imemvaa kwa sababu hiyo.

Hivyo ili kupona ikabidi mzazi wake atoe sadaka kwa wahitaji. Hadi leo huyo mtoto hajawahi kuiba tena.
Kwa hiyo kuna wakati tunaweza kuwalaumu watoto kwa tabia zao kumbe kuna mababu zetu na mabibi walifanya maagano yao au walifanya mabaya kwa watu.

Ili vizazi viwe salama tuache kufanya mabaya kwa wengine. Mabaya yanaishi na mema yanaishi
 
Ishi na Mama vizuri , mwambie ukweli kuhusu hali yako. We msaidie mama kadri ya uwezo wako, msisitizie abane matumizi kwa kuwa hali yako mbaya. Ili uokoe gharama mwekee ratiba utamtumia hela ama kila mwezi au wiki mbili . Na mwambie kutokana na hali yako utakuwa tayari kutoa kiasi ambacho utakipanga. Panga kiasi ambacho hakitokuumiza kiuchumi.
 
Mfano hili suala nahisi kuna ukweli ndo maana unaweza kushangaa watoto wa familia moja wanafanya vizuri shule ,na kinyume chake unakuta watoto wamezaliwa hata 7 ila wote akilini hamna kitu kama elimu wote wanapiga zero.
 
Unaambiwa Bwana Mungu huwapatiliza Watoto wa Uzao Mwovu hadi kizazi cha Nne.

Kama wewe unapata pesa kwa kudhulum endelea kula bata ila kuna uzao wako utalipa hiyo gharama ikiwa na wewe uko hai ili uchungu ukurudie.
 

Kaka we acha tu umri ninao na majukumu acha ibaki siri yangu familia zetu zina shida sana haki ya mungu, huwenda ningekuwa mbali sana kimaendeleo ila familia haki jamani na hapo still una wazazi wote wawili daaaaah! Qmmake wallah
 
Walau mshukuru mungu kaka iliwahi kula bata kipindi cha mshua sisi wengine hatujawahi kula bata hata kipindi mshua yupo tumekuwa kwa nguvu za mungu tu aiseee
Bila mama na wadogo zangu hata pesa ningekuwa situmi qmmke ila wanaujua udhaifu wangu uko wapi na ndio wanaoutumia kunilegeza [emoji3525][emoji3525][emoji3525]
 
Usiombe kuna wale wazazi wao walitengana na huko walipoenda kuoa na kuolewa familia zao zikavunjika na wengi wazee ,unakuwa unahudumia pande mbili huku na huku na kila mzazi ana mahitaji yake.

Kumbukumbu labda uliachwa upande mmoja ukapata madhila hapa duniani katika mqkuzi yako ,unapokuwa wale wazazi unatakiwa kuwasaidia kwa pamoja whilst ulikuwa unalelewa upande mmoja.

Ukianza tu kazi inawezekana hata mzazi mmoja zaidi ya miaka 10 hajui wewe unakula nn ila ukifanikiwa unatakiwa umjengee nyumba .😅
 
Asee wamekupa mtihani lakini hapo kwa mama huna namna msaidie tu Familia zetu zina mtihani Mola ndio anajua Wallahi.
 
Pole Sanaa kijana,Jipangeni ongea na ndugu Yako ambae akili zipo fresh,mchukueni mama either akae nammja wapo wenu aliejipanga halfu muwekeane mikakati ya kuwa mnatoa pesa kwa mama Kila mwezi.

Wale wahunii waacheni wajipambanie huko,tofauti na hapo huta sogea na watamstretisha pia bimkubwa mmkose..... Maana najua hapo alipo kelele ni nyingi. Lakini tatizoo nahisi hata wazazi kunanamna wamelitengeneza tatizoo kimalezii.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…