Familia nyingine ni za ajabu sana

Ni kweli kabisa maana kuna kipindi tulitaka tumtoe akatuambia hilo wazo tufute yeye awezi kuhama kwake
Kuna jamaa yangu aliniombaga Ushauri..yeye Mama yake yuko mkoani halafu Dada wa huyo jamaa yuko Dar..sasa jamaa akipeleka pesa kwa mama yake yule mama anagawa ile pesa anamtumia mwanawe wa Dar..baada ya siku mbili yule Mama analalamika kuishiwa pesa.
Nilimshauri jamaa atafute duka jirani na pale anapoishi mama yake na aongee na yule jamaa mama awe anachukua vitu pale dukani halafu bili ya vitu itumwe kwa jamaa na malipo yalikuwa yanafanywa moja kwa moja kwa mwenye duka.
Mama alikuwa anapewa pesa kidogo tu ya kununua vitu vidogo vidogo.
Hii ilisaidia.
 
Nimeipenda hii mbinu japo kwangu aiwez kufanya kazi maana wahusika wenyewe wapo hapo hapo nyumbani na sometime hz tunazotuma mama pia anawapa hao wanae
 
Kuendelea kusaidia huku unaumia roho siyo vizuri, afadhali usitoe kabisa, kuhusu hao ndugu zako ni wazi hawako normal, inawezekana wapo kwenye vifungo vya giza, wapeleke kwenye maombi watafunguliwa na watakuwa huru, Humu duniani mambo ni mengi mdogo wangu.
 
Ahsante mkuu nitalifanyia kazi wazo lako
 
Mkuu,huwa hatuaniki mambo ya kifamilia namna hii kwenye umma.Komaa na usaidie familia yako.Usijilizelize kama mwanamwali.Ukichukia kimpango wako.Huwa hatuanikani.
 
Binadamu wa kawaida hawezi kuishi Maisha Kama hayo unabidi kuelewa Familia yenu hipo Katika nguvu za giza ni swala la kuwaza kuwakomboa hao ndugu zako na dada zako walifungwa kiroho .

Hata Mama yako kafungwa kiroho tafuta watu sahihi wakusaidie.

Ndo maana hawawezi lolote Wapo vifungoni na sifa kuu ya mtu kuwa kifungoni ni ubishi wa Jambo na kutokujua maamuzi au kujali maumivu ya mwenzie.
 
Kijana yupo sahihi Mkuu hapa JF ndo Sehemu pekee Tz unaweza kutana na watu wenye kuelewa mambo.
Sehemu sahihi kinadharia.Sehemu sahihi zaidi ni kwa wale wanao kuona uso kwa macho na wakakuambia kinaga ubaga kilicho chema.JF ni njema lakini utashauriwa kwa hisia bila uhalisia.Tuwe na vyanzo vingi vya maarifa.
 
Usichokiona kuhusu familia yako ni kikubwa na kigumu zaidi ya kile unachokiona.

Usipotafuta mzizi wa shida ya familia yenu na kuimaliza hata wewe utaishia humohumo. Na dalili ushaziona huwezi save pesa yoyote wala huwezi fanya maendeleo

Mungu akufungue macho uone na kutatua tatizo


 
Ushauri wangu nikikupa kwa lugha laini hutaelewa. Nianze kwa kusema wewe ni mpuuzi unayejibebesha mizigo isiyokuhusu. Unadhani utambadilisha nini mtu wa miaka 50? Acha huo upumbavu. Kama tayari mama anawatetea basi fanya kumtumia hela ambazo unaona ziko ndani ya uwezo wako kisha kausha songa mbele na maisha yako. Pia anza ku-plan familia yako mapema. Yale makosa ya wazazi wetu tusiyarudie. Kuzaa watoto 9 huku kipato duni ni sawa na kujiua taratibu. Zaa unaomudu na hakikisha wanapata elimu bora ya kutosha. Nyie kwenu inaonekana karibu wote vipato duni hali inayochangiwa na elimu ndogo. Kwa sasa pambania maisha yako.
 
Tatizo mama akiondoka watapauza hapo home,au Wataanza kuuza vitu
 
Wewe ndio mpuuzi, nilijua utatoa ushauri wa maana. Kwa hiyo asimtumie mama yake hela? Unawajua akina mama wewe? Hata akituma elfu tano bado atakula na hao watoto wake wavivu na mwisho wa siku atapata presha afe kwa kukosa chakula cha kulisha wake
 
Nachukia watu wavivu kuliko navyomchukia shetani.

UVIVU NDIO CHANZO KIKUU CHA UMASKINI.
Dawa ya watu wavivu ni kuwakatia mirija yote mbona akili zitakaa sawa, mimi nina ndugu zangu mwaka wa pili huu hawajaona hata mia mbovu, wamelalama kila mahali, wamenisema kwa ubaya ni kama sijawahi wasaidia ila sasa wametulia. Mwisho wa siku mimi sio niliyewaleta duniani.

Sent from my CPH2219 using JamiiForums mobile app
 
Mpe condition bi mkubwa kuwa mkae naye ninyi...
 
Kabisa yaani nimeona ndugu na familia za Uongozi wa Juu ktk Taifa hili jinsi wanavyopitia mambo mazito na magumu.

Ukiwaona ni mawaziri na wakurugenzi kwenyw vyombo nyeti huku kwenye nyumba zao zinawaka moto.

I learned it must be karma.
Ni ukweli sio UONGO Ila kuna wabishi watakubishia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…