Familia ya Freeman Aikaeli Mbowe yathibitisha mwanafamilia kuwa na Corona

Familia ya Freeman Aikaeli Mbowe yathibitisha mwanafamilia kuwa na Corona

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
57,761
Reaction score
216,011
Mtoto wa Mbowe anaeitwa James Mbowe amesema kuwa ugonjwa wa korona ni janga la kitaifa na halipaswi kufanyiwa mchezo wala mzaha.

Amesema kitendo cha Mh. Makonda ni kitendo cha kushangaza kwa kuwa amejivika usemaji wa familia ya Mbowe kuwa anamshukuru Mungu kwa kuwa ugonjwa wa korona umepiga hodi kwenye familia ya Mbowe.

Amesema kuwa kwenye vita dhidi ya korona hatutakiwi kuweka itikadi za vyama bali tulitangulize Taia mbele katika vita dhidi ya korona.

Amesema kuwa amesikitishwa na kitendo hicho kwa kuwa ugonjwa ni siri kati ya mgonjwa na daktari anaemuhudumia. Hivyo aache kutafuta umaarufu wa kisiasa kwa kutumia ugonjwa wa korona.




TAARIFA YA FAMILIA YA FREEMAN AIKAELI MBOWE KWA UMMA WA WATANZANIA NA DUNIA.

KORONA NI JANGA KUBWA KULIKO VIONGOZI NA WATANZANIA WENGI TUNAVYODHANI:

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda, leo asubuhi ametangazia dunia kuwa mmoja wa Wanafamilia wangu (mtoto) amebainika kuwa na virusi vya Corona na pamoja na mambo mengine anamshukuru Mungu kwa janga hili kutokea kwa familia yangu.

Bila kujali Maadili na upotoshaji ulioambatana na taarifa hizo, ni kweli mwanangu Dudley amethibitika kupatikana na virusi vya Corona baada ya kupata homa za vipindi, kuumwa kichwa mfululizo na kukohoa kwa siku tano.

Mama yake, ambaye ni Daktari alipobaini hali hiyo alizitaarifu mamlaka za Serikali zinazoshughulikia Janga hili nazo zilimtaka kijana apelekwe Hospitali ya Mwananyamala, Dar es Salaam kwenye vipimo zaidi ambapo ilithibitika rasmi kuwa ana virusi vya Corona.

Aidha, timu ya Serikali imeendelea kutoa ushirikiano na ufuatiliaji wa karibu kwa familia yote ikiwemo ushauri nasaha kwa wanafamilia na marafiki wengine waliokutana na Dudley katika mikusanyiko mbalimbali ikiwemo kuweka wengine in Isolation au karantini.

Familia yangu inakiri kupokea ushirikiano wa kiwango kilichowezekana kutoka kwa Mamlaka husika za Serikali wakiongozwa na Waziri Ummy Mwalimu, Katibu Mkuu wake, Mganga Mkuu wa Serikali na Wataalam wao wote nikimaanisha Madaktari, Wauguzi nk.

Hali ya Dudley sasa imeimarika. Homa zimekwisha. Kichwa kimepona. Bado anakohoa kiasi na yuko chini ya uangalizi maalum kwenye “isolation”.

Dudley hajasafiri nje ya nchi mwaka huu. Maambukizi haya kayapata ndani ya Mkoa wa Dar es Salaam.

Ugonjwa huu haupaswi kuwa siri japo kuna miiko inayoongoza utaji wa taarifa za wagonjwa. Tatizo ni kubwa kuliko tulivyojiandaa na tunavyojiandaa.

Wengi wameitafuta familia kutaka kujua ukweli na undani wa jambo hili. Pengine kupitia ushuhuda wangu, tutaweza kuokoa wengi katika nchi yetu. Hakika leo kila mmoja anastahili kujua janga hili
liko mlangoni mwake!

Nimekiri kupata ushirikiano “kwa kiwango kilichowezekana”. Sina uhakika ni wangapi watapata “bahati” hiyo. Nimejifunza mengi. Nazungumza kwa mamlaka ya kuwa mhanga na shuhuda wa hali halisi tuliyo nayo. Tuna mlima mrefu wa kupanda. Hakika Serikali inahitaji msaada. Mlipuko hauko mbali. Tuelezane ukweli tusijechelewa.

Njia mojawapo muhimu ya kulishinda tatizo ni kulikubali na kulikabili kwa nguvu zote na kwa Umoja wetu.

Hatustahili kuchefuliwa na kejeli za Paul Makonda kipindi hiki. Tusiiachie serikali pekee. Tutajuta. Tusiilaumu tu, tuishauri nayo iwe tayari kuupokea ushauri na ishirikishe. Ni janga la Dunia na hakika tutaumizwa kuliko tunavyowaza.

Rai kwa Rais wetu Mheshimiwa John Pombe Magufuli: Unda timu ya kukusaidia na ushirikishe wadau wengine nje ya Serikali yako. Yako mengi ya kufanya nje ya mikakati ya kitabibu inayosimamiwa na Waziri Mkuu na Waziri Ummy Mwalimu.

Katika maisha maandalizi hayajawahi kuwa hasara, bali hasara iliyo
majuto ni kutokujiandaa na kupuuza yanayofanywa na walioyapitia kama
Ilivyo nchi za wenzetu zilizoendelea na hata nahitaji zetu!

Wengi wako tayari kukusaidia. Chadema tuko tayari kukusaidia na kulisaidia Taifa. Siyo wakati wa kulumbana huu.

Freeman Aikaeli Mbowe
Mkuu wa Familia na Shuhuda wa Janga
 
Kwa majina anaitwa James ambowe

Kama mnavyo fahamu ndugu zangu Watanzania, Mkuu wa Mkoa wa Dar-es-Salaam leo afajiri aliamkia kwenye kituo cha mabasi cha Ubungo. Na akawa anazungumza na abiria wanaokwenda mikoani. Lakini Jambo la kushangaza ambalo ninaamini hata nyinyi Watanzania limewashangaza ni la bwana Makonda kujivika usemaji wa familia.
 
Makonda anayoyafanya siyo kwamba hajui anakosea ila anafanya ili awe anazungumzwa na kutrend kwenye social media, hizi taarifa zake ambazo mtu mwenye akili timamu huona hazina maana ingekuwa zinaachwa ingemsaidia sana kumrekebisha kuzungumza mambo ya msingi ila kuzipublish hivi ndiyo matokeo yake haya kila siku ni vihoja
 
Nimependa hapo alipomalizia

Mithali 26 4-12
Usimjibu mpumbavu sawasawa na upumbavu wake;
Usije ukafanana naye.

5 Umjibu mpumbavu sawasawa na upumbavu wake;
Asije akawa mwenye hekima machoni pake.
6 Apelekaye ujumbe kwa mkono wa mpumbavu
Hujikata miguu, na kunywa hasara.
 
Mjanja hajaingia kichwa kichwa kama halima mdee na bulaya! Nilifikiri angesema makonda mpumbavu tumuone.

Wanajitokeza kipindi cha corona ila kwenye maandamano hawaonekani.

Harafu hajakanusha kama hakuna mgonjwa nyumbani kwao!
Au ndio njia za kula rudhuku.
 
Nimeelewa hayo maneno aliyoyanukuu toka kwenye biblia kama mwenyewe Yakobo alivyosema.
Pia nimepata ujumbe kuwa maadili ya kitabibu hayazingatiwi taarifa za ugonjwa wa mtu zimemfikiaje Makonda bila ridhaa ya mgonjwa mwenyewe na kwanini zimfikie yeye
 
Huyo Mtoto wa Mbowe ameshiba kodi za Watanzania

Akamatwe mara moja apigwe lupango

Sent using Jamii Forums mobile app
Usingizi wa mchana usipojidhibiti unaweza ukajikuta ukaamka halafu ukaamua uvue nguo zote ili ulale sawasawa ukidhani ni usiku wa manane kumbe ni saa nane mchana

Huyo mtoto wa Mbowe amekula hela yako lini mkwepa Kodi mkubwa wewe
 
Back
Top Bottom