Kwavile sikumuelewa, ikabidi nimpigie simu. Maelezo aliyonipa ni kwamba Baba yake alinipigia simu kunikumbushia ahadi yetu, Mimi nilivyopokea nikamjambia kisha nikakata simu. Nikakataa kwamba sijaongea na baba yake leo. Mpenzi nae akaona kama namdharau, akanikatia simu. Nilipoangalia kwenye call logs ni kweli nikakuta kuna simu iliingia toka kwa baba Mkwe na tuliongea kwa sekunde kumi. Inaonekana simu ilijipokea bila Mimi kujua, na inawezekana muda niliojamba ndio muda ambao ilijipokea ila sikumjambia makusudi.