Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,761
- 216,011
Kuna mama alituekeza maisha ya familia yake. Yeye na mume wake wamebarikiwa kupata watoto wanne. Walichukua jukumu la kulea watoto wawili wa ndugu waliofiwa na wazazi wao. Msichana wa kazi na kijana wa shamba.
Waliamua kuondoka mjini miaka mitano iliyopita baada ya kununua eneo la ekari tano kando ya mji na kujenga makazi yako. Wamefanikiwa kuzungusha uzio katika eneo lao lote. Ndani wanafuga kuku wa kienyeji 200 na bata 70. Wanalima mboga kama nyanya, vitunguu, mchicha, bilinganya, hoho nk.
Watoto wanasoma mjini, hivyo asubuhi kuna gari ya kupeleka watoto wanne wadogo shule kwani wakubwa wanasoma vyuoni na hurudi nyumbai wakati wa likizo. Usafiri wao ni pick up double cabin. Asubuhi inabeba pia na mboga za kupeleka sokoni baada ya watoto kushushwa shuleni.
Yule mama anasema tangu amehamia ‘kijijini’ kama anayoita mwenyewe, budget yake ya chakula imeshuka sana. Kila siku wanachinja kuku mmoja kutoka bandani wakiongeza na mboga kutoka katika bustani yao.
Vyakula anavyonunua ni sukari, mafuta ya kula, unga wa ngano, mchele na unga wa mahindi. Hata wakiamua kubadilisha mboga badala ya kuku hununua nyama ya ng’ombe au samaki kutokana na mauzo ya mboga kila siku.
Kulisha familia ya watu 10 kwa milioni 3 kwa mwaka na kila mtoto anapata mayai asubuhi, mchana kuna uhakika wa nyama na jioni chakula kizuri ni mafanikio.
Ninapenda kuishi mjini, zile harakati za umesikia uvivu wa kupika kuna chips mayai hapo mbele, kuna shishi kebab au kuna biryani mtaa wa pili, kuyakosa haya inahitaji moyo.