Familia ya watu 10 kutumia milioni 3 kwa mwaka kwa manunuzi ya vyakula

Familia ya watu 10 kutumia milioni 3 kwa mwaka kwa manunuzi ya vyakula

Kweli kabisa.
Yeye anaishi kwenye kijiji kabsa kuna maduka na like 3 kms kutoka hapo kuna center ya kijini ambapo kuna mawakala wa benki na huduma nyingine
Wale ma settler wa Kizungu walipofika Afrika walikimbilia vijijini. Kijijini ukiwa na plans utaishi vizuri sana. Jkiwa na eneo kubwa unafuga mbuzi, kila baada ya miezi mitatu unaweza kuuza mabeberu kumi, mwezi unaofuata unauza bata 10. Pesa haikakuki mfukoni.
 
Hilo ni kweli kabisa na wakawa matajiri wa kutupwa.
Aisee kweli kabisa yani umeongea ukweli kabisa
 
Kuchinja kuku mmoja kila siku kutoka bandani, kwa mwezi ni kuku 30, ukila kwa miezi tano hivohivo ni sawa na kuku 150, katika 200 wamebaki 50. Kuku kumlea hadi afikie kiwango cha kula ni atleast 5 months kwa kuku wa kienyeji na kama anapta chakula kizuri. Sijajua kama wanaongezeka au laa. Hii ni ngumu kuamini.
 
Kuku 200 kati yao 20 wana vifaranga, 20 wanataga, wakua kila siku. Kuna siku za kuchimba bata, kuna siku za kula samaki na kuna siku za kula nyama ya ng’ombe.
 
Inaitaji kujipanga sana. Sema ni jambo zuri kula vitu ulivyo viandaa mwenyewe maana kuna baadhi ya madawa( dawa kukuzia mboga mboga ) hautazitumia
 
Hapo kwenye kula Kuku Kila siku....! Sijui inabidi uwe na Kuku wangapi ili ule kwio Kila siku, anyway chini ya jua Mengi yanawezekana
 
Chai ya mchana jua kali na haina sukari.

Eniwei wabarikiwe.
 
Kuna mama alituekeza maisha ya familia yake. Yeye na mume wake wamebarikiwa kupata watoto wanne. Walichukua jukumu la kulea watoto wawili wa ndugu waliofiwa na wazazi wao. Msichana wa kazi na kijana wa shamba.

Waliamua kuondoka mjini miaka mitano iliyopita baada ya kununua eneo la ekari tano kando ya mji na kujenga makazi yako. Wamefanikiwa kuzungusha uzio katika eneo lao lote. Ndani wanafuga kuku wa kienyeji 200 na bata 70. Wanalima mboga kama nyanya, vitunguu, mchicha, bilinganya, hoho nk.

Watoto wanasoma mjini, hivyo asubuhi kuna gari ya kupeleka watoto wanne wadogo shule kwani wakubwa wanasoma vyuoni na hurudi nyumbai wakati wa likizo. Usafiri wao ni pick up double cabin. Asubuhi inabeba pia na mboga za kupeleka sokoni baada ya watoto kushushwa shuleni.

Yule mama anasema tangu amehamia ‘kijijini’ kama anayoita mwenyewe, budget yake ya chakula imeshuka sana. Kila siku wanachinja kuku mmoja kutoka bandani wakiongeza na mboga kutoka katika bustani yao.

Vyakula anavyonunua ni sukari, mafuta ya kula, unga wa ngano, mchele na unga wa mahindi. Hata wakiamua kubadilisha mboga badala ya kuku hununua nyama ya ng’ombe au samaki kutokana na mauzo ya mboga kila siku.

Kulisha familia ya watu 10 kwa milioni 3 kwa mwaka na kila mtoto anapata mayai asubuhi, mchana kuna uhakika wa nyama na jioni chakula kizuri ni mafanikio.

Ninapenda kuishi mjini, zile harakati za umesikia uvivu wa kupika kuna chips mayai hapo mbele, kuna shishi kebab au kuna biryani mtaa wa pili, kuyakosa haya inahitaji moyo.
Achana na motivational speakers! They advocate what they don't practice in real situation. All is ideal.
 
Hizo ni hadithi za kilimo cha matikiti maji.
 
Yaani ni kuwa:

Shilingi 3,000,000 ÷ siku 365 = 8219. 18/= kwa siku .

Kwahiyo anatumia sh.8219. 18/= kwa siku kwa familia ya watu 10 kwa chakula (asubuhi, mchana na jioni).

Labda. Ila sidhani
 
Maisha ya pembeni mwa mji matamu sana yaani, nakumbuka baada ya kumaliza chuo nilikuwa nakaa mjini kwenye nyumba ya mzee wakati huo sina ramani yoyote, ukiamka asubuhi unakuwa bored sana hususani kwa wale tunaopenda kujishughulisha.

Bahati nzuri mzee alinunua eka mbili pembeni huko, basi nikaona niende huko nikazungushia zile eka mbili, nikajenga kijumba kidogo sana, Banda la kuku na kuanzisha bustani.

Kusema kweli angalau naenjoy sijisikii kuwa bored Kama ilivyokuwa awali kipindi nakaa katikati ya mji.

Ushauri wangu Kama mtu ana nafasi nzuri kiuchumi na ana familia, basi anunue ardhi pembeni mwa mji, hii inaweza kuwasaidia graduates wa familia Kama hizo kuwa na sehemu za kuanzia kujitegemea.
 
Hongera sana
Kama utaweza kuongeza eneo ongeza. Ukiwa na plans nzuri shamba linaweza kuingiza laki tatu kwa siku kwa uchache. Ukifikia kiwango hicho ajiri hata bwana shamba. Wale wa diploma na certificate ukimwambia kazi ya laki tatu kwa mwezi anachukua. Atakupa ushauri wa wadudu na dawa pia mbolea.
 
Yaani ni kuwa:

Shilingi 3,000,000 ÷ siku 365 = 8219. 18/= kwa siku .

Kwahiyo anatumia sh.8219. 18/= kwa siku kwa familia ya watu 10 kwa chakula (asubuhi, mchana na jioni).

Labda. Ila sidhani
Kama kuna unga wa ngano ndani na mafuta ya kula, dada anaoka scones asubuhi na mayai ya kukaanga watoto wanawahi shule. Wakirudi kuna wali kuku mchicha. Jioni chapati mchuzi wa bilinganya na chai.
 
Hongera sana
Kama utaweza kuongeza eneo ongeza. Ukiwa na plans nzuri shamba linaweza kuingiza laki tatu kwa siku kwa uchachu. Ukifikia kiwango hicho ajiri hata bwana shamba. Wale wa diploma na certificate ukimwambia kazi ya laki tatu kwa mwezi anachukua. Atakupa ushauri wa wadudu na dawa pia mbolea.
Shukrani sana kwa ushauri mzuri, bado naendelea kuweka mipango mizuri, maana Mimi nimepitia mabegani mwa mzee wangu, basi na Mimi ninalo jukumu la kufanya hivyo kwa wale wanaonifuata.
 
Nimeipenda..ila mjini Kuna Raha yake.
Ukipita sinza Africa sana usiku warembo kibao wamejipanga unajichagulia tu tena wanakuita wenyewe bebi twende ukanipige pumbu huku akikupapasa zipu ya suruali. Sitaki kurudi kijijini mimi nikaliwe na nyoka.
 
Back
Top Bottom