Familia yake wanataka kunitolea mahari

Kwa uzoefu wangu wababa wengi huwa tunalogwa kwanza ili kulea watoto wasio wetu.
Yaani ole wako ulalamike eti mtoto fulani ana nywele kubwa anamaliza sabuni hivyo azinyoe wee hapo singo mama hakucheleweshii maana ataona ushaanzaa so unazimwa fastaa
 
Si ndio hapo,na ndio jambo silitak,mpenzi niliyenaye sijamwambia,kwakua nilikuja kula eid na watoto ndio wazazi wa bwana yule wakanipa taarifa hiyo,yeye anajua mipango ya kuwachukua watoto tu.

Aiseee, sasa umwambie fasta ila ukiwa unawashangaa hao, na kumuonyesha ni kituko kwako ili asifikirie bado unakituvna Baba watoto. Kama anajua Una watoto na yupo tayari muwalee pamoja, basi itakuwa jambo rahisi kwako akisaidia kuwarudisha kwako akijua mzigo wake kuwalea pia
 
Nimesoma comment nilipomaliza nahitimisha umeshafanya maamuzi ya kuwachukua ila fahamu kwao ni Kwa bibi Yao na baba yao, hapo unapotaka waishi ni kwako , hao watoto wanaenda kukosa identity kwa kuishi na baba wa kambo .Bora likizo waje kukusalimia italeta maana , pia fidia ilipwe ili wawe na urithi(kutambulika rasmi)kwao . Go west , go east home is the best.
 
Uzi unapata vybes hatari, hio hoja haikuhusu wewe inahusu hao wazazi, wenye Nia waende kwenu kwa wazazi wako kueleza nia yao na sababu zao, pia na wewe weka mezani hio ishu kwa wazazi mjadili. Kimsingi pesa ya utambulisho wa baba aliezaa na binti bila kumuoa ipo kundi la faini ya kuharibu usichana wa mwanamke na kuharibu future yake ikiwemo ufinyu wa kupata mume kirahisi. Kamwe haitwi mahari hio ni FAINI/Penalty. Na kwenye hilo ni huyo jamaa kuomba ahadi kufika mbele ya familia au kutuma mshenga na kupewa utaratibu.
 
Point nzito sana aisee hii
 
Wanaume gani hao wasiopenda watoto wa kambo...hiyo sample size Yako ndogo mno...labda ni wewe! Wanaume wakipenda wanapenda mazima!
Mmmmmmhmn hilo toleo la wanaume vilaza liliacha kutolewa miaka ya 1980. Kuanzia miaka ya 1990 kulitolewa toleo jipya la wanaume ambao upuuzi wa kuwekeana mitego ya malezi ya watoto wa wanaume wengine hauwaingii.

Yaani wewe ukapate watoto zaidi ya m'moja na mtu ambaye mnafanya maamuzi hayo kizembe zembe tu bila kutazama hatima yenu huko mbeleni halafu ukisha ya koroga unaanza kutumbua macho na kutaka huruma za jamii.

Hiyo haipo babu. Aliyekatika kiuno na kumwaga bao ndie atalea watoto wale. Uanaume ni kuzaa tu hovyo kama ng'ombe wa nyama ila kulea mnaanza sukumia vijana wa watu. Mxiem [emoji19][emoji19]
 
Wanazaa tu kama kuku wa amadoli. Yaani anaona kabisa kuwa huyu mtu mimi hajaniposa kwetu hatujaweka mazingira ya kuishi pamoja kama wachumba wanakulana kihuni tu then mtu huyu anakwenda kujishikisha ujauzito tena sio mara moja, mara mbili zote. Halafu anakuwa single mother ndio anajifanya anajua taratibu za kufuata.

Matoto ya kike ya siku hizi ni majinga. [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mimi niliamua kukaa pembeni baada ya kumfumania na kugundua hatuna malengo /ndoto sawa za maisha.
Kwann ukazaa nae halafu ndio uanze kutafakari hayo maneno unayosema, why haukufikiria mapema wakati mnaenda Lodge kupigana miti.
 
Ndugu yangu kwahiyo nibaki singo for the rest of my life?[emoji1787][emoji1787]ndugu mie bado kijana,baba yao yupo ila anafamilia yake tayari,so hakuna tabu katika hilo.maisha lazima yaendelee.
Me swali langu bado nakuhoji kuwa ilikuwaje ukafanya maamuzi ya kulala na kuzaa na mtu ambaye ana familia yake ulikuwa unatarajia nini kitokee. Kwamba atabonyeza delete familia yake itatoweka utaenda kukaa wewe?
 
Takataka kabisa hawa viumbe wacha tu wawe wanasemwa vibaya.
 
Nimemuelewa huyu Ironbutterfly kama mimimnyenyekevu alivyomsoma! Bado anampenda baby dad wake. Huyo Mwanaume ajiandae maana kibarua atakuwa nacho! Wanawake waone Hivi, akikupenda mkazaa wote na akakuacha kwa shingo upande, utakula wa chuya! Sijawahi kuona mahari inakuwa proposed na upande wa Mwanaume ! Kuna kitu kimejificha
 
Baby dady sio.
Hizi ni kauli ambazo zinakupa ishara huwa huko mbeleni huyu mwanamke atakuwa bado analeta mazoea na huyu jamaa na pengine wanaweza kuendelea kwa usiri.

Wanawake wa siku hizi wanapenda sana mambo ya hovyo hovyo. Mahusiano ambayo hayana mbele wala nyuma.
 
Haipo hiyo najiheshimu na tushakuwa watu wazima sasa,tunafocus kuwapatia watoto malezi Bora kwa wote kuwajibika[emoji120]
Ungekuwa unataka kuwapa watoto malezi bora usingewaweka katika situation ya baba huku mama kule. Huo ni unafiki tu unavyojaribu kujielezea kuwa unafanya hivi kwaajiri ya watoto. Sio kweli.

Acha watoto wabakie kwa bibi yao mzaa baba watalelewa huko. Kama ulikuwa hauyataki haya ungefanya mahusiano yako kwa kufuata taratibu na mila zetu. Sio unaenda kuzaa na mtu huko tena watoto wawili halafu unakuja hapa kujielezea elezea as if ni mtu reasonable.
 
Kwa upande wangu itaniharibia,we mtu wangu akijua nimetolewa mahari na baby dady atajisikiaje?
Ni suala la msamiati. Sidhani kama ni mahari bali ni fine ya "kukuharibu". Makabila mengi wana huo utaratibu kwa mwanaume ambae amemzalisha mwanamke kabla ya kumuoa. Mahari inaendana na posa ya kukuoa. Kama hawajatoa posa, hawawezi kutoa mahari. Na mahari inapangwa na aliyetolewa posa ( labda kama wewe ni mhindi) na sio anayetoa posa. Hata hii faini ilitakiwa ipangwe na upande wako na sio wao kujiamulia. Ni wazo jema lakini ungehusisha familia na mkubaliane kuhusu hatma ya watoto wenu.

Mababu na mabibi wanaweza kuwa ving'ang'anizi kwa wajukuu wao kutokana na mapenzi yao kwao. Ila ni lazima uwashukuru kwa sababu ulipokuwa na shida walikusaidia. Lazima kuna sababu iliyokufanya uwakabidhi wao watoto wako na sio wazazi wako au ndugu zako wengine.

Amandla...
 
Kubali utolewe hiyo mahari utakuja kunishukuru.

Ila ukishalipiwa hiyo mahari hiyo Ndoa ya jamaa inaenda kutingishika au Kuna kitu hukijui kinaendelea.

Jiandae kuwa mke Sasa na punguza au acha barabara kupitika hovyo na huyo The Mr Nice guy.
 
Kubali utolewe hiyo mahari utakuja kunishukuru.

Ila ukishalipiwa hiyo mahari hiyo Ndoa ya jamaa inaenda kutingishika au Kuna kitu hukijui kinaendelea.

Jiandae kuwa mke Sasa na punguza au acha barabara kupitika hovyo na huyo The Mr Nice guy.
Ila mi sijaelewa hapa,hivi kutolewa mahari ndio ndoa?
 
Mkuu,una hasira[emoji23][emoji23]
 
Ila mi sijaelewa hapa,hivi kutolewa mahari ndio ndoa?
Kimila Mwanamke akishalipiwa mahari ndio tayari kashaolewa huyo, kinachobaki ni sherehe tu.

Wamesema wanataka kumlipia mahari na sio kulipa fidia au kugomboa watoto.

Wanataka wauwe Ndege wawili kwa jiwe Moja yaani kujihakikishia watoto wameingia kwenye mamlaka yao na Mwanamke hatoki kwenye familia yao.

Maana yake wanamtaka mkamwana wao hivyo Ndoa ni lazima hapo ila mahusiano yenu kila mmoja yatateteleka na kuvunjika
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…