Mkuu kwanza ondoa hiyo fikra ya kwamba hao ni wanao tu.Hilo litakusababisha ufanye maamuzi ya kibinafsi yatakoyoathiri mahusiano yaliyopo na kuleta migogoro na hata kuwaathiri watoto.
Hao ni watoto wenu,wewe na mzazi mwenzako.Hivyo,katika kuamua lolote litakalowahusu watoto,kila mmoja ana nguvu sawa na mwenzake
Na watoto(bila ya kujali umri wao) wanahaki ya kuishi popote ambapo ni pazuri kwa ustawi wao,haijalishi kwa mama au kwa baba na hata nje ya baba na mama.
Hivyo,jadiliana pamoja na mzazi mwenzako,weka matamanio yako pembeni,uelewe nia yake,mueleze mawazo yako...na wote amueni jambo moja,tena bila kuvutana au kulumbana.
Yote hayo yanayotokea sasa,jua chanzo ni maamuzi ya kutokuwa pamoja,hivyo tumia akili sana kufanya maamuzi yako,mgogoro ulio katika nafsi yako au zenu msiuingize kwa watoto na kuwafanya nao waanze kuchagua na kubagua kwamba kule ni kuzuri huku kubaya.
Hilo la mahari,jadiliana na upande wa uliopendekeza hilo ujue nia yao kabla ya kuamua chochote,kuna mambo lazima yafanyike yanayowahusu watoto na mwenza wako wa sasa lazima akubaliane nayo,likiwemo pale ukiwa na watoto mzazi mwenzako ana haki ya kuja kuwaona na kuwatembelea.