Familia yake wanataka kunitolea mahari

Familia yake wanataka kunitolea mahari

Mkuu kwanza ondoa hiyo fikra ya kwamba hao ni wanao tu.Hilo litakusababisha ufanye maamuzi ya kibinafsi yatakoyoathiri mahusiano yaliyopo na kuleta migogoro na hata kuwaathiri watoto.

Hao ni watoto wenu,wewe na mzazi mwenzako.Hivyo,katika kuamua lolote litakalowahusu watoto,kila mmoja ana nguvu sawa na mwenzake

Na watoto(bila ya kujali umri wao) wanahaki ya kuishi popote ambapo ni pazuri kwa ustawi wao,haijalishi kwa mama au kwa baba na hata nje ya baba na mama.

Hivyo,jadiliana pamoja na mzazi mwenzako,weka matamanio yako pembeni,uelewe nia yake,mueleze mawazo yako...na wote amueni jambo moja,tena bila kuvutana au kulumbana.

Yote hayo yanayotokea sasa,jua chanzo ni maamuzi ya kutokuwa pamoja,hivyo tumia akili sana kufanya maamuzi yako,mgogoro ulio katika nafsi yako au zenu msiuingize kwa watoto na kuwafanya nao waanze kuchagua na kubagua kwamba kule ni kuzuri huku kubaya.

Hilo la mahari,jadiliana na upande wa uliopendekeza hilo ujue nia yao kabla ya kuamua chochote,kuna mambo lazima yafanyike yanayowahusu watoto na mwenza wako wa sasa lazima akubaliane nayo,likiwemo pale ukiwa na watoto mzazi mwenzako ana haki ya kuja kuwaona na kuwatembelea.
 
Ndiyo concern yangu kubwa,kuishi na kulea wanangu on daily basis,hivi vya kutuma hela na kuwatembelea once in a while sijaviafiki🙏kwanza hii situation imenifanya nione kama ndio naanza maisha ya kujitegemea,of which is not
pambania hilo mama, hapa chini ya jua ni nadra sana mtu atamthamini mtoto wa mwingine kama aliyemzaa mwenyewe.
 
Shukran kwa ushauri wako🙏🙏
Mkuu kwanza ondoa hiyo fikra ya kwamba hao ni wanao tu.Hilo litakusababisha ufanye maamuzi ya kibinafsi yatakoyoathiri mahusiano yaliyopo na kuleta migogoro na hata kuwaathiri watoto.

Hao ni watoto wenu,wewe na mzazi mwenzako.Hivyo,katika kuamua lolote litakalowahusu watoto,kila mmoja ana nguvu sawa na mwenzake

Na watoto(bila ya kujali umri wao) wanahaki ya kuishi popote ambapo ni pazuri kwa ustawi wao,haijalishi kwa mama au kwa baba na hata nje ya baba na mama.

Hivyo,jadiliana pamoja na mzazi mwenzako,weka matamanio yako pembeni,uelewe nia yake,mueleze mawazo yako...na wote amueni jambo moja,tena bila kuvutana au kulumbana.

Yote hayo yanayotokea sasa,jua chanzo ni maamuzi ya kutokuwa pamoja,hivyo tumia akili sana kufanya maamuzi yako,mgogoro ulio katika nafsi yako au zenu msiuingize kwa watoto na kuwafanya nao waanze kuchagua na kubagua kwamba kule ni kuzuri huku kubaya.

Hilo la mahari,jadiliana na upande wa uliopendekeza hilo ujue nia yao kabla ya kuamua chochote,kuna mambo lazima yafanyike yanayowahusu watoto na mwenza wako wa sasa lazima akubaliane nayo,likiwemo pale ukiwa na watoto mzazi mwenzako ana haki ya kuja kuwaona na kuwatembelea.
 
Sawa basi endelea kumpa uno la kisingle mama😂
Suala la uno lipo tu,mie binadamu,nakula vizuri,nakunywa,narelax ,niko kwenye umri wa ujana na uzazi ni ngumu niseme niishi kama mjane,na kulea wanangu kwa ukaribu nakutaka sana,ndiyo ishu kubwa hapo.
 
Wee mwaga uno tuu na vile wote tayari mnakuja na baggage zenu ngoma draw so mtaishi poa tuu
 
Basi ana haki ya kukaa na watoto wake,huenda alikuwa na nia ya kuomba msamaha na Wewe hukumruhusu,pengine mngeongea na kuyamaliza mkaendelea kama familia,ila kwa sababu we ulifanya maamuzi ya haraka ndo na yy akaamua kuoa. Hapo inabidi uchague Moja kuwaacha watoto walelewe na bibi yao ili uolewe au uwachukue uishi nao pasipo uwepo wa huyu bwana mpya.
Ushauri mwafaka!!!
 
Ndugu yangu kwahiyo nibaki singo for the rest of my life?🤣🤣ndugu mie bado kijana,baba yao yupo ila anafamilia yake tayari,so hakuna tabu katika hilo.maisha lazima yaendelee.
Huwezi kushika watoto na bwana mwingine! Ukiamua kuwa na mahusiano mengine, achana na idea ya kuishi na hao wanao. Kama kuishi na watoto hao ni lazima achana na mwanaume mpya. Choice zipo mbili tu. Hakuna ya tatu kuwachanganya wote itakuwa mtihani utakaopata F tu
 
Ukitolewa hiyo mahali utakuwa mke wa pili. Huyo mpenzi uliyenae yeye anasemaje?
Neno Mahari lina maana yake. Na anayetakiwa kudai mahari ni mzazi wa msichana si mzazi wa mwanaume. Hata kugomboa watoto, utagomboaje watoto wanakaa kwa mwanaume?. Kitu Ironbutterfly hajui, ni kuwa wazazi wa mwanaume wanataka akaolewe mke wa pili.
 
Hakuna mwanaume akiyekamilika akataka kulea watoto w mwanaume mwingine

Pili kwa sisi waafrica mtoto anachukua ubini wa baba. Kuchanganya family mbili zenye damu na koo tofauti huwa zinaleta shida sana. I have experienced this. .
Kuchanganya familia mbili zenye damu na koo tofauti huwa zinaleta shida sana, jaribu kufafanua hili kidogo.
 
Back
Top Bottom