Familia yake wanataka kunitolea mahari

Familia yake wanataka kunitolea mahari

Washirikishe wazee upande wako pia,

Pia neno "mahari" sio sahihi kutumika, sababu huto olewa na huyo baba watoto.

Pande zote mbili za wazazi wako(mama watoto) na wazazi wake mwanaume(baba watoto), wakubaliane na watafute msamiati sahihi usio na ukakasi hasa atakapo julishwa huyu mume wako mpya,

Walio tangualia kuchangia wamependekeza neno kama | "Gharama za kukomboa watoto" ili watambulike rasmi ukoo wa mwanaume , au "Fidia kwa familia yako", ili kuziunganisha hizi familia mbili, kwa sababu ya kuzaa watoto ambao wao tayari wamewatambua pasipo wewe kuolewa baba husika wa watoto ambaye tayari ana familia nyingine.

Familia zote mbili zikifikia muafaka, mapema kabisa mueleze mume wako mpya bila kufichwa Jambo lolote,

Kitu muhimu kwa sasa weka "haki na maslahi ya watoto kwa siku za usoni", wote hatujui nani atatangulia kufariki kati ya wewe na huyo baba wa watoto, Na je hatima ya watoto ni ipi?
Watoto hawskombolewi mkuu
 
Dah wanawake bhana ni wabinafsi, eti wamemzuia kuchukua watoto wake, au uliwapata na mchepuko, siyo wa huyo jamaa, ila ulimpa akupige tafu kwenye malezi.

Hii ni kwa wote kwanini usifunge ndoa kwanza ndiyo mpate watoto na siyo watoto kwanza then ndoa.
 
Hiyo kukutolea Mahari kisheria ni kuwahalalisha ( Legitimize) hao watoto watambulike katika familia yao.
Kama hao wazazi wana mtazamo kama wangu, ikiwa wanataka kutoa mahari ili uolewe na jamaa hiyo ni issue nyingine.
So rudi waulize wanakutolea mahari kwa minajili gani?
Yes, na huwa haiitwii mahari, bali ni kukomboa watoto kwa mujibu wa mila, tamaduni na desturi nyingi.

Mi nakushauri watoto ukae nao wewe angalau waambulie malezi ya mama, maana ninavyosoma btn lines hawaendi kuishi kwa baba.
 
Waache watoto waendelee kulelewa na Bibi yao..Wabibi ni Walezi wazuri sana..utakapowachukua means watalelewa na Dada utakapokua kazini of which they will be in highly risk of facing abuse unless otherwise you’re a PROUDLY HOUSEWIFE

HAKUNA MWANAUME ANAEPENDA KULEA WATOTO WA MWANAUME MWENZIE HUSUSANI AKIJUA KABISA MWANAUME MWENZIE YUKO HAI ..YAAN MWANAUME HUYO HAYUPO
 
Ila watu wa zamani walikuwa wabunifu sana kwenye hii inshu ya maisha,unaweza kuta mama anaishi na watoto wake pamoja na wajukuu kwa kuuza ndizi tu na hadangi na hadi anajenga

Lakin vijana wa siku hz wanapenda sana kurudisha mpira kwa kipa
 
Over my dead body siwez kuruhusu mwanangu kuish kwa mwanaume mwingne nikiwa hai,tatizo wanawake wabnafsi sana(baadh),sasa kama watt wanaish kwa bib yao na una access nao shda iko wap?plus unawachukua wakalelewe na house maid na baba wa kambo?hao watoto nina uhakika watateseka mno waache waish kwa bib yao na wew na mzaz mwenzio muwalee pale pale.ova
 
Waambie ukweli kwmba mm ni mchumba wa mtu , kwa hiyo cwezi kuwa na wanaume 2 kuhusu . Kuhusu watoto make chini mjadili nataka ikuambie tu watoto hawagombaniwi. Ikiwa watakaa kukupa achana nao baki kama mama unatuwa unaenda kuwatembelea nk,

Ukiona wanakuambia bora wakutolee mahali tambua ya kwamba mzazi mwenzo yie mwanamke wake wa sasa kuna changamoto kubwa sana ya mahusiano hivyo wakaona bora jamaa arudi nyuma , yaani kukurudia ww
 
Over my dead body siwez kuruhusu mwanangu kuish kwa mwanaume mwingne nikiwa hai,tatizo wanawake wabnafsi sana(baadh),sasa kama watt wanaish kwa bib yao na una access nao shda iko wap?plus unawachukua wakalelewe na house maid na baba wa kambo?hao watoto nina uhakika watateseka mno waache waish kwa bib yao na wew na mzaz mwenzio muwalee pale pale.ova
Sasa nawaleaje watoto wako mkoa mwingine na mimi mkoa mwingine?yani hapa naonana nao Mara tatu kwa mwaka tu,mie naona haijakaa sawa.
 
Habari za eid pili waungwana,

Iko hivi, nimejaliwa kuzaa watoto wawili wa kiume na bwana mmoja. Kutokana na sababu zilizokuwa nje ya uwezo, hatukuoana na huyo bwana. Watoto wote nilikuwa naishi nao kwangu, huku tukisaidizana malezi. Yeye alishaoa kama miaka mitatu nyuma.

Kama miaka miwili nyuma nilipata changamoto kazini na mambo mengi yalitokea upande wangu hivyo sikuwa stable kuendelea kuishi na watoto. Tulipojadiliana pande zote, wazazi wake wakasema niwakabidhi watoto wawalee hadi hapo nitakapo kuwa sawa.

Basi watoto nikawapeleka kwao, nikawa na still huwa naenda kuwatembelea pindi nipatapo nafasi pamoja na kuchangia gharama za ada na mahitaji mengine ya watoto.

Muda umeenda, nimerudi kwenye fomu, na nimeona nahitaji kuwachukua watoto niwalee sasa, yaani niishi nao huku nilikohamia kikazi. Wazazi wake bwana yule wamekuja na wazo kuwa, familia yao imeamua jamaa anitolee mahari kwa mujibu wa mila zao, so wamenambia niifahamishe wazee wangu ili taratibu zifanyike.

Binafsi sijaafiki suala hilo, kwani jamaa alishaoa na kashazaa watoto wengine wawili kwa mkewe. Hata mila za kwetu haziafiki jambo hilo, isitoshe mimi niko na mtu wangu ambaye tuna plan zetu za hapo baadae kidogo, naona kama ni mbinu ya kunizuia kuchukua wanangu.

Hebu mnipe ushauri wadau, namna gani naweza kuwachukua watoto bila kuleta mikwaruzano?
Kati yako na yeye,nani alimuacha mwenzake?Nikipata jibu la hapo,nitatoa ushauri wangu
 
Sasa nawaleaje watoto wako mkoa mwingine na mimi mkoa mwingine?yani hapa naonana nao Mara tatu kwa mwaka tu,mie naona haijakaa sawa.
my sister,bora nusu shari kuliko shari kamili!as long as watoto wanakutambua,na wako kwa bib yao mahal ambapo hata usku unaenda,waache pale pale kama ambavyo uliwaacha kipnd una changamoto na hukupata malalamiko!!walipo ndo salama zaid kulko kwako na kwa baba yao
 
Over my dead body siwez kuruhusu mwanangu kuish kwa mwanaume mwingne nikiwa hai,tatizo wanawake wabnafsi sana(baadh),sasa kama watt wanaish kwa bib yao na una access nao shda iko wap?plus unawachukua wakalelewe na house maid na baba wa kambo?hao watoto nina uhakika watateseka mno waache waish kwa bib yao na wew na mzaz mwenzio muwalee pale pale.ova
Wateseke kivip ilhal nilikuwa naishi nao vizuri tu 🙏 ni changamoto flan ilinipata so sikuwa na uwezo wa kuwalea ndo tukakubaliana niwapeleke kwao hadi nitakapo kaa sawa,ofwhich Niko sawa sasa,so nawahitaj.
 
Wala haikuwa changamoto ya fedha,ni ishu nyingine iliyonithrow off balance,hadi nikahitaj usaidiz wa kulea watoto.
Ila watu wa zamani walikuwa wabunifu sana kwenye hii inshu ya maisha,unaweza kuta mama anaishi na watoto wake pamoja na wajukuu kwa kuuza ndizi tu na hadangi na hadi anajenga

Lakin vijana wa siku hz wanapenda sana kurudisha mpira kwa kipa
 
Yes, na huwa haiitwii mahari, bali ni kukomboa watoto kwa mujibu wa mila, tamaduni na desturi nyingi.

Mi nakushauri watoto ukae nao wewe angalau waambulie malezi ya mama, maana ninavyosoma btn lines hawaendi kuishi kwa baba.
Ndiyo concern yangu kubwa,kuishi na kulea wanangu on daily basis,hivi vya kutuma hela na kuwatembelea once in a while sijaviafiki🙏kwanza hii situation imenifanya nione kama ndio naanza maisha ya kujitegemea,of which is not
 
Back
Top Bottom