Familia yangu imenigomea nisimuoe mpenzi wangu sababu wanahisi nitakuja kuteseka

Familia yangu imenigomea nisimuoe mpenzi wangu sababu wanahisi nitakuja kuteseka

Mboka man

JF-Expert Member
Joined
Aug 22, 2020
Posts
478
Reaction score
1,647
Ndugu zangu huyu binti nimetoka naye mbali sana zaidi ya miaka 5 tupo katika mahusiano na mimi ndio ninamjua vizuri sana.

Ila shida inakuja familia yangu imenigomea kumuoa huyu binti kwa kigezo ntakuja kuteseka badaye na hii inatokana kuna kauli alipishana na mdogo wangu wa kike katika mazungumzo nae kwenye simu.

Hivyo ikapelekea huyu dogo langu kuwaambia wazee wangu yote yaliyojitokeza hivyo hili swala likapelekea wazazi wangu hawataki nimuoe huyu binti kwani wanamuona kama mtu mwenye jeuri na kiburi hivyo atakuja kunipa shida sana hapo baadaye.

Je nifanye nini ndugu zangu ukiangalia familia yangu imeshamkataa huyu binti hawataki hata kumsikia.
 
Wamepishana kauli gani?

Wewe kama waona hana kasoro, weka mchuchu ndani...

hii inatokana kuna kauli alipishana na mdogo wangu wa kike katika mazungumzo nae kwenye simu
 
weka hapa ilo neno / maneno aliyochambwa nayo mdogo wako, usikute dogo lako nalo lina mdomo kama juma lokole
Swala zima ni harusi, dogo langu alikuwa anajaribu kuzungumza nae harusi isogezwe mbele kidogo sababu ya changamoto, yee akamjibu hilo halimhusu ila nyumbani wazungumze na mshenga ndio atoe taarifa nyumbani basi hapo ndio ikawa sababu nyumbani kumchukia huyu binti
 
Umekaa kwenye mahusiano na mtoto wa watu for 5 years na still huwezi kufanya decision ya ndoa yako mwenyewe? Mkuu, how old are you?? Just for your interest, wanawake (dada yako being inclusive ) by nature huwaga hapendani; lini umewahi kusikia baba ana ugomvi na mkwewe wa KIKE!?

Lini umewahi kusikia mashemeji wa kiume wana ugomvi na mke wa kaka/mdogo wao? Always mama mkwe na wifi/dada! Umempenda, weka msimamo, mwambie dada yako hata yeye ni mwanamke, huenda huko anako date nako hakubaliki, na wanatafuta asikubalike ili asiolewe.
 
Umekaa kwenye mahusiano na mtoto wa watu for 5 years na still huwezi kufanya decision ya ndoa yako mwenyewe? Mkuu, how old are you?? Just for your interest, wanawake (dada yako being inclusive ) by nature huaga hapendani; lini umewahi kusikia baba ana ugomvi na mkwewe wa KIKE!? Lini umewahi kusikia mashemeji wa kiume wana ugomvi na mke wa kaka/mdogo wao? Always mama mkwe na wifi/dada! Umempenda, weka msimamo, mwambie dada yako hata yeye ni mwanamke, huenda huko anako date nako hakubaliki, na wanatafuta asikubalike ili asiolewe.
Huu uzi uishie hapa! Jamaa kamaliza kila kitu!
 
Ndugu zangu huyu binti nimetoka nae mbali sana zaidi ya miaka 5 tupo katika mahusiano na mimi ndo ninamjua vizuri sana.

Ila shida inakuja familia yangu imenigomea kumuoa huyu binti kwa kigezo ntakuja kuteseka badae na hii inatokana kuna kauli alipishana na mdogo wangu wa kike katika mazungumzo nae kwenye simu hivyo ikapelekea huyu dogo langu kuwambia wazee wangu yote yaliyojitokeza hivyo hili swala likapelekea wazazi wangu hawataki nimuoe huyu binti kwani wanamuona kama mtu mwenye jeuri na kibuli hivyo atakuja kunipa shida sana hapo badae.

Je nifanye nini ndugu zangu ukiangalia familia yangu imeshamkataa huyu binti hawataki hata kumsikia.
Mchuma janga hula na wa kwao... Sasa kijana wazee wanakupendea wema.
But anyway unapaswa kuwa na akili kama za mama yako ila maamuzi ya mzee....😎
 
Majuto yaje tu sijaona cha maana hapo! Kajibiwa exactly ambavyo alitakiwa kujibiwa sababu mwenye mandate ya kufanya communications baina ya familia ni mshenga!
Ni kweli Kuna sbb zengine hazina maana Ila Kuna ushauri mwengine wazazi wakitoa. Au mtu zaidi ya 3 wameutoa, basi unatakiwa kukaa chini na kuutafakari vizuri .

Mi nna ushuhuda kabisa, mtu kaambiwa usiolewe, usiolewe na huyo mwanaume. Watu zaidi ya 5 lakini jibu lake likawa Mimi ndo nishampenda, hamniambii kitu. Sasa hivi anagangamala huko na ndoa yake, kulia anataka, kuacha anataka. Ila uwezo Hana, atamwambia nani na hakutaka kusikiliza ya wakubwa?
 
Back
Top Bottom