Familia yangu imenigomea nisimuoe mpenzi wangu sababu wanahisi nitakuja kuteseka

Familia yangu imenigomea nisimuoe mpenzi wangu sababu wanahisi nitakuja kuteseka

Swala zima ni harusi dogo langu alikuwa anajaribu kuzungumze nae harusi isogezwe mbele kidogo sababu ya changamoto yee akamjibu hilo halimhusu ila nyumbani wazungumze na mshenga ndio atoe taarifa nyumbani basi hapo ndio ikawa ndio sababu nyumbani kumchukia huyu binti
Acha ujinga huu mkuu, mkeo alikuwa sahihi, dadako ana kiherehere tu
 
Simama imara kama Mwanaume uchukue maamuzi magumu, kama sababu yenyewe ni hiyo huyo Mchumba wako sidhani kama ana makosa labda kama kuna kingine umeficha.
 
Mahari ya milioni 7 ndio iliyoanzisha tatizo kwenye hizo familia.

Halafu inawezekana mdogo wako alikua na lengo la kujenga ukaribu na wifi yake, lakini badala ya mwanamke wako kumuelezea vizuri ameongezea hayamhusu
 
KwanZa dada yako nae ana kimbelembele sana au wewe ndo uliruhusu mazoea ya kijinga.Hiyo ishu ni sensitive sana

Mimi mke wangu kabla sijamuoa alikuwa kazoeana sana na mdg wangu wa kike siku moja tukiwa sebuleni wife kanitembelea enzi hizo wachumba wapo wenyewe wanajifanya wanapendanaaa na wanajuana sanaaa nikawaambia tu nyie jifanyeni mnapendana hivyo hivyo na kama mnaigiza basi igizeni hivyo hivyo hata mkigombana.Mimi sitakuwa na mda wa kusuluhisha unafiki wa kike kike kwahiyo km mnanafikiana basi endeleeni hivyo hivyo.Nakujuana kwenu kusilete shobo kwenye mahusiano yangu.

Wanawake uwaga na competition za kipuuzi unaweza kukuta demu wako kaona dada yako ana shobo sana kampa makavu basi na dada yako nae kaona hataaa sikubali huyu lzm nimfitini mpk asiolewe.

Lakini dmeu wako hana dharau kweli???na wewe usigekuwa unajifanya kipovu wkt ukweli mwanamke mwenye dharau one day lzm atazingua
 
Kuwa muwazi ili tukushauri,. weka wazi hiyo kauli aliyoongea.
 
Swala zima ni harusi dogo langu alikuwa anajaribu kuzungumze nae harusi isogezwe mbele kidogo sababu ya changamoto yee akamjibu hilo halimhusu ila nyumbani wazungumze na mshenga ndio atoe taarifa nyumbani basi hapo ndio ikawa ndio sababu nyumbani kumchukia huyu binti

Mbona alijibu vizuri tu.....

Hao ndugu zako nao chemistry tu hazijaenda na Wife.... hakuna kiburi chochote hapo... KIsirani tu
 
Ndugu zangu huyu binti nimetoka nae mbali sana zaidi ya miaka 5 tupo katika mahusiano na mimi ndo ninamjua vizuri sana.

Ila shida inakuja familia yangu imenigomea kumuoa huyu binti kwa kigezo ntakuja kuteseka badae na hii inatokana kuna kauli alipishana na mdogo wangu wa kike katika mazungumzo nae kwenye simu.

Hivyo ikapelekea huyu dogo langu kuwambia wazee wangu yote yaliyojitokeza hivyo hili swala likapelekea wazazi wangu hawataki nimuoe huyu binti kwani wanamuona kama mtu mwenye jeuri na kiburi hivyo atakuja kunipa shida sana hapo badae.

Je nifanye nini ndugu zangu ukiangalia familia yangu imeshamkataa huyu binti hawataki hata kumsikia.
Mwanaume atamwacha Baba na Mama yake, na ataambatana na mkewe. Iliandikwa mahala, sijui unaamini lipi?
 
Swala zima ni harusi dogo langu alikuwa anajaribu kuzungumze nae harusi isogezwe mbele kidogo sababu ya changamoto yee akamjibu hilo halimhusu ila nyumbani wazungumze na mshenga ndio atoe taarifa nyumbani basi hapo ndio ikawa ndio sababu nyumbani kumchukia huyu binti
Protocol au itifaki ya masuala hayo imekaaje? Mara ya kwanza mlipotangaza uchumba na tarehe ya harusi mlikuwa mnainua simu na kuongea na bibie moja kwa moja?
Dogo lako ni mwanaume au mwanamke? Anajua suala la harusi na ndoa kwa ujumla lilivyo na nafasi kwa mwanamke kweli?
 
Ukioma familia inaamua uoe au usioe...au umuoe.nani

Kaka

Achana na msichana wa watu usiendelee kumpotezea muda

Maana bado hujapevuka.
 
Swala zima ni harusi dogo langu alikuwa anajaribu kuzungumze nae harusi isogezwe mbele kidogo sababu ya changamoto yee akamjibu hilo halimhusu ila nyumbani wazungumze na mshenga ndio atoe taarifa nyumbani basi hapo ndio ikawa ndio sababu nyumbani kumchukia huyu binti
Sasa alichokosea huyu bonti hapa ni nini

Mbona yupo sahihi

Labda dada yako nae alikuwa na kisirani

Hilo neno "hayamhusu" ndio familia imepanic?

Ina maana wazazi wako hawajui taratibu za kusogeza tarehe mbele??????
 
Huyo mdogo wako ana mamlaka gani ya kumuambia mkeo mtarajiwa ndoa isogezwe na isiwe wewe? kwani mwenye mamlaka ya kusogeza ndoa ni nani kati yako na dada yako??

Mpaka mmefika process za ndoa maana yake na mahari imeshatolewa, na kama imetolewa kumbuka naye binti kwao wameshaanza kujiandaa kwa ajili ya ndoa hiyo sasa kuahirisha hilo suala haliko mikononi mwa binti ndio maana mdogo wako kaambiwa waongee na mshenga ndio apeleke taarifa kwenye familia ya bint.

Mdogo wako ameongea ya uongo tu nyumbani ili wazazi wajae sasa hapo mwenye maamuzi ni wewe.
Yaani hapo inaonyesha familia ya mwanaume wana tatizo......

Hivi ina maana watu wazima (baba yake na mama yake) wameshindwa kuwasiliana na wazazi wenzao (achikia mbali mambo ya mshenga) kuhusu kusogeza mbele???

Wana shida hawa!!!
 
Back
Top Bottom