Familia yangu imenigomea nisimuoe mpenzi wangu sababu wanahisi nitakuja kuteseka

Familia yangu imenigomea nisimuoe mpenzi wangu sababu wanahisi nitakuja kuteseka

Majuto yaje tu sijaona cha maana hapo! Kajibiwa exactly ambavyo alitakiwa kujibiwa sababu mwenye mandate ya kufanya communications baina ya familia ni mshenga!
Extrovert huwa unafanyaga kosa gani. Mbona ban zinakuandama Sana? [emoji1787]
 
Umekaa kwenye mahusiano na mtoto wa watu for 5 years na still huwezi kufanya decision ya ndoa yako mwenyewe? Mkuu, how old are you?? Just for your interest, wanawake (dada yako being inclusive ) by nature huaga hapendani; lini umewahi kusikia baba ana ugomvi na mkwewe wa KIKE!? Lini umewahi kusikia mashemeji wa kiume wana ugomvi na mke wa kaka/mdogo wao? Always mama mkwe na wifi/dada! Umempenda, weka msimamo, mwambie dada yako hata yeye ni mwanamke, huenda huko anako date nako hakubaliki, na wanatafuta asikubalike ili asiolewe.
Kesi imeishia hapa
 
Swala zima ni harusi dogo langu alikuwa anajaribu kuzungumze nae harusi isogezwe mbele kidogo sababu ya changamoto yee akamjibu hilo halimhusu ila nyumbani wazungumze na mshenga ndio atoe taarifa nyumbani basi hapo ndio ikawa ndio sababu nyumbani kumchukia huyu binti
Huyo mdogo wako ana mamlaka gani ya kumuambia mkeo mtarajiwa ndoa isogezwe na isiwe wewe? kwani mwenye mamlaka ya kusogeza ndoa ni nani kati yako na dada yako??

Mpaka mmefika process za ndoa maana yake na mahari imeshatolewa, na kama imetolewa kumbuka naye binti kwao wameshaanza kujiandaa kwa ajili ya ndoa hiyo sasa kuahirisha hilo suala haliko mikononi mwa binti ndio maana mdogo wako kaambiwa waongee na mshenga ndio apeleke taarifa kwenye familia ya bint.

Mdogo wako ameongea ya uongo tu nyumbani ili wazazi wajae sasa hapo mwenye maamuzi ni wewe.
 
Swala zima ni harusi dogo langu alikuwa anajaribu kuzungumze nae harusi isogezwe mbele kidogo sababu ya changamoto yee akamjibu hilo halimhusu ila nyumbani wazungumze na mshenga ndio atoe taarifa nyumbani basi hapo ndio ikawa ndio sababu nyumbani kumchukia huyu binti
Yaani unaruhusu dada yako na mkeo mtarajiwa wakae wazungumze muda wa ndoa yako?

Jando zirudi.
 
Ni kweli Kuna sbb zengine hazina maana Ila Kuna ushauri mwengine wazazi wakitoa. Au mtu zaidi ya 3 wameutoa, basi unatakiwa kukaa chini na kuutafakari vizuri .

Mi nna ushuhuda kabisa, mtu kaambiwa usiolewe, usiolewe na huyo mwanaume. Watu zaidi ya 5 lakini jibu lake likawa Mimi ndo nishampenda, hamniambii kitu. Asa ivi anagangamala uko na ndoa yake, kulia anataka, kuacha anataka. Ila uwezo Hana, atamwambia nani na hakutaka kusikiliza ya wakubwa?
Hahahahahah yeye ndio kampenda😅 muacheni akomae na ndoa yake jamani!

Ushauri mzuri ila kwa huo unaotolewa hapo ni baada ya mdogo mtu kumsagia kunguni wifi yake😅
 
Huyo mdogo wako ana mamlaka gani ya kumuambia mkeo mtarajiwa ndoa isogezwe na isiwe wewe? kwani mwenye mamlaka ya kusogeza ndoa ni nani kati yako na dada yako?? mpaka mmefika process za ndoa maana yake na mahari imeshatolewa, na kama imetolewa kumbuka naye binti kwao wameshaanza kujiandaa kwa ajili ya ndoa hiyo sasa kuahirisha hilo suala haliko mikononi mwa binti ndio maana mdogo wako kaambiwa waongee na mshenga ndio apeleke taarifa kwenye familia ya bint. Mdogo wako ameongea ya uongo tu nyumbani ili wazazi wajae sasa hapo mwenye maamuzi ni wewe.
Hahaahahah dogo kamsagia kunguni wifi baada ya kupewa kubwa! Inaonekana dogo ana tabia ya kihere here
 
Huyo mdogo wako ana mamlaka gani ya kumuambia mkeo mtarajiwa ndoa isogezwe na isiwe wewe? kwani mwenye mamlaka ya kusogeza ndoa ni nani kati yako na dada yako?? mpaka mmefika process za ndoa maana yake na mahari imeshatolewa, na kama imetolewa kumbuka naye binti kwao wameshaanza kujiandaa kwa ajili ya ndoa hiyo sasa kuahirisha hilo suala haliko mikononi mwa binti ndio maana mdogo wako kaambiwa waongee na mshenga ndio apeleke taarifa kwenye familia ya bint. Mdogo wako ameongea ya uongo tu nyumbani ili wazazi wajae sasa hapo mwenye maamuzi ni wewe.
Huyo mwanamke ndo anaolewa sehemu itakayomletea matatizo. Akubali tu ombi bora awe single mama.
 
Kuna kaka mmoja aliambiwa na mama ake kua mkewe hafai. Huyo mkewe walishapata na mtoto mmoja mama mkwe gubu balaa. Bas kaka akaamua kuachana na mkewe kwa kushurutishwa na mama ake.

Akaja kupata mwanamke mwingine, huyo mwanamke alikua bomu. Anawasumbua wote mume na mama yake. Akienda kwa mama mkwe hamsaidii kazi anakaa anakunja 4 anasubiri kupikiwa. Yule bibi alijuta akaanza kumkumbuka yule wa kwanza. Na yule wa kwanza alishamove on na maisha yake.

Moral of the story; sio kila kitu mzazi anachosema ni sahihi. Vingine vitakuja kukucost wewe maisha yako yote na yeye ajisahaulishe kua alikupotosha.
 
Huyo mwanamke ndo anaolewa sehemu itakayomletea matatizo. Akubali tu ombi bora awe single mama.
ombi ilitakiwa apewe na mchumba wake sio mtu mwingine yeyote, kwa sababu hao wengine hawafahamu kitu juu ya mahusiano yao, yaani endapo huyu binti ataolewa na ndoa yake ikawa na shida, yeye hatakuwa na tatizo, tatizo litakuwa kwa mumewe
 
Ndugu Zangu Oeni Haraka
Wewe Ndiyo Una Uamuzi
Miruzi Mingi Humpoteza Mbwa
 
Yani ni wazi kabisa, huyo mwanamke ndio anaenda matatizoni haswa! Hio familia kama sio wanyakyusa sijui😅 maana ndio tabia zao kuwawekea wali vipengele..Af wanakomalia ukoo mzima yani hakuna hakuna hapa😂😂😂
Hahaha huyu mwanamke hataki kupanda basi anang'ang'ania kusafiri na BMW inayochemsha na yenye tatizo la umeme sababu ni private car na ni BMW.
 
Kuna kaka mmoja aliambiwa na mama ake kua mkewe hafai. Huyo mkewe walishapata na mtoto mmoja mama mkwe gubu balaa. Bas kaka akaamua kuachana na mkewe kwa kushurutishwa na mama ake. Akaja kupata mwanamke mwingine, huyo mwanamke alikua bomu. Anawasumbua wote mume na mama yake. Akienda kwa mama mkwe hamsaidii kazi anakaa anakunja 4 anasubiri kupikiwa. Yule bibi alijuta akaanza kumkumbuka yule wa kwanza. Na yule wa kwanza alishamove on na maisha yake.

Moral of the story; sio kila kitu mzazi anachosema ni sahihi. Vingine vitakuja kukucost wewe maisha yako yote na yeye ajisahaulishe kua alikupotosha.
Hahahahahah hapo tatizo naliona kwenye familia zaidi kuliko kwa mke wa jamaa😅!

Wanyaki muache mambo yenu haya alaaah!

Ndoa ya sister angu ilienda kwenye safe mode kwa style hio hio...Mtoto wa mjomba kamchokonoa sister muda mrefu tu sister akampa kubwa kaenda kutangaza ukoo mzima kuwa wifi ... kanitukana oneni sms zake.

Jamaa kashikwa maskio na mama yake akaja kumfukuza mke 😅 eti aondoke kwake. Matokeo yake kila kukicha anaomba msamaha sasa penzi lilishachacha anaonekana ng’ombe tu!!!
 
Dada yako ndio kimeo ila huyo mchumba pia kimeo hana kauli nzuri,dada yako yeye kama nani anaongelea harusi isiyomuhusu,we pia kimeo harusi yako inaongekewaje na dada yako we uko tu unaangalia
 
Ndugu zangu huyu binti nimetoka nae mbali sana zaidi ya miaka 5 tupo katika mahusiano na mimi ndo ninamjua vizuri sana.

Ila shida inakuja familia yangu imenigomea kumuoa huyu binti kwa kigezo ntakuja kuteseka badae na hii inatokana kuna kauli alipishana na mdogo wangu wa kike katika mazungumzo nae kwenye simu hivyo ikapelekea huyu dogo langu kuwambia wazee wangu yote yaliyojitokeza hivyo hili swala likapelekea wazazi wangu hawataki nimuoe huyu binti kwani wanamuona kama mtu mwenye jeuri na kibuli hivyo atakuja kunipa shida sana hapo badae.

Je nifanye nini ndugu zangu ukiangalia familia yangu imeshamkataa huyu binti hawataki hata kumsikia.
Sisi tunamjua kwani huyo mtarajiwa wako?

Acha ubwege, fanya maamuzi ya kuoa au kuacha ili usimpotezee muda
 
Back
Top Bottom