Fani yako inakusaidiaje katika kutatua Kero za Jamii?

Fani yako inakusaidiaje katika kutatua Kero za Jamii?

Fundi seremala, nimetatua kero za jamii kwa kiasi kikubwa sana, ukiacha kazi kubwa kubwa ninazofanya, zile dharura jamii inazozipata natatua sana, mfano mtu amepoteza ufunguo wa mlango, mtu amevunja Chaga za kitanda huwa na wa Save sana.

Pia nimefunza wengi sana kazi yangu hii, kwa hesabu ya haraka sio chini ya vijana 70 wamepita mikononi mwangu na wengi wao wanaendelea na maisha ya ufundi wakiwa na familia.

Pia kwa sababu kazi yangu hii inahitaji miti kwaajili ya mbao, nipo kwenye mchakato wa kupanda miti isio pungua 1000 ndani ya miaka 5 .
 
Back
Top Bottom