Fani yako inakusaidiaje katika kutatua Kero za Jamii?

Fani yako inakusaidiaje katika kutatua Kero za Jamii?

Wengi huwa tunajifunza fani mbalimbali ili mwisho wa siku tuweze kutatua kero au changamoto za jamii; mfano:
  • Daktari atatatua kero za wagonjwa kwa kuwatibu.
  • Mwalimu atatatua kero za wajinga kwa kuwapa elimu na ujuzi.
  • Mzibua vyoo atatatua kero ya kuzagaa kwa maji taka na kuelekea kwenye mfumo wake.
  • n.k

Sasa tushirikishe kwa upande wako; fani yako inatatua kero ipi kwa jamii?, au unapokea tu mshahara na posho bila kutatua kero yoyote?
Wewe unafaida gani katika jamii?[emoji23]
 
Me n afsa ubashir natatua kero za vijana kwa kuwatengenezea mikeka yenye odd za kutosha kila siku na vijana wanafarijika na mm mtaani kwang huwa wana kauli yao wananiambia mungu aniweke miaka dahar sijui wanamaanisha nn
 
Jamii inaona mchango wako
 
Mimi ni nyange nyange Mr White natatua kero za madereva wazembe na wavunja sheria za barabarani nawasaidia kwa kuwachomoa afu mbili ya kubrashia viatu badala ya kuwalima mkeka wa afu 30.wananipongeza Sana na Mimi na wao tunaongea lugha moja
 
😀 😀 Hapo unasaidia au unaumiza, kwa nini usiwashauri tu bila kuchukua chochote?
 
Hapana si moja kwa moja. ya kwangu inawasaidia watoa maamuzi “Decision makers” wakija kuamua kwa usahihi kwa faida ya jamii basi nakuwa nimesaidia kutatua matatizo ya jamii.
 
Back
Top Bottom