Fanya yote ila usimzalie mtoto huyo mwanaume!

Fanya yote ila usimzalie mtoto huyo mwanaume!

Ndoa has never been a protection kwasababu naweza kukuoa Leo ukabeba mimba baada ya Mwaka Nika divorce na wewe Kikubwa ni maelewano na Security tu na wadada wajitahidi kuwa na Vipato ila kusema ndoa ndio ita guarantee safety yako kwake huo ni Uongo Mkubwa sana
Umewasilisha vizuri 💯 📌 , ni kweli ndoa inarasimisha tu mahusiano ila haikulindi.
Wanawake wawe na vipato na uwezo wa kiuchumi kabla ya kuzaa.
 
Mwanamke anayestahili hiyo treatment ni mwenye bikra Tu. Zaidi ya hapo mitambo lazima itestiwe
Kwahiyo mwenye bikra inamaanisha pia ana uwezo wa kuzaa na hakuna haja ya kutest? hiyo baiolojia yako umejifunzia wapi mkuu ?
 
Waambie kwanza wajitegemee kiuchumi.
Unataka mwanaume akulipie kodi, akupe pocket money na mahitaji yako yote,
unadhani akija kusema umzalie utaanzia wapi kukataa?
Sasa mkuu si itabidi huyo Mwanamke amjibu huyo Mwanaume kama anataka mtoto si aende kujitambulisha nyumba kwao mwanamke kisha wafunge ndoa.
 
Utakufa - hiyo ni fact na huwezi kuibadili.
Andaa mazingira, ikitokea umetangulia wewe, watoto wako wasiteseke.
“Unajua tatizo si kwamba wanaume wanakufa mapema – tatizo ni kwamba jamii imewatwika majukumu mazito, msongo wa mawazo, ukosefu wa emotional support, na bado hamuoni umuhimu wa kuwajali hadi wakishakufa. Badala ya kujadili lini tutakufa, kwa nini tusijadili namna ya kushirikiana kwa upendo, kusaidiana kupunguza pressure, na kujenga maisha yenye usawa? Huo mtazamo wa kungoja mwanaume afe ndio maisha yaanze ni wa kishenzi sana. Kama mwanaume anakufa mapema, siyo sababu ya kusherehekea au kupanga urithi – ni sababu ya kuumiza moyo na kujitafakari kama wanawake mnachangia vipi kuifanya dunia iwe better place kwa wote, si kwa kujiandalia tu maisha ya baada ya kifo chake.”
 
Mabinti, hasa nyie wadogo wa alfu mbili, hata akuambiaje, Usijichanganye kumzalia mtoto.
  1. Hakuna jukumu kubwa kwenye maisha zaidi ya kuzaa na kulea watoto. Mwanaume akikuambia bado hayuko tayari kukuoa ila anataka umzalie, huyo ni tapeli kama matapeli wengine tu.

  2. Kama huna kipato cha kueleweka na hajakuoa usizae kiholela. Na ukiolewa, hakikisha una shughuli ya kiuchumi ya kukuwezesha kuhudumia watoto wako ikitokea amefariki, amekutelekeza au mmeachana.

  3. Mapenzi kunoga na ahadi za kukuoa siyo sababu ya kubeba mimba. Wanaume wasio wababaifu, wenye kujua nafasi yao kwenye malezi wamebaki wachache sana ni kama bahati nasibu (Rejea hoja No 1 & 2).

  4. Zaa kwa ajili yako pale utakapokua tayari kiuchumi, kiakili na kimwili. Usizae ili uolewe au ili umtulize mwanaume, fahamu kuwa jukumu la malezi kwa kiasi kikubwa ni lako kama mama na yakitokea matatizo, atakayehangaika na mtoto / watoto ni wewe.

  5. Tumia uzazi wa mpango kuepuka mimba zisizotarajiwa kama hutaki basi tumia Kalenda au Condom (Kama hujui namna ya kujikinga kwa kutumia kalenda njoo hapa wamama tukusaidie na tukuelimishe.)

Ukitaka kujua huyo baba watoto wako mtarajiwa atakuwaje mkikosana na mna mtoto nenda kasome replies za wababa kwenye uzi wa jana wa waziri Dkt. Gwajima D - Jamii tuzungumze kuhusu baadhi ya wababa na matunzo kwa watoto - humo wamefunguka bila kuficha makucha yao.


Usiwe kama kenge mpaka uvuje damu ndiyo usikie - USIMZALIE BILA NDOA au UHAKIKA WA KUWEZA KUHUDUMIA MWANAO PEKE YAKO BILA YEYE.

Ni hayo tu, siku njema kwenu!


********
Naomba mtoe neno kwenye hili Lamomy , Leejay49 , nakwede97 , Demi , Aaliyyah , Mamndenyi , Bantu Lady , Ms R , leo dada , Numbisa , cocochanel , cocastic , Evelyn Salt , ephen_

Cc:
Wanawake wa JF:

waifu material * Mallerina
Atoto * Sister Abigail
realMamy ⋆ Qashy Lilith⋆ To yeye
Msweet ⋆ Chujio * Palina
Anastasia21 * ledada ⋆ Carleen * Midekoo
Mama Mwana * Hornet
SweetyCandy ⋆ Ellerie Bexley
Donatila *Jackcharty * Kelsea * Braying * Mrs Byesige
Acha kupangia watu maisha! Ishi maisha yako na wao maisha yao eboooh!
 
Hizi mada waislamu hazituhusu nilipokuwa naozeshwa walii/baba wa mtoto aliniambia kuwa

"Mzee/mwanangu nakuozesha binti yangu kwanzia sasa majukumu niliyokuwa nayafanya mimi sasa hivi ni majukumu yako kumvisha, kumlisha, na kuhakikisha anakaa makazi salama. Pia kama kuna malezi sikuyafanya mie jukumu ni la kwako kwanzia sasa kumlea katika malezi bora amjue Mungu na afanye ibada kwangu hiyo dhima nimeivua kuanzia leo"

Kwa kifungu hicho kinanifanya niwajibike 💯 kwa mtoto wa baba mkwe na kitokanacho na manii yangu nitakihudumia mpaka atakapofikia umri na yeye wa kuoa ama kuolewa kama nilivyo mkuta mtoto wa mama/baba mkwe na haya ni maagizo ya dini yetu na ni utaratibu mzuri kabisa wa kuishi
Inapendeza sana 🙏🙌
Tunashukuru Mungu kwa tamaduni na dini zinazoelekeza mahusiano, kujali majukumu na malezi bora kwa namna hii.
 
Una uwezo wa kudhani upo na mwanamke wa ndoa Sasa huyu mwanamke bado anakuwa akifikiria wakati mumewe atakapo kufa ku spenda mali za mmewe Hii ni dharau kubwa na fikra mbovu kabisa Badala ya kuishi maisha yenye heshima na kutafuta mafanikio anajishughulisha na mambo ya urithi na kufikiria kifo sijuh mfano akifa ! Hili si tabia ya mtu mwenye moyo wa uzalendo wala heshima bali ni tabia ya ubinafsi na wivu usio na kikomo
 
Very sad, yaani kuna wakati nilishindwa kuendelea machozi yakawa yanatoka nilikuwa natoka Bristol kuja London yaani we acha tu.
It's a very sad movie, hard to watch.
Ila nilichojifunza, tuwe wakarimu kwa wenye shida, lugha zetu ziwe rafiki. Yule bosi wake aisee alikuwa ananikera mno, na yule polisi. Ila U single mama mbaya sana.
Hatujui mtu anapitia nini, tuwe kind kwa wengine.
Usingle mama unatesa, yule mama kaenda jela na mtoto is gone 💔.
 
Back
Top Bottom