Fanya yote ila usimzalie mtoto huyo mwanaume!

Fanya yote ila usimzalie mtoto huyo mwanaume!

Mimi nafikiri wanawake tuzae watoto tukiwa na utayari, kuanzia huduma mpaka malezi..!!
Tusizae ili kumfurahisha mwanaume au kumfanya akuoe..!!

Hii kujipa mategemeo kwa mwanaume ambaye hujui kesho atakuwaje ni kujitafutia matatizo ambayo yatapelekea kushinda ustawi wa jamii..!!

Umeshindwa tumia kinga ili kuzuia kutesa watu ambao hawakuwaomba muwazae..!!
Nakazia ujumbe wako Lamomy
 
Kila nikitaka kuzaa nakumbana na hizi Post naishiwa PAWA
Tafuta hela mdogo wangu, hakikisha utaweza kumudu malezi ya huyo mtoto kabla hujazaa.

Zingatia ushauri wa Leo dada nimeupin 📌 ndiyo reply ya kwanza, na pia ukasome uzi wa waziri Gwajima, akili izidi kukukaa sawa.
 
Inapendeza sana 🙏🙌
Tunashukuru Mungu kwa tamaduni na dini zinazoelekeza mahusiano, kujali majukumu na malezi bora kwa namna hii.
Nashukuru pia, mtoto wa baba mkwe ananitii, ananiheshimu na ananisikiliza katika familia najiona kweli ni baba na nikichwa cha familia maana kila kitu mimi ndio napanga nikikwama ananishauri

Wote tumesoma na wote hatujaajiriwa nimemwambia tupambane tuone njia hii itakuwaje akasema sawa hatujawahi feli namshukuru Mungu.

Kiuhalisia ni kuwa mkiishi kwa malengo mengine tofauti na uchumi na pesa mapenzi yatadumu Sana tena mtaishi kwa raha hata kama hamna hata mia ya kula. Matakwa ya ndoa kwa uislamu ni kutimiza amri za Mungu kama takwa la kidini mkiishi humo hamna kitakacho halibika
 
Wewe una upwiru wa miaka mingapi?
Umeenda kuedit nyuzi yangu kujiambia unachotaka kusikia 🤣 au kweli wewe ni kenge 🤣
Sina upwiru,nimet#!!@!!mba jana usiku mzima nimemaliza bao sita za nguvu

Hapana sijaenda kuedit nyuzi yako na kujiambia ninavyotaka kusikia mkuu

Nimesoma nyuzi yako yote ndo nikaona sehemu niliyoinukuu wanaume umetuita kenge

HAPANA MIMI SIYO KENGE
 
Nyie wadada msikilizeni mwenzenu ana watoto 5 hapo alipo na ana.mimba changa.

Wewe kaa hapo usizae uje uzae uzeeni...

Mimi nawambia MA BINTI zaeni ila zaa ukijua nazaa kwa ajili yangu binafsi, nazaa kwasababu namuhitaji mtoto, nazaa kwasababu ni muda wangu umefika.

Huzai kwa ajili ya mwanaume
Humzaliii mwanaume
Huzaliii ndugu zake au ukoo wake

Kama ulivyopambana ukatafuta hela ukafungua biashara Yako, ukalipa kodi kwako,ukanunua vitu vya ndani,nk

Fahamu Ujauzito ni Jukumu kama hayo mengine na NI JUKUMU LAKO.

Jipange zako BINTI YANGU weka hela yako Binti angu, kisha Ukiona una ki Balance chako cha kukutunza kwa kipindi ulichojipangia.

BEBA MIMBA Yako, Mwanaume akikutunza hiyo ni BONUS ila usije zaaa kisa UMEAMBIWA kisa Mwanaume Kataka, Kisa unampenda unatamani umkamate kwa kumzalia.

Zaa Tu ikiwa ushajua MTOTO ni kitu unakihitaji.

Msimsikilize sana huyu mdada mtoa MADA mtazeeka Bila watoto na Sio SIFA una KIZAZI zaa ila TAMBUA kuzaaa/kulea ni JUKUMU LAKO.

Kadhalika na Wanaume hii iende vice versa pia.
Safi sana mkuu
 
“Unajua tatizo si kwamba wanaume wanakufa mapema – tatizo ni kwamba jamii imewatwika majukumu mazito, msongo wa mawazo, ukosefu wa emotional support, na bado hamuoni umuhimu wa kuwajali hadi wakishakufa.
Nina watoto wa kiume tu na nishawahi kuandikia kuhusu hii topiki miezi kadhaa iliyopita. Ipitie hapo chini.
Badala ya kujadili lini tutakufa, kwa nini tusijadili namna ya kushirikiana kwa upendo, kusaidiana kupunguza pressure, na kujenga maisha yenye usawa? Huo mtazamo wa kungoja mwanaume afe ndio maisha yaanze ni wa kishenzi sana.
Hakuna mtu ameongelea kungoja wanaume kufa, nimesema wanawake wawe na nguvu za kiuchumi na wawe tayari kulea watoto wakibaki peke yao kwa sababu yoyote ile including kifo.
Kama mwanaume anakufa mapema, siyo sababu ya kusherehekea au kupanga urithi – ni sababu ya kuumiza moyo na kujitafakari kama wanawake mnachangia vipi kuifanya dunia iwe better place kwa wote, si kwa kujiandalia tu maisha ya baada ya kifo chake.”
Hatujui tutaondoka lini, wote wanaume na wanawake tuandae mazingira ikitokea tumeondoka watoto wetu wasiteseke.
 
Hii reply ya leo dada naipin📌 hapa wasichana / wanawake wote muione.

📌📌
Kwangu mimi Nina mtazamo wa tofauti kidogo na nina misimamo yangu .......

Binti au mwanamke kwanza zaa ukiwa tayari ukihisi na kujua kabisa kwamba uko tayari kuzaa na kubeba majukumu bila kusumbua watu.....
Hapa namaanisha si kuzaa tu kufurahisha jamii, au unazaa kufurahisha bwana, au unazaa ili asikuache. Zaa ukiwa tayari na ukijua kabisa kwamba ukishazaa maisha yanabadilika completely jukumu kwa asilimia kubwa ni lako hata kama baba atahudumia fedha kaa ukijua kwa asilimia kubwa ya malezi yanakutegemea wewe mwenyewe.

Hawa wanaume hubadilika pindi mwanamke akizaa sababu ni nyingi mojawapo ni;

1. Malezi
Ukisha zaa malezi yanakutegemea hata kama tutapata dada wa kazi lakini ni lazima uwajibike hasa mtoto akiwa mdogo.

2. Usafi
Hapa ukisha zaa mwanamke kwanza Kuna kiharufu cha uzazi hili kuisha huchukua muda kidogo. Na harufu ya mtoto hii pia huchukua muda japo huisha lakini.

3. Huruma.
Baada ya kuzaa baadhi ya wanaume huona huruma na kuamua kuwa na mpango wa kando kipindi ambacho mwanamke ana uzazi au malezi. Sasa huruma hugeuka shubiri kwenye mahusiano kwani mwanaume anaweza kuzama huko mpaka ndoa au mahusiano kuvunjika.

4. Mabadiliko.
Mwanamke akishazaa Kuna mabadiliko hutokea na wengi kuanzia mabadiliko ya mwili, unene, ziwa kulegea, alama yaani stretch mark, urembo kwa baadhi ya wanawake kupungua na kupelekea mwanaume kukuona tofauti.

Sasa hapa binti/ mdogo wangu utakapo pata mtoto bila kuwa tayari utateseka sanaaa. Sababu utayari utakupa uvumilivu kuweza kuvumilia mabadiliko ya mtoto/ watoto kwani kila kitu kina raha na karaha zake.......
Ni vyema sana kuzaa ukiwa ndani ya ndoa kwani mwanaume anaweza kupokea mabadiliko na mkaweza kulea kwa amani na kufurahia uzao wenu.

Binti watoto changamoto na uzazi una changamoto nyingii mno usikubali kuwa single mother kirahisi ikitokea sawa.

Na binti kumbuka kuzaa sio lazima na kuolewa sio lazima.

Usiweke mitego ya kuolewa kwa kuwa wewe unataka kuolewa. Au kwa kuwa wewe ni jobless mwenzio anakazi ujitege either kwa mimba au madawa au kivyovyote ujifanye malaika dada hiyo ndoa utaachwa mchana kweupe na kubaki kuwa single mother na uanze kuona uchungu wa one hand.
Olewa na olewa na mtu ambaye Yuko tayari kwani akiwa tayari atakuvumilia kwa halisi zote na mabadiliko yote yatakayotokea kwenye maisha yenu.

Mimi sisapot mabinti kuzaa kwa fasheni, kuzaa wakiwa na umri mdogo , binti kuzaa kwa manufaa yake binafsi hilo suala anaye tumia zaidi ni binti.

Wanaume.
Hawa siwatetei na sina mengi ya kuongea juu yao kwa sababu.
Hakuna mwanaume anayeweza kupindua kwa mwanamke anayesimama katika nafasi yake na vitu vingi kwenye mahusiano hata ndoa kuwa imara inategemea mwanamke na nafasi yake alivyosimama.

Sasa wewe mpe utii, heshima , uvumilivu na upendo bila bila kusahau mizagamuano ya kutosha mpe mahaba mpe ufundi wako wote hata akipeleka kegeli zake huko nje kimoyoni akili kuwa wewe ndio kiboko yao.
Mpe utulivu mwanaume atatambua thamani yako na atakuthamini mengine yataenda bila kusahau maombi/ Dua kulingana na Imani yako maana Hawa kenge hawatabiliki.

Namalizia kwa kusema hivi nikiwa kama mama na kwenye ndoa nina miaka kumi na tatu.
Kuzaa sio lazima usizae kwa mihemuko eti kisa class mate zako wamezaa, sijui umri umeenda hapana kwa kweli maana huyo mtoto atakuwa nuksi tu kwako.

Na wale mabinti mlioko kwenye mahusiano na waume za watu au mahusiano ya muda mrefu eti mwanaume hataki ndoa anataka mzae kataa na usikubali na ukikubali hakikisha anakujengea na kukupa mradi endelevu utakaokuwezesha kulea na kusomesha mwanae haiwezekani binti usijaribu kubeba mizigo peke yako.

Mahusiano ni starehe na si karaha sasa kama ni starehe binti furahia na ikikuchosha acha sio lazima na hakikisha unachagua mtu sahihi wa kustarehe nae sio kila mtu. Usisahau mwili wako ni hekalu na hekaluni kunakaa vitu visafi na vitakatifu
Ndoa sio lazima olewa ukiwa tayari na si kwa sababu maana hizo sababu zikikosena ni lazima ndoa ivunjike.
Binti wa zamani yangu ni hayo.

📌📌

KATAA NDOA wanaendelea kupata credits
 
Una uwezo wa kudhani upo na mwanamke wa ndoa Sasa huyu mwanamke bado anakuwa akifikiria wakati mumewe atakapo kufa ku spenda mali za mmewe Hii ni dharau kubwa na fikra mbovu kabisa Badala ya kuishi maisha yenye heshima na kutafuta mafanikio anajishughulisha na mambo ya urithi na kufikiria kifo sijuh mfano akifa ! Hili si tabia ya mtu mwenye moyo wa uzalendo wala heshima bali ni tabia ya ubinafsi na wivu usio na kikomo
Sijui kwanini watu mnapata makasiriko kuhusu hili. Hakuna mtu anakitaka kifo wala anaombea watoto wake wafiwe na mzazi.

Hapa tunawashauri wanawake wajizatiti kulea watoto peke yao ikitokea wamepatwa na changamoto yoyote, iwe kuachana, kutelekezwa au mzazi mwenzake kutangulia mbele za haki.

Sasa wapi kwenye huu uzi wangu nimeongelea mambo ya urithi au kusubiri mume afe? Hebu kasome tena!
 
Nashukuru pia, mtoto wa baba mkwe ananitii, ananiheshimu na ananisikiliza katika familia najiona kweli ni baba na nikichwa cha familia maana kila kitu mimi ndio napanga nikikwama ananishauri

Wote tumesoma na wote hatujaajiriwa nimemwambia tupambane tuone njia hii itakuwaje akasema sawa hatujawahi feli namshukuru Mungu.

Kiuhalisia ni kuwa mkiishi kwa malengo mengine tofauti na uchumi na pesa mapenzi yatadumu Sana tena mtaishi kwa raha hata kama hamna hata mia ya kula. Matakwa ya ndoa kwa uislamu ni kutimiza amri za Mungu kama takwa la kidini mkiishi humo hamna kitakacho halibika
Asanteni kwa kuwa mfano mzuri, inapendeza sana.
Ikawe heri kwenu, muendelee kudumu na kuwa na furaha kwenye ndoa yenu.
 
Sijui kwanini watu mnapata makasiriko kuhusu hili. Hakuna mtu anakitaka kifo wala anaombea watoto wake wafiwe na mzazi.

Hapa tunawashauri wanawake wajizatiti kulea watoto peke yao ikitokea wamepatwa na changamoto yoyote, iwe kuachana, kutelekezwa au mzazi mwenzake kutangulia mbele za haki.

Sasa wapi kwenye huu uzi wangu nimeongelea mambo ya urithi au kusubiri mume afe? Hebu kasome tena!
Ni kweli ujaongea lakini mtazamo mkubwa kwa wanawake na uwona hivyo
 
Back
Top Bottom