Hii reply ya
leo dada naipin📌 hapa wasichana / wanawake wote muione.
📌📌
Kwangu mimi Nina mtazamo wa tofauti kidogo na nina misimamo yangu .......
Binti au mwanamke kwanza zaa ukiwa tayari ukihisi na kujua kabisa kwamba uko tayari kuzaa na kubeba majukumu bila kusumbua watu.....
Hapa namaanisha si kuzaa tu kufurahisha jamii, au unazaa kufurahisha bwana, au unazaa ili asikuache. Zaa ukiwa tayari na ukijua kabisa kwamba ukishazaa maisha yanabadilika completely jukumu kwa asilimia kubwa ni lako hata kama baba atahudumia fedha kaa ukijua kwa asilimia kubwa ya malezi yanakutegemea wewe mwenyewe.
Hawa wanaume hubadilika pindi mwanamke akizaa sababu ni nyingi mojawapo ni;
1.
Malezi
Ukisha zaa malezi yanakutegemea hata kama tutapata dada wa kazi lakini ni lazima uwajibike hasa mtoto akiwa mdogo.
2.
Usafi
Hapa ukisha zaa mwanamke kwanza Kuna kiharufu cha uzazi hili kuisha huchukua muda kidogo. Na harufu ya mtoto hii pia huchukua muda japo huisha lakini.
3.
Huruma.
Baada ya kuzaa baadhi ya wanaume huona huruma na kuamua kuwa na mpango wa kando kipindi ambacho mwanamke ana uzazi au malezi. Sasa huruma hugeuka shubiri kwenye mahusiano kwani mwanaume anaweza kuzama huko mpaka ndoa au mahusiano kuvunjika.
4.
Mabadiliko.
Mwanamke akishazaa Kuna mabadiliko hutokea na wengi kuanzia mabadiliko ya mwili, unene, ziwa kulegea, alama yaani stretch mark, urembo kwa baadhi ya wanawake kupungua na kupelekea mwanaume kukuona tofauti.
Sasa hapa binti/ mdogo wangu utakapo pata mtoto bila kuwa tayari utateseka sanaaa. Sababu utayari utakupa uvumilivu kuweza kuvumilia mabadiliko ya mtoto/ watoto kwani kila kitu kina raha na karaha zake.......
Ni vyema sana kuzaa ukiwa ndani ya ndoa kwani mwanaume anaweza kupokea mabadiliko na mkaweza kulea kwa amani na kufurahia uzao wenu.
Binti watoto changamoto na uzazi una changamoto nyingii mno usikubali kuwa single mother kirahisi ikitokea sawa.
Na binti kumbuka kuzaa sio lazima na kuolewa sio lazima.
Usiweke mitego ya kuolewa kwa kuwa wewe unataka kuolewa. Au kwa kuwa wewe ni jobless mwenzio anakazi ujitege either kwa mimba au madawa au kivyovyote ujifanye malaika dada hiyo ndoa utaachwa mchana kweupe na kubaki kuwa single mother na uanze kuona uchungu wa one hand.
Olewa na olewa na mtu ambaye Yuko tayari kwani akiwa tayari atakuvumilia kwa halisi zote na mabadiliko yote yatakayotokea kwenye maisha yenu.
Mimi sisapot mabinti kuzaa kwa fasheni, kuzaa wakiwa na umri mdogo , binti kuzaa kwa manufaa yake binafsi hilo suala anaye tumia zaidi ni binti.
Wanaume.
Hawa siwatetei na sina mengi ya kuongea juu yao kwa sababu.
Hakuna mwanaume anayeweza kupindua kwa mwanamke anayesimama katika nafasi yake na vitu vingi kwenye mahusiano hata ndoa kuwa imara inategemea mwanamke na nafasi yake alivyosimama.
Sasa wewe mpe utii, heshima , uvumilivu na upendo bila bila kusahau mizagamuano ya kutosha mpe mahaba mpe ufundi wako wote hata akipeleka kegeli zake huko nje kimoyoni akili kuwa wewe ndio kiboko yao.
Mpe utulivu mwanaume atatambua thamani yako na atakuthamini mengine yataenda bila kusahau maombi/ Dua kulingana na Imani yako maana Hawa kenge hawatabiliki.
Namalizia kwa kusema hivi nikiwa kama mama na kwenye ndoa nina miaka kumi na tatu.
Kuzaa sio lazima usizae kwa mihemuko eti kisa class mate zako wamezaa, sijui umri umeenda hapana kwa kweli maana huyo mtoto atakuwa nuksi tu kwako.
Na wale mabinti mlioko kwenye mahusiano na waume za watu au mahusiano ya muda mrefu eti mwanaume hataki ndoa anataka mzae kataa na usikubali na ukikubali hakikisha anakujengea na kukupa mradi endelevu utakaokuwezesha kulea na kusomesha mwanae haiwezekani binti usijaribu kubeba mizigo peke yako.
Mahusiano ni starehe na si karaha sasa kama ni starehe binti furahia na ikikuchosha acha sio lazima na hakikisha unachagua mtu sahihi wa kustarehe nae sio kila mtu. Usisahau mwili wako ni hekalu na hekaluni kunakaa vitu visafi na vitakatifu
Ndoa sio lazima olewa ukiwa tayari na si kwa sababu maana hizo sababu zikikosena ni lazima ndoa ivunjike.
Binti wa zamani yangu ni hayo.
📌📌
Kumbe kuna vita ya kijinsia na wengine hata hatujui, aiseeh 🤦♀️! Kumbe hii thread sio uwanja wa vita?
www.jamiiforums.com