Fanya yote ila usimzalie mtoto huyo mwanaume!

Fanya yote ila usimzalie mtoto huyo mwanaume!

Wanawake sijui huwa mna akili za namna gani asee, sasa wewe unaona ndoa ndio kitu kinachoweza kumzuia mwanaume fedhuli asiyejali majukumu yake kukuletea mapicha picha hapo mbele??!!! No wonder mkiingia kwenye ndoa huwa mnaanza kuota mapembe kwa kuona mmemaliza yote, na hapa ndio wanaume na sisi tunawonyesha kuwa huu mchezo hauhitaji hasira.

Hapa ndio huwa naona nilichukua uamuzi sahihi wakuachana na masuala ya kutaka kuoa, kuoa kwa enzi hizi ni sawa na kufuga kijini kidogo ndani yako kinacho kuangamiza taratibu. Unaingia kwenye ndoa na mtua anayewaza 'Je ukifariki' huu ni ushetani wa hali ya juu sana
Ndio ugundue akili za huyu mtu zilivyo fupi. Ni ma emotions tu kayaweka hapa
 
Kwanini wanawake wanafikiri wanatuzalia watoto? Mtoto akizaliwa sio wa baba pakee, ni wa wote. Kwani kwenye maisha ndoa ni ya lazima? Cha muhimu mwanamme atoe matumizi ya mtoto na mama
Nakubaliana na wewe cha muhimu mwanaume ahudumie mtoto.
Ila pia ni vizuri kufahamu familia ya mtu unayezaa naye siyo kukutana vichochoroni tu bila kufahamiana vizuri.
 
Ukitaka kuzaa Anza kujipanga kiuchumi hata kama huyo mwanaume atageuza shingo yake wewe utakua umesimama vizur
Tatizo wanawake akili zetu ni za kuambiwa Kuna kale kausemi et nikimzalia atanioa au nikimzalia atakua ananipa hela aloooh zaa huyo mtoto utalia kilio zaid ya huyo mtoto
 
Hawa wanaume wa siku hizi ni .......................................................... (wape jina unalofikiri na linawafaa).
Mabinti, hasa nyie wadogo wa alfu mbili, hata akuambiaje, Usijichanganye kumzalia mtoto.
  1. Hakuna jukumu kubwa kwenye maisha zaidi ya kuzaa na kulea watoto. Mwanaume akikuambia bado hayuko tayari kukuoa ila anataka umzalie, huyo ni tapeli kama matapeli wengine tu.

  2. Kama hajaja kwenu kukuchumbia, hajakuoa usizae kiholela. Na ukiolewa, hakikisha una shughuli ya kiuchumi ya kukuwezesha kuhudumia watoto wako ikitokea amefariki, amekutelekeza au mmeachana.

  3. Mapenzi kunoga na ahadi za kukuoa siyo sababu ya kubeba mimba. Wanaume wasio wababaifu, wenye kujua nafasi yao kwenye malezi wamebaki wachache sana ni kama bahati nasibu (Rejea hoja No 1 & 2).

  4. Tumia uzazi wa mpango kuepuka mimba zisizotarajiwa kama hutaki basi tumia Kalenda au Condom (Kama hujui namna ya kujikinga kwa kutumia kalenda njoo hapa wamama tukusaidie na tukuelimishe.)

Ukitaka kujua huyo baba watoto wako mtarajiwa atakuwaje mkikosana na mna mtoto nenda kasome replies za wababa kwenye uzi wa jana wa waziri Dkt. Gwajima D - Jamii tuzungumze kuhusu baadhi ya wababa na matunzo kwa watoto - humo wamefunguka bila kuficha makucha yao.


Usiwe kama kenge mpaka uvuje damu ndiyo usikie - USIMZALIE BILA NDOA au UHAKIKA WA KUWEZA KUHUDUMIA MWANAO PEKE YAKO BILA YEYE.

Ni hayo tu, siku njema kwenu!


********
Naomba mtoe neno kwenye hili Lamomy , Leejay49 , nakwede97 , Demi , Aaliyyah , Mamndenyi , Bantu Lady , Ms R , leo dada , Numbisa , cocochanel , cocastic , Evelyn Salt , ephen_
Kwani aliye kwambia akikuowa hawezi kukuacha na kukutelekeza na watoto wako ni nani ? Mimi nimeona ndowa zilizo dumi miaka mitatu na watoto watatu na mme akasepa. Mke akabaki analea. Ushauri mzuri ni kuwambia wanawake wajuwe suala la kulea watoto ni jukumu la wazazi wawili . Wahakikishe kabla ya kuolewa wanajenga uwezo wao wa kiuchumi kwanza. Ili waingie kwenye mahusiano kama equal partners. Hakuna wmanaume anaweza kumwacha mwanamke anaye saidia kuongeza kipato cha familia. Ukiona mwanaume anacha familia ujuwe amepinga mahesabu akaona kuna faida kuacha kuliko kuendela na majukumu.
 
Hivi,kuna mwanamke huwa anasaidia kulea mtoto (tukiacha kumnyonyesha)
Mwanamke hasaidii analea, tukiachana na kutoa hela, nyie wanaume mnafanya nini kwenye malezi.?
zaidi ya kulazimisha mwanaume awajibike kwa kila kitu?
Kwenye kuwajibika kiuchumi, mfano: ukiamriwa na ustawi ulipe 100,00 ya matumizi ni kweli unaamini malazi, mavazi na chakula kwa mwezi mtoto wako anatumia 100K au kiasi kilichobaki kinatoka kwa mama yake?
 
Mwanamke hasaidii analea, tukiachana na kutoa hela, nyie wanaume mnafanya nini kwenye malezi.?

Kwenye kuwajibika kiuchumi, mfano: ukiamriwa na ustawi ulipe 100,00 ya matumizi ni kweli unaamini malazi, mavazi na chakula kwa mwezi mtoto wako anatumia 100K au kiasi kilichobaki kinatoka kwa mama yake?
-Labda neno "KULEA" maana yake ni nini?
-Ni mtoto gani kwenye nchi yetu ambayo wastani kamili wa matumizi ya familia ni nusu dola(US)ieTsh.1300 kuna mtoto mdogo mmoja atumie zaidi ya familia yote?
 
Kuna wengine tuliwapa ujauzito !tukabeba na kuishi NAO na kuhakikisha watoto wana kwao!lakini Bado tulipigwa tukio hadi tukaamua tuoe tena japo wa mwanzo hatumuachi !tunamwachia mungu TU awe name coz ni wa kwake alimuumba yeye!!

Usifanye generalization kabisa!!

Tupo tuliofunga safari ndeeefu yenye milima na mabonde plus Kona nyingi Hadi hofu kwamba Bus linaweza kuanguka!tukifuata mtoto na Mama yake!baadae tuliambulia majibu kama haya:-

1.Unafikiri Kuna kitu Gani Cha maaana ninachobembeleza kwako!

2.najua no akaunti yangubndio inakupa shida coz uliishika sana (Hakuja na akaunti yenye Hela kazi aliipata akiwa na Mimi)

3.ukipataga mwanamke nendaga tu uniache na wanangu hapa (baada ya kuona tumejenga nyumba ya kuishi)

4.Hivi ukisikia natoka na MTU Fulani hivi utafanya nini kwamfano!!?kumbe tayari ana mtu na wanaaljenga pamoja Kwa siri!!

5.kuwa na mahusiano na..........(kazi yangu) ni shida hawana hela kabisa!wakatinndio KAZI iliyomlisha kabla hajapata kazi wakati nimemleta!!

6."hahudumii familia anahonga tu!Kodi zote mnioe Mimi"!!! Wakati kiwanja nilinunua na kujenga tulishirikiana kiasi fulani ndio kimekua pa kwake na aibu kibao nazoa Kwa wapangaji ambao ni Mimi ndio niliwapokea kitambo!!
Kwanza pole na changamoto za mahusiano.

Pili, wanawake si malaika, wapo wengi wa hovyo na wanaofanya mambo ya ajabu ambayo hayakubaliki na hatuwezi kuyatetea.
Mnapokua mnaandika nyuzi hizi muwe mnafikiria na upande was pili na ujiulize swali "kama ungempata Punda mwaminifu was kubeba hatma ya maisha Yako na watoto wako ungemheshimu baada ya kukufikisha mwisho wa safari yako au mafanikio!!!?Hicho ndicho kitendawili ambacho wanawake wengi wameshindwa kukitegua nacho ni "KUSHINDWA KUYAISHI MAFANIKIO BAADA YA KUYAPATA!!!!!UBINAFSI HUINGIA!!
Huu uzi si wa generalization, bali ushauri kwa mabinti wadogo kutozaa hovyo hovyo.
Story ya mshikaji hapa namsikiliza!
Mwambie mshikaji, hata kama anavunga ujumbe tumeupata 😂
 
🤣🤣🤣🤣🤣 daaah
Ujue nini..

Kesho asbhi kuna maza anakuja getto ..
Huyu maza namkanda kesho najua nikisha muonjesha tuu atataka kila alhamis utamu anyway mi takula tuuu kila day..

Mbele za watu tunaitana kaka na dada ila deep down anataka....

Kuhusu ushauri wako kwa vijana ni kweli kabisa aiseeee wasiwazalie hiyo haitakiwi
Amempa kipochi Cha nini Sasa? Maadamu ametanua miguu mimba itapita hapohapo, washaur wasitoe kipochi Hadi waolewe na Wala sio mwanaume kuja nyumbani kuchumbia, Bali waolewe kabisa hapo watakuwa wamefanikiwa vinginevyo hamna kitu pia maisha yanawasumbua wengi anaona labda akimzalia mambo yatanoga zaid, kuweni na kampeni hii, Hakuna ndoa hakuna tendo la Ndoa, Kataa Zinaa. Imeisha hiyo.
 
Usizae mtoto kama huwezi kumhudumia mwenyewe.
Ndoa sio guarantee ya kuhudumiwa hakikisha unafanya kazi sana.
Ndoa inaweza kukupa guarantee ya kusikilizwa kuhusu mtoto japo sio 100%
Asante mamie, sina cha kuongezea, wazingatie 👆💯
giphy 22.GIF
 
Hii vita ya kijinsia inavyoenezwa ni kama kuna mfumo unaandaliwa, au maisha mapya yanaandaliwa. Sioni hata ni kwanini kuna hiyo vita. Ukishajua kwanini ulizaliwa uwe mwanamke au mwanaume, hutashabikia hii vita inavyopiganwa mitandaoni.
Kumbe kuna vita ya kijinsia na wengine hata hatujui, aiseeh 🤦‍♀️!
 
Nyie wadada msikilizeni mwenzenu ana watoto 5 hapo alipo na ana.mimba changa.

Wewe kaa hapo usizae uje uzae uzeeni...

Mimi nawambia MA BINTI zaeni ila zaa ukijua nazaa kwa ajili yangu binafsi, nazaa kwasababu namuhitaji mtoto, nazaa kwasababu ni muda wangu umefika.

Huzai kwa ajili ya mwanaume
Humzaliii mwanaume
Huzaliii ndugu zake au ukoo wake

Kama ulivyopambana ukatafuta hela ukafungua biashara Yako, ukalipa kodi kwako,ukanunua vitu vya ndani,nk

Fahamu Ujauzito ni Jukumu kama hayo mengine na NI JUKUMU LAKO.

Jipange zako BINTI YANGU weka hela yako Binti angu, kisha Ukiona una ki Balance chako cha kukutunza kwa kipindi ulichojipangia.

BEBA MIMBA Yako, Mwanaume akikutunza hiyo ni BONUS ila usije zaaa kisa UMEAMBIWA kisa Mwanaume Kataka, Kisa unampenda unatamani umkamate kwa kumzalia.

Zaa Tu ikiwa ushajua MTOTO ni kitu unakihitaji.

Msimsikilize sana huyu mdada mtoa MADA mtazeeka Bila watoto na Sio SIFA una KIZAZI zaa ila TAMBUA kuzaaa/kulea ni JUKUMU LAKO.

Kadhalika na Wanaume hii iende vice versa pia.
 
Nyie wadada msikilizeni mwenzenu ana watoto 5 hapo alipo na ana.mimba changa.

Wewe kaa hapo usizae uje uzae uzeeni...

Mimi nawambia MA BINTI zaeni ila zaa ukijua nazaa kwa ajili yangu binafsi, nazaa kwasababu namuhitaji mtoto, nazaa kwasababu ni muda wangu umefika.

Huzai kwa ajili ya mwanaume
Humzaliii mwanaume
Huzaliii ndugu zake au ukoo wake

Kama ulivyopambana ukatafuta hela ukafungua biashara Yako, ukalipa kodi kwako,ukanunua vitu vya ndani,nk

Fahamu Ujauzito ni Jukumu kama hayo mengine na NI JUKUMU LAKO.

Jipange zako BINTI YANGU weka hela yako Binti angu, kisha Ukiona una ki Balance chako cha kukutunza kwa kipindi ulichojipangia.

BEBA MIMBA Yako, Mwanaume akikutunza hiyo ni BONUS ila usije zaaa kisa UMEAMBIWA kisa Mwanaume Kataka, Kisa unampenda unatamani umkamate kwa kumzalia.

Zaa Tu ikiwa ushajua MTOTO ni kitu unakihitaji.

Msimsikilize sana huyu mdada mtoa MADA mtazeeka Bila watoto na Sio SIFA una KIZAZI zaa ila TAMBUA kuzaaa/kulea ni JUKUMU LAKO.

Kadhalika na Wanaume hii iende vice versa pia.
Sina Watoto 5 ila ushauri wako ni mzuri sana 💯📌, wazae kwa ajili yao na wawe na uwezo wa kuhudumia watoto wao bila kutegemea wanaume, maana wengi hawaeleweki.
 
Back
Top Bottom