Fanya yote ila usimzalie mtoto huyo mwanaume!

Fanya yote ila usimzalie mtoto huyo mwanaume!

Nimeiona, very sad 😢😔
Mtoto mgonjwa, umaskini umepitiliza mpaka mtu anapata mental breakdown.
Very sad, yaani kuna wakati nilishindwa kuendelea machozi yakawa yanatoka nilikuwa natoka Bristol kuja London yaani we acha tu. Ila nilichojifunza, tuwe wakarimu kwa wenye shida, lugha zetu ziwe rafiki. Yule bosi wake aisee alikuwa ananikera mno, na yule polisi. Ila U single mama mbaya sana.
 
Kwani aliye kwambia akikuowa hawezi kukuacha na kukutelekeza na watoto wako ni nani ? Mimi nimeona ndowa zilizo dumi miaka mitatu na watoto watatu na mme akasepa. Mke akabaki analea.
Ni kweli ndoa siyo guarantee, ila ukijizuia kuzaa mpaka uolewe unakua umerasimisha mahusiano na unafahamu familia ya unayezaa naye (japo haitokusaidia kwenye malezi mwenzako akiondoka.) Sisi watu wazima tuliopitia mambo ya vifo na mirathi tunajua pia umuhimu wa ndoa yakikutokea matatizo kama ya kufiwa (japo kwenye huu uzi watu hawataki kusikia kwamba wanaweza kudondoka muda wowote na kuacha watoto wao wakihangaika).
Ushauri mzuri ni kuwambia wanawake wajuwe suala la kulea watoto ni jukumu la wazazi wawili . Wahakikishe kabla ya kuolewa wanajenga uwezo wao wa kiuchumi kwanza. Ili waingie kwenye mahusiano kama equal partners.
Huu ushauri mzuri na nimeutoa pia, nakubaliana na wewe asilimia 💯
Hakuna wmanaume anaweza kumwacha mwanamke anaye saidia kuongeza kipato cha familia. Ukiona mwanaume anacha familia ujuwe amepinga mahesabu akaona kuna faida kuacha kuliko kuendela na majukumu.
Hii pia ni kweli kabisa 💯💯📌
 
Wanawake sijui huwa mna akili za namna gani asee, sasa wewe unaona ndoa ndio kitu kinachoweza kumzuia mwanaume fedhuli asiyejali majukumu yake kukuletea mapicha picha hapo mbele??!!! No wonder mkiingia kwenye ndoa huwa mnaanza kuota mapembe kwa kuona mmemaliza yote, na hapa ndio wanaume na sisi tunawonyesha kuwa huu mchezo hauhitaji hasira.

Hapa ndio huwa naona nilichukua uamuzi sahihi wakuachana na masuala ya kutaka kuoa, kuoa kwa enzi hizi ni sawa na kufuga kijini kidogo ndani yako kinacho kuangamiza taratibu. Unaingia kwenye ndoa na mtua anayewaza 'Je ukifariki' huu ni ushetani wa hali ya juu sana
Sawa sawa kiongozi wanadai Sisi ndo tunaanza kufa
 
Mimi baba yangu alikua na wanawake watano, watoto 28. Kila mwanamke alikua na jukumu la kulea watoto wake. Sijwahi kusikia malalamiko yoyote kwa mzee kwamba hahudumii watoto. Kuna majukumu ya mzee na majukumu ya akina mama.
Wazee wa zamani hao, akioa analeta mke kwenye boma na anampa nyumba na mashamba ya kulima. Kila mama na watoto wake wanalima, wanafuga na wanajihudumia.

Aina hiyo ya maisha ilijitosheleza kulingana na mazingira, ila kwa sasa, hasa huku mjini utawezaje hayo.
 
Back
Top Bottom