Farhan: Siku ya mwisho career ya Fei itakua judged kwa vikombe na Tuzo Binafsi

Farhan: Siku ya mwisho career ya Fei itakua judged kwa vikombe na Tuzo Binafsi

THE FIRST BORN

JF-Expert Member
Joined
Apr 24, 2019
Posts
2,224
Reaction score
4,472
Niliongea hapa na watu mkaleta Njaa zenu coz Watanzania wengi tunatamaa sana na tunawaza hela sana na ndio maana hata viongozi vijana nao wamejaa Rushwa because wanawaza pesa tu wakipata nafasi wapige pesa tu.

Farhan kasema nilichosema kwenye uzi wangu niliondika hapa leo

Screenshot_20240603-182517_X.jpg
Pia soma
- Mchezaji yeyote duniani hutafuta vitu viwili tu, Kucheza na kushinda Makombe
 
Niliongea hapa na watu mkaleta Njaa zenu coz watanzania wengi tunatamaa sana na tunawaza hela sana..na ndio maana hata viongozi vijana nao wamejaa Rushwa because wanawaza pesa tu wakipata nafasi wapige pesa tu...
Acheni chuki zenu kwa huyo kijana, vikombe na medali bila hela vinakusaidia nini? Chukua vikombe wewe ibaki masikini itatosha lakini sio kumpangia mwingine
 
Yani unaweza ukawa unachukua vikombe na huna maisha? Acheni kukuza mambo
Fei alivyokuwa Yanga unadhani alikuwa hapati vikombe?, mbona alivikataa akatafuta maisha kwanza.

Vikombe ni bonus, ila fedha ndo kitu cha kwanza.

Mfano Denis Nkane ana vikombe ila hawezi mfikia maisha Suleiman Sopu ambaye hana kikombe.
 
Feisal ameboresha kile alichokua anapokea na sio kwamba hana maisha. Mimi nimesimamia hapo kama hujanielewa.
 
Nitajie vikombe vinamsaidia nini mchezaji asiye na maisha?
We jamaa vikombe ndivyo vinaleta pesa na bonus kibao.

Tuzo binafsi pia huleta pesa na hizo tuzo zenyewe ni pesa ukiamua kuziuza.

Kina Ronaldo na Messi kawafuatilie UEF zimewapaje hela pamoja na LALIGA.
 
Niliongea hapa na watu mkaleta Njaa zenu coz watanzania wengi tunatamaa sana na tunawaza hela sana..na ndio maana hata viongozi vijana nao wamejaa Rushwa because wanawaza pesa tu wakipata nafasi wapige pesa tu...
Mkuu, mbona umeikuza sana kauli ya Farhan? Kwani yeye ana uzito gani hadi kila anachowaza kuhusu soka kiwe sahihi?

Yeye si mtangazaji tu wa Clouds FM? Si mtangazaji tu kama Baba Levo na Mwijaku? Tusiwakuze sana hawa watu kwa vile wako redioni.

Hata wao wakati mwingine huwa na mawazo ya kipuuzi tu yanayopaswa kupuuzwa kama maoni mengine ya kipuuzi.

Nashauri, tuwe na kiasi na hawa watu. Tusijimalize kiasi hiki.

Ova
 
We jamaa vikombe ndivyo vinaleta pesa na bonus kibao.
Tuzo binafsi pia huleta pesa na hizo tuzo zenyewe ni pesa ukiamua kuziuza.
Kina Ronaldo na Messi kawafuatilie UEF zimewapaje hela pamoja na LALIGA.
Unajua mkataba wa Messi akiwa Barcelona, kipengele kimojawapo kilihitaji yeye kuwa mchezaji anayelipwa fedha nyingi kuliko wacheza mpira kote duniani.

Pia Cr7 mshahara wake ulikuwa unazidiwa na Messi tu duniani, hivyo mataji tu hayatoshi kukufanya upate fedha nyingi.

Tuchukue mfano wa ligi yetu, kabla ya Azam kutia mpunga bingwa wa ligi alikuwa anazawadiwa 100M.

Sasa hiyo 100M unadhani kuna bonus ya kufika 3M kwa kila mchezaji na benchi la ufundi?.

Kikubwa makombe yaambatane na cash ndefu siyo makombe kibao mshahara kasungura.

Hata wachezaji wengi wanaosema wanahitaji makombe, ukifuatilia kwa undani hawafuati makombe pekee, bali utakuta mpunga anaoenda kulipwa kama mshahara ni mkubwa kuliko ule wa awali.
 
Mchezaji gani hapa duniani amewahi chagua vikombe akaacha fedha?
Kylian Mbape amekataa mabilioni ya hela kwa kukataa kwenda Uarabuni msimu uliopita, kama alivyofanya mchezaji wenzake Neymar! Na badala yake ameona asaini Real Madrid msimu huu ili kuchukua zaidi makombe na tuzo binafsi.
 
Unajua mkataba wa Messi akiwa Barcelona, kipengele kimojawapo kilihitaji yeye kuwa mchezaji anayelipwa fedha nyingi kuliko wacheza mpira kote duniani...
Mbona hauwi specific!?

Kwani Feisal alikua halipwi Yanga?

Bonus za Champions league alikua hapati?

Bonus za makombe alikua hapati?

Kwani Feisal alikua maskini alivyokua Yanga?

Ulitakiwa useme kuongezeka kwa ukwasi,ila sio kuunasibisha umasikini/ukapuku moja kwa moja.

Maana kwa kauli ulizoongea ni kana kwamba vikombe havina thamani kabisa.
 
Back
Top Bottom