Farhan: Siku ya mwisho career ya Fei itakua judged kwa vikombe na Tuzo Binafsi

Farhan: Siku ya mwisho career ya Fei itakua judged kwa vikombe na Tuzo Binafsi

angekuwa anacheza ulaya sawa mana mataji ya kule yana hadhi zaidi ila kwa bongo apa cha kwanza ni mshiko.

pesa na ubingwa wa ligi ya Tanzania bara.. bora pesa.
Kama ishu ni pesa tu mbona Dogo alisepa kuvalishwa medali? Alichukia nin?
 
Vikombe vinakusaidia nini ukiwa kapuku?, hivi huko shuleni mlienda kusomea ujinga?
vikombe ndivyo vitakujengea CV ya kupata huo mkwanja,fei angeenda huko azam au hata timu za nje kwa mkwanja mrefu.
 
Kylian Mbape amekataa mabilioni ya hela kwa kukataa kwenda Uarabuni msimu uliopita, kama alivyofanya mchezaji wenzake Neymar! Na badala yake ameona asaini Real Madrid msimu huu ili kuchukua zaidi makombe na tuzo binafsi.
Kuna kitu tunapaswa kuelewa, kuna kuchukua hela nyingi kwa mara chache na kuchukua hela chache kwa mara nyingi.

Kingine, Mbape anajua kama hiyo hela ya Uarabuni anaweza kuipata baada ya kutoka Real Madrid, na Ulaya kwa ujumla.

Ila hatoweza kuipata hela ya Real Madrid baada ya kutoka Uarabuni.

Ova
 
Kylian Mbape amekataa mabilioni ya hela kwa kukataa kwenda Uarabuni msimu uliopita, kama alivyofanya mchezaji wenzake Neymar! Na badala yake ameona asaini Real Madrid msimu huu ili kuchukua zaidi makombe na tuzo binafsi.
Huyo makombe anayo, ila anatafuta ile tuzo binafsi ya wateule wachache wenye vitu vya ziada.

Ballon d'or ndo anaitafuta.
Signing bonus anayopewa na Madrid ni £150M, kiasi ambacho PSG hawakumpa, pia haki ya picha amepewa 80% kitu ambacho hakijawahi tokea pale Madrid.

Ukiangalia yote hayo yameambatana na mpunga uliochangamka.

Sasa hebu tuachane na hao wateule wachache ambao hawafiki watano duniani, tujikite kwenye kundi la kawaida la wengi, naomba uniambie mchezaji aliyeamua kupunguza maslahi akiwa kwenye peak ya kiwango chake akaamua kufuata makombe?
 
Huyo makombe anayo, ila anatafuta ile tuzo binafsi ya wateule wachache wenye vitu vya ziada.

Ballon d'or ndo anaitafuta.
Signing bonus anayopewa na Madrid ni £150M, kiasi ambacho PSG hawakumpa, pia haki ya picha amepewa 80% kitu ambacho hakijawahi tokea pale Madrid...
Mrisho Halfan Ngassa aka Uncle, alikataa mkwanja mrefu wa kwenda kucheza Al Merreikh ya Sudan akitokea Azam, kwa lengo la kubakia Yanga.
 
Mbona hauwi specific!?
Kwani Feisal alikua halipwi Yanga?
Bonus za Champions league alikua hapati?
Sijasema vikombe havina thamani, bali nimesema vikombe viwe direct proportional na maslahi.

Kwa mfano pale Yanga Fei tuseme kwa mwaka mshahara na bonuses zote alikuwa anapata tuchukulie 50M na vikombe juu, halafu pale Azam anapata 150M ila hana kikombe.

Kwa hesabu hiyo kimaisha tunasema cash kwanza vikombe vitafuata. Ila kuna wachezaji kama Aziz vikombe vinawiana na maslahi, mtu kama huyo ruksa kudumu hapo ingawa na yeye anaweza akageuka kama Mayele akachagua cash akaacha vikombe.
 
Mrisho Halfan Ngassa aka Uncle, alikataa mkwanja mrefu wa kwenda kucheza Al Merreikh ya Sudan akitokea Azam, kwa lengo la kubakia Yanga.
Lakini baadae ameishia kulia lia mitandaoni kuwa hali yake mfukoni si njema.

Wakati huo huo kuna mchezaji kama Msuva alichagua mpunga kwanza vikombe baadae, yuko vizuri japo hajawahi twaa kikombe chochote baada ya kuondoka Yanga.
 
Kylian Mbape amekataa mabilioni ya hela kwa kukataa kwenda Uarabuni msimu uliopita, kama alivyofanya mchezaji wenzake Neymar! Na badala yake ameona asaini Real Madrid msimu huu ili kuchukua zaidi makombe na tuzo binafsi.
Mbappe amelipwa vizuri sana PSG na kwa umri wake bado ana nafasi ya kucheza baadaye huko uarabuni. Ametengeneza pesa nyingi pale PSG kwahiyo sasa hivi anatafuta makombe.

Hoja yako nitaikubali kama ukiniambia mbappe hana pesa
 
Mbona hauwi specific!?
Kwani Feisal alikua halipwi Yanga?
Bonus za Champions league alikua hapati?
Bonus za makombe alikua hapati?
Kwani Feisal alikua maskini alivyokua Yanga!?
Ulitakiwa useme kuongezeka kwa ukwasi,ila sio kuunasibisha umasikini/ukapuku moja kwa moja.
Maana kwa kauli ulizoongea ni kana kwamba vikombe havina thamani kabisa.
Mkuu endelea kutoa somo hadi waelewe
 
Unajua mkataba wa Messi akiwa Barcelona, kipengele kimojawapo kilihitaji yeye kuwa mchezaji anayelipwa fedha nyingi kuliko wacheza mpira kote duniani...
Ila sasa Fei alitaka hicho akanyimwa alifata tamaa ila alikua na uwezo akaa na washauri wake akashauriana jaman naombeni ongezeko na tunaomba tufanye marekebisho ya vipengele unahisi wangegoma?
 
Mkuu, mbona umeikuza sana kauli ya Farhan? Kwani yeye ana uzito gani hadi kila anachowaza kuhusu soka kiwe sahihi?

Yeye si mtangazaji tu wa Clouds FM? Si mtangazaji tu kama Baba Levo na Mwijaku? Tusiwakuze sana hawa watu kwa vile wako redioni...
Sijaikuza ila amesema kile nilichosema hata mimi
 
Niliongea hapa na watu mkaleta Njaa zenu coz watanzania wengi tunatamaa sana na tunawaza hela sana..na ndio maana hata viongozi vijana nao wamejaa Rushwa because wanawaza pesa tu wakipata nafasi wapige pesa tu...
Uyo Farhan ni nani kiasi kwamba anachokisema ndio kiwe hitimisho la mjadala?. Mchezaji yoyote akiwa kwenye peak lazima aangalie ulinganisho wa mataji na masilahi kwamba ni wapi anaweza kupata vyote viwili, dau alilowekewa azam ni kubwa sana kuliko ambalo angepewa yanga akichokosea fei ni kuvunja mkataba kihuni. Fei toto kacheza azam msimu mmoja tu bado ni mapema kumuhukumu.
 
Back
Top Bottom