Fatma Karume ajipanga kukazia hukumu dhidi ya Musiba

Fatma Karume ajipanga kukazia hukumu dhidi ya Musiba

Fatima Karume alifungua hiyo kesi mahakama ya nchi huru ya Zanzibar ambayo ina had I jaji mkuu wake

Msiba ni mwanahabari aliye nchi ya Tanganyika yeye wala sio raia wa Zanzibar na hana mpango wa kuwa raia wa nchi ya Zanzibar

Pili Musiba na vyombi vyake vya habari. Vimesajiliwa Wizara ya habari ya Tanganyika.

Mambo ya habari si mambo ya muungano kwa mujibu wa katiba ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ni sawa na Mtanzania kufungua kesi Tanzania kushtaki gazeti linalochapisha habari japan na lililosajiliwa nchi huru ya Japani kuwa limemkashfu na mahakama ya Tanzania ikalihukumu hilo gazeti kuwa limlipe fidia huyu raia wa nchi huru ya Tanzania !!!

Hiyo hukumu anayokazia nchi za nje kwenye nchi ya nje ya Zanzibar yenye katiba yake,Raisi wake,Jaji mkuu wake na wimbo wa taifa wake watajuana huko huko akazie atakavyo .
Jiwe aje kumsaidia Musiba.
 
Swali kawaulize Zanzibar ambao ndio waliowaleta Tanzania bara hao wazanzibari wenzao Jumbe na hao mashehe unataka watanganyika tuwajibie wazanzibari? Jumbe alikuwa Raisi wao na hao mashehe walikuwa mashehe wao wa nchi yao huru nchi ya Zanzibar wakawaleta Tanganyika waulize wenyewe sio sisi watanganyika
Sasa na wewe tuliza kitenesi usiisemee mahakama. Hata kama Musiba ni bebi wako basi mtetee shemeji yetu kwa hoja zenye mashiko.
 
Unamkumbuka Mh. Mohamed Seif Khatib (rip)..
Huyu alikuwa mbunge wa jimbo la Uzini Znz, na awamu ya 4 alikuwa waziri wa habari Bara kwa miaka kadhaa.
Kama mambo ya habari si ya muungano, ina maana Watanganyika walipigwa changa la macho?!
Ndio tulipigwa changa la macho mzanzibari hatakiwi kuwa waziri wizara isiyokuwa ya muungano ni zile za muungano tu ndizo wanatakiwa wapewe
 
Zanzibar na Tanganyika zina mikataba ya kubadilishana wahalifu.

Lakini inawezekana una hoja hapa. Kwa nini usitengeneze defence team kumtetea Musiba? Hii hoja inaweza kuzungumzika Mahakama ya Rufaa

Vipi kuhusu kuhusu dude zito linalokuja la Jasusi Mbobezi? Mahakama ina jurisdiction kumhukumu Musiba pia?

Wakati ukawa wanapiga kelele tuwe na mfumo wa serikali tatu kwenye Katiba nyie ndio mlipinga. Lazima ufahamu ya kwamba nchi ni moja. Na mahakama ya Rufaa ilishatoa maamuzi kwenye kesi ya Machano Hamis na Wenzake kuwa Zanzibar sio dola ni sehemu ndani ya nchi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Tanzania bara.
 
Sasa na wewe tuliza kitenesi usiisemee mahakama. Hata kama Musiba ni bebi wako basi mtetee shemeji yetu kwa hoja zenye mashiko.
Wala sijaisemea mahakana popote after all hiyo mahakama iliyoamua hiyo kesi ni ya nchi nyingine huru ya nje ya nchi inaitwa Zanzibar kwa kesi ya raia wa nchi yao mzanzibari Fatuma Karuma nchi ambayo Musiba hana mpango wa kuomba uraia au kwenda kutembelea utalii sababu kwao Setengeti kuna mbuga yenye vivutio vya kutosha hivyo hana mpango wa hata kwenda kutalii nchi ya zanzibar kwenda kuangalia magofu ya kale ya sultani
 
Ni mifano inafanana sema kichwa chako kigumu kuelewa , nahis ww ni F material [emoji3]

Yani Japan na Zanzibar ni sawa?. Rais anayeiongoza Tanganyika anatokea Zanzibar. Na Rais wa Zanzibar ni sehemu ya Baraza la mawaziri kwenye serikali ya Jamhuri ya Muungano. Hivyo Japan na Zanzibar ni mfano tofauti kabisa.
 
Wakati ukawa wanapiga kelele tuwe na mfumo wa serikali tatu kwenye Katiba nyie ndio mlipinga. Lazima ufahamu ya kwamba nchi ni moja. Na mahakama ya Rufaa ilishatoa maamuzi kwenye kesi ya Machano Hamis na Wenzake kuwa Zanzibar sio dola ni sehemu ndani ya nchi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Tanzania bara.
Hizo kesi za kina Machano mara baada ya kesi kuamriwa kuwa Zanzibar sio nchi wazanzibar wakaona mahakama kama inawadharau wakaenda mbuo kubadilisha katiba iliyokuwepo ya Zanzibar isomeke wazi kabisa kuwa Zanzibar ni nchi

Ndio hadi leo inasomeka kuwa Zanzibar ni Nchi hiyo kesi ndio ililetelea hayo mabadiliko
 
Wala sijaisemea mahakana popote after all hiyo mahakama iliyoamua hiyo kesi ni ya nchi nyingine huru ya nje ya nchi inaitwa Zanzibar kwa kesi ya raia wa nchi yao mzanzibari Fatuma Karuma nchi ambayo Musiba hana mpango wa kuomba uraia au kwenda kutembelea utalii sababu kwao Setengeti kuna mbuga yenye vivutio vya kutosha hivyo hana mpango wa hata kwenda kutalii nchi ya zanzibar kwenda kuangalia magofu ya kale ya sultani
Kwahiyo unataka kusema mahakama kuu ya Tanzania imechemka? Haijui sheria? Haijui mipaka yake na Mahakama ya Zanzibar?
 
Kwahiyo unataka kusema mahakama kuu ya Tanzania imechemka? Haijui sheria? Haijui mipaka yake na Mahakama ya Zanzibar?
Iliyotoa hayo maamuzi sio mahakama kuu ya Tanzania ni ya nchi ya nje ya nchi iitwayo Zanzibar kusoma huoni au?
 
Lazima ufahamu ya kwamba nchi ni moja. Na mahakama ya Rufaa ilishatoa maamuzi kwenye kesi ya Machano Hamis na Wenzake kuwa Zanzibar sio dola ni sehemu ndani ya nchi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Tanzania bara.
Wana Lumumba akina YEHODAYA mnaitwa huku!
 
Iliyotoa hayo maamuzi sio mahakama kuu ya Tanzania ni ya nchi ya nje ya nchi iitwayo Zanzibar kusoma huoni au?
Soma post ya kwanza ya mleta mada.... Mahakama kuu ya Tanzania....

Tufanye mleta mada kakosea.... unadhani mahakama ya Zanzibar haina akili hata ijishughulishe na kesi ya mtu asiye raia wake? Unajua mipaka/makubaliano ya hizi mahakama kuu mbili juu ya kesi za raia wake?
 
Back
Top Bottom