Fatma Karume: Serikali imlinde Tundu Lissu na familia yake, tusikubali mtu apigwe risasi kwa sababu ya siasa

Fatma Karume: Serikali imlinde Tundu Lissu na familia yake, tusikubali mtu apigwe risasi kwa sababu ya siasa

Si walisema Magufuli ndio aliagiza kama kweli walikuwa wanaamini hivyo wasiwasi wa nini leo.

Magufuli hayupo, Kamanda Sirro hayupo, DC Athumani hayupo, Makonda hayupo, Mambosasa yupo makao makuu na admin work za jeshi la polisi.

Sasa wanamuogopa nani tena leo.

Ndio maana anarudi.
 
Wakili Fatma Karume amezungumza na Wakili TV na kufafanua mambo kadhaa ikiwemo kuhusu hali ya demokrasia nchini, siasa ya Tanzania na kurejea kwa Tundu Lissu. Huyu hapa anafafanua:

Nikiwa kama Rais mstaafu wa TLS nimefurahi sana kusikia Tundu Lissu anarudi Nchini Tanzania kwa sababu mazingira aliyoondokea hayakuwa ya kuridhisha, yalikuwa mabaya sana.

Hatuwezi kukubali mtu apigwe risasi kama vile kwa sababu ya siasa, haikubaliki kwenye Nchi yoyote inayopenda amani na demokrasia.

Nawaomba Serikali watazame hili suala, kwani waliofanya hicho kitendo cha kihalifu hawajakamatwa, ilikuwa ni kosa la jinai la kujaribu kufanya mauaji.

Serikali imekaa kimya, ni muhimu sana wale watu wakamatwe, kama inashindikana kukamatwa basi Tundu Lissu apewe ulinzi, yeye mwenyewe, familia yake wasipitie yale aliyopitia Septemba 7, 2017.

Baada ya Lissu kupigwa risasi, Watanzania tulipata mshtuko mkubwa sana, tulipitia katika kipindi cha traumatic period.

Niwaambie Watanzania wenzangu, kuwa hakuna jambo baya kukaa kimya ukiona uovu, ni jambo baya sana, tumia chochote ilichokuwa nacho kuonesha haujafurahishwa, tumia hata uso wako au sauti yako kuonesha hivyo.

Kukaa kimya na kupiga makofi huku mambo maovu yakitendeka ni kuungana na huo uovu, tusifanye hiyo tabia na tuiache.

Kuhusu ukimbizi wa kisiasa inasikitisha kuna watu walikimbia Tanzania kutokana na mambo ya kisiasa, siasa si ugomvi, siasa ni haki ya kutazama namna nyingine ya kuendesha Nchi, ni haki ya kila mwananchi kufanya siasa.

Kuwa na Wakimbizi wa kisiasa Tanzania ni aibu sana, niwakumbushe hasa CCM hawa wakimbizi wa kisiasa wametokea wakati wa CCM, tumepata wakimbizi wengi tu zaidi ya Lissu na watu kama kina Lema.

Pemba kuna watu walikimbia kwa sababu ya kisiasa, tuache huu ugomvi, tuishi kama binadamu, Tanzania ni kubwa sana, tupo watu Milioni 62, kuna nafasi sote kuishu humu ndani kwa amani.

Japokuwa hatuwezi kubaliana kwa mawazo lakini sote ni Watanzania, tupendane.

Kuhusu Demokrasia Nchini kwetu, tunakwenda hatua mbili mbele tunarudi tatu nyuma, tunakwenda tano tunarudi nne, tupo kwenye transitional democracy.

Tunatakiwa kutoka huko tuingie kwenye Demokrasia, kwa sabababu bado tupo kwenye transitional democracy, hatuwezi kuingia huko bila kubadilisha Katiba.

Lazima tutazama mfumo wetu wa kisheria na Katiba ili tuingie kwenye demokrasia inayoweza stahili na siyo mtu kuingia kwenye madaraka mkukimkuki.
Mh 🤔🤔 kwan S/Gang wanasemaje?
 
..wanadai walinzi wake ndio waliomuambukiza corona.
Halafu baada ya hapo wakampa habari lisu? Mana lisu alikua wa kwanza kutweet kuwa rais wetu kafariki na alisema kaambiwa na sources zake za kuaminika toka marekani. Sasa sisi tunataka atuelezee zaidi mana inaonekana alifahamu vizuri mlolongo mzima wa Rais wetu kuondoka
 
Halafu baada ya hapo wakampa habari lisu? Mana lisu alikua wa kwanza kutweet kuwa rais wetu kafariki na alisema kaambiwa na sources zake za kuaminika toka marekani. Sasa sisi tunataka atuelezee zaidi mana inaonekana alifahamu vizuri mlolongo mzima wa Rais wetu kuondoka

..wengi walikuwa wanajua kuwa Jpm amefariki ila hawakuwa na ujasiri wa kutoa taarifa.

..haiwezekani Raisi afariki ktk jiji kubwa kams D'Salaam halafu kifo chake kiwe siri.

..angefia Chato wangeweza kuficha siri yao kwa muda mrefu zaidi.
 
Naunga mkono ushauri wako, Ulinzi kwa Lissu ni haki yake na anastahili. Lakini tumuombe na yeye aje na siasa zenye Tija na sio za udanganyifu.
 
..wengi walikuwa wanajua kuwa Jpm amefariki ila hawakuwa na ujasiri wa kutoa taarifa.

..haiwezekani Raisi afariki ktk jiji kubwa kams D'Salaam halafu kifo chake kiwe siri.

..angefia Chato wangeweza kuficha siri yao kwa muda mrefu zaidi.
Kwanini unamsemea? Sisi tunataka kufahamu mamlaka ya kutangaza kifo cha rais wetu kwenye ukurasa wake wa mtandao wa udaku aliitoa wapi. Source zake za marekani alizosema 'zimemhakikishia' rais wetu kafariki nazo zilikuwepo dar es salaam?
 
Kwanini unamsemea? Sisi tunataka kufahamu mamlaka ya kutangaza kifo cha rais wetu kwenye ukurasa wake wa mtandao wa udaku aliitoa wapi. Source zake za marekani alizosema 'zimemhakikishia' rais weru kafariki nazo zilikuwepo dar es salaam?

..jaribuni kulifikisha suala lenu MAHAKAMANI.

..huwezi kujua taarifa gani zaidi mtazipata kupitia shauri lenu.

..Mahakama inaweza hata kuitisha UCHUNGUZI kuhusu kifo cha Jpm.
 
Mmoja wapo Leo kalewa kwenye mkutano, kwanini mnamuogopa kumtaja?
 
Mahakamani hatuendi. Tutalimaliza kwa style ileile waliyoitumia waliolianzisha

.🤣🤣

..kwa hiyo shida yenu ni Lissu kutangaza kifo cha Jpm?

..hamna shida na wanaosemekana wamemuua Jpm?

..kwani Lissu asingetangaza nini kingebadilika?

..Hiyo siri mlitaka mkae nayo kwa muda gani?
 
Si walisema Magufuli ndio aliagiza kama kweli walikuwa wanaamini hivyo wasiwasi wa nini leo.

Magufuli hayupo, Kamanda Sirro hayupo, DC Athumani hayupo, Makonda hayupo, Mambosasa yupo makao makuu na admin work za jeshi la polisi.

Sasa wanamuogopa nani tena leo.
Marehemu atakua anapata tabu sana huko alipo damu alizokunywa ni nyingi sana.
 
upuuuz mtupu tanzania ina watu milion 62 yeye alindwe kama nan akae kwake hakuna wakumshambulia aishi kama alivyokuwa anaishi awali nchi yetu ni ya amani hata huyo lema alienda huko kwa manufaa yake binafisi na wala siyo mkimbizi
Baba yenu marehemu alikua muuaji ngoja tumuone huyu bibi ushungi ila huwa nina imani waislam wengi hawana roho mbaya.
 
Back
Top Bottom