Fatma Karume: Serikali imlinde Tundu Lissu na familia yake, tusikubali mtu apigwe risasi kwa sababu ya siasa

Kwanini unamsemea? Sisi tunataka kufahamu mamlaka ya kutangaza kifo cha rais wetu kwenye ukurasa wake wa mtandao wa udaku aliitoa wapi. Source zake za marekani alizosema 'zimemhakikishia' rais wetu kafariki nazo zilikuwepo dar es salaam?
Pole Sana kwa Kufiwa na Kipenzi chako.

Ndio hatunaye Tena, ameshatangulia iwe kwa corona au kwa kibetri kuisha chaji.

Hizo "abracadabra" wala hazitasaidia chochote.

Mungu aliyemnusuru Lissu dhidi ya Kifo cha Kikatili ndiye Huyo huyo alitoa Kibali Mpendwa wako aende.

Tumrejeshee Sifa, heshima na Shukrani kwa Kuwa amedhihirisha Ukuu wake.
 
Wananchi wote tuna haki sawa za kulindwa. Yeye alindwe zaidi kama nani? Familia yake ni raia wa nchi ya kigeni, kwa nini tupoteze raslimali zetu kutoa special treatment kwa raia wa mataifa ya kigeni badala ya kulinda raia wetu? Waende kwenye nchi yao wakalindwe huko.
Wewe ulipigwa risasi kumi na ngapi,na ukapona na huhitaji ulinzi?
Kama hujawahi kupigwa risasi,hebu siku moja upigwe risasi mbili tu au moja,labda kisa unakosoa serikali,ukipona usihitaji ulinzi na ujitokeze hadharani uwe wa mfano,useme kua 'mbona mimi nilipigwa risasi na watu wasiojulikana,na hawajatiwa nguvuni,na bado sihitaji ulinzi?'
Hakika utaeleweka zaidi,omba ufanyiwe shambulio ili uwe shuhuda.Sema amen.
 
Asante sana kwa kunipa pole mtanzania nliyefiwa na Rais wetu. Lisu atakufa nae. Wewe pia utakufa. Kwahayo pole na wewe pia. Kuhusu hizo ulizoziita 'abracadabra' ambazo umedai hazitasaidia chochote ningekushauri tu uuache muda uchukue nafasi yake, utakuja kujionea.
 
Wakili Fatma Karume amezungumza na Wakili TV na kufafanua mambo kadhaa ikiwemo kuhusu hali ya demokrasia nchini, siasa ya Tanzania na kurejea kwa Tundu Lissu. Huyu hapa anafafanua:

Nikiwa kama Rais mstaafu wa TLS nimefurahi sana kusikia Tundu Lissu anarudi Nchini Tanzania kwa sababu mazingira aliyoondokea hayakuwa ya kuridhisha, yalikuwa mabaya sana.

Hatuwezi kukubali mtu apigwe risasi kama vile kwa sababu ya siasa, haikubaliki kwenye Nchi yoyote inayopenda amani na demokrasia.

Nawaomba Serikali watazame hili suala, kwani waliofanya hicho kitendo cha kihalifu hawajakamatwa, ilikuwa ni kosa la jinai la kujaribu kufanya mauaji.

Serikali imekaa kimya, ni muhimu sana wale watu wakamatwe, kama inashindikana kukamatwa basi Tundu Lissu apewe ulinzi, yeye mwenyewe, familia yake wasipitie yale aliyopitia Septemba 7, 2017.

Baada ya Lissu kupigwa risasi, Watanzania tulipata mshtuko mkubwa sana, tulipitia katika kipindi cha traumatic period.

Niwaambie Watanzania wenzangu, kuwa hakuna jambo baya kukaa kimya ukiona uovu, ni jambo baya sana, tumia chochote ilichokuwa nacho kuonesha haujafurahishwa, tumia hata uso wako au sauti yako kuonesha hivyo.

Kukaa kimya na kupiga makofi huku mambo maovu yakitendeka ni kuungana na huo uovu, tusifanye hiyo tabia na tuiache.

Kuhusu ukimbizi wa kisiasa inasikitisha kuna watu walikimbia Tanzania kutokana na mambo ya kisiasa, siasa si ugomvi, siasa ni haki ya kutazama namna nyingine ya kuendesha Nchi, ni haki ya kila mwananchi kufanya siasa.

Kuwa na Wakimbizi wa kisiasa Tanzania ni aibu sana, niwakumbushe hasa CCM hawa wakimbizi wa kisiasa wametokea wakati wa CCM, tumepata wakimbizi wengi tu zaidi ya Lissu na watu kama kina Lema.

Pemba kuna watu walikimbia kwa sababu ya kisiasa, tuache huu ugomvi, tuishi kama binadamu, Tanzania ni kubwa sana, tupo watu Milioni 62, kuna nafasi sote kuishu humu ndani kwa amani.

Japokuwa hatuwezi kubaliana kwa mawazo lakini sote ni Watanzania, tupendane.

Kuhusu Demokrasia Nchini kwetu, tunakwenda hatua mbili mbele tunarudi tatu nyuma, tunakwenda tano tunarudi nne, tupo kwenye transitional democracy.

Tunatakiwa kutoka huko tuingie kwenye Demokrasia, kwa sabababu bado tupo kwenye transitional democracy, hatuwezi kuingia huko bila kubadilisha Katiba.

Lazima tutazama mfumo wetu wa kisheria na Katiba ili tuingie kwenye demokrasia inayoweza stahili na siyo mtu kuingia kwenye madaraka mkukimkuki.
Mhh, je 1964 Hadi 1972 ilikuwaje,
 
Wananchi wote tuna haki sawa za kulindwa. Yeye alindwe zaidi kama nani? Familia yake ni raia wa nchi ya kigeni, kwa nini tupoteze raslimali zetu kutoa special treatment kwa raia wa mataifa ya kigeni badala ya kulinda raia wetu? Waende kwenye nchi yao wakalindwe huko.

Una wivu uliojikita kwenye hasira!! Umeshindwa kujiuliza jambo dogo sana, kama ni raia wa kigeni - anakujaje kujihusisha na siasa??? Au una ushahidi gani ni raia wa kigeni? Au kwa kuwa anaishi usipoishi wewe ndio unasikia hasira??

Special treatment unayolalamikia pamoja na kujifanganya wananchi wote wana haki sawa anapewe mpaka mkuu wa wilaya!! Kinachomfany aonekane kustahili ulinzi tofauti (hata kama ni binafsi) ni UKWELI kuwa waliofanya shambulio lile hawakuwahi kukamatwa na haijulikani kama bado wanataka kutekeleza azma yao.

Mkuu wivu huleta upofu wa filra na hasira ndani ya mtu! Punguza utakuwa binadamu!!
 
Wewe ulipigwa risasi kumi na ngapi,na ukapona na huhitaji ulinzi?
Kama hujawahi kupigwa risasi,hebu siku moja upigwe risasi mbili tu au moja,labda kisa unakosoa serikali,ukipona usihitaji ulinzi na ujitokeze hadharani uwe wa mfano,useme kua 'mbona mimi nilipigwa risasi na watu wasiojulikana,na hawajatiwa nguvuni,na bado sihitaji ulinzi?'
Hakika utaeleweka zaidi,omba ufanyiwe shambulio ili uwe shuhuda.Sema amen.
Kwa maana hiyo watu wote waliojeruhiwa kwa mishale, mapanga, mikuki, nk nao wanastahili kupewa ulinzi maalumu. Au unataka yeye apewe ulinzi maalumu kwa kuwa ni mwanasiasa, au kwa kuwa alijeruhiwa kwa risasi? Raia wengine waliojeruhiwa na majambazi mbona huombi wapewe ulinzi maalumu? (Majambazi pia ni watu wasijulikana)
 
Halafu baada ya hapo wakampa habari lisu? Mana lisu alikua wa kwanza kutweet kuwa rais wetu kafariki na alisema kaambiwa na sources zake za kuaminika toka marekani. Sasa sisi tunataka atuelezee zaidi mana inaonekana alifahamu vizuri mlolongo mzima wa Rais wetu kuondoka
Lissu anajua,ila waliomuua Jpm hawezi kuwafahamu. Wabaya serikalini walimpa taarifa kwa wakati za kifo Cha Jpm kwa sababu walijua uadui uliopo baina yake na magufuli na pia ni Msiri hawezi kusema Nani alimpa taarifa hizo kutoka serikalini
 
Wananchi wote tuna haki sawa za kulindwa. Yeye alindwe zaidi kama nani? Familia yake ni raia wa nchi ya kigeni, kwa nini tupoteze raslimali zetu kutoa special treatment kwa raia wa mataifa ya kigeni badala ya kulinda raia wetu? Waende kwenye nchi yao wakalindwe huko.
 
Wakili Fatma Karume amezungumza na Wakili TV na kufafanua mambo kadhaa ikiwemo kuhusu hali ya demokrasia nchini, siasa ya Tanzania na kurejea kwa Tundu Lissu. Huyu hapa anafafanua:

Nikiwa kama Rais mstaafu wa TLS nimefurahi sana kusikia Tundu Lissu anarudi Nchini Tanzania kwa sababu mazingira aliyoondokea hayakuwa ya kuridhisha, yalikuwa mabaya sana.

Hatuwezi kukubali mtu apigwe risasi kama vile kwa sababu ya siasa, haikubaliki kwenye Nchi yoyote inayopenda amani na demokrasia.

Nawaomba Serikali watazame hili suala, kwani waliofanya hicho kitendo cha kihalifu hawajakamatwa, ilikuwa ni kosa la jinai la kujaribu kufanya mauaji.

Serikali imekaa kimya, ni muhimu sana wale watu wakamatwe, kama inashindikana kukamatwa basi Tundu Lissu apewe ulinzi, yeye mwenyewe, familia yake wasipitie yale aliyopitia Septemba 7, 2017.

Baada ya Lissu kupigwa risasi, Watanzania tulipata mshtuko mkubwa sana, tulipitia katika kipindi cha traumatic period.

Niwaambie Watanzania wenzangu, kuwa hakuna jambo baya kukaa kimya ukiona uovu, ni jambo baya sana, tumia chochote ilichokuwa nacho kuonesha haujafurahishwa, tumia hata uso wako au sauti yako kuonesha hivyo.

Kukaa kimya na kupiga makofi huku mambo maovu yakitendeka ni kuungana na huo uovu, tusifanye hiyo tabia na tuiache.

Kuhusu ukimbizi wa kisiasa inasikitisha kuna watu walikimbia Tanzania kutokana na mambo ya kisiasa, siasa si ugomvi, siasa ni haki ya kutazama namna nyingine ya kuendesha Nchi, ni haki ya kila mwananchi kufanya siasa.

Kuwa na Wakimbizi wa kisiasa Tanzania ni aibu sana, niwakumbushe hasa CCM hawa wakimbizi wa kisiasa wametokea wakati wa CCM, tumepata wakimbizi wengi tu zaidi ya Lissu na watu kama kina Lema.

Pemba kuna watu walikimbia kwa sababu ya kisiasa, tuache huu ugomvi, tuishi kama binadamu, Tanzania ni kubwa sana, tupo watu Milioni 62, kuna nafasi sote kuishu humu ndani kwa amani.

Japokuwa hatuwezi kubaliana kwa mawazo lakini sote ni Watanzania, tupendane.

Kuhusu Demokrasia Nchini kwetu, tunakwenda hatua mbili mbele tunarudi tatu nyuma, tunakwenda tano tunarudi nne, tupo kwenye transitional democracy.

Tunatakiwa kutoka huko tuingie kwenye Demokrasia, kwa sabababu bado tupo kwenye transitional democracy, hatuwezi kuingia huko bila kubadilisha Katiba.

Lazima tutazama mfumo wetu wa kisheria na Katiba ili tuingie kwenye demokrasia inayoweza stahili na siyo mtu kuingia kwenye madaraka mkukimkuki.
Kwan akina jilala, etwege magonjwa mtambuka countrywide ussr na wengine wanasemaje?
 
Si walisema Magufuli ndio aliagiza kama kweli walikuwa wanaamini hivyo wasiwasi wa nini leo.

Magufuli hayupo, Kamanda Sirro hayupo, DC Athumani hayupo, Makonda hayupo, Mambosasa yupo makao makuu na admin work za jeshi la polisi.

Sasa wanamuogopa nani tena leo.
Kwani Hao uliowataja ndiwo walikamata bunduki wakafyatua risasi ?
 
Back
Top Bottom