Baada ya maoni mengi ya wadau , mimi naomba nichangie pia mtazamo wangu.
Mosi Mafwele iwe kutekwa, kufanyiwa ukatili kama inavyosemekana ni suala ambalo linawezekana vizuri tu , ila linaweza kuwa na motive kadhaa nyuma, mfano ukichunguza kurudi nyuma 2024 jina la huyu mtu halikua likisikika katika vyombo vya habari sana ila baada ya tukio la Sativa mengi juu yake yalisemwa kwani ilibainika huyu mtu ni mtekelezaji wa amri nyingi haramu ambazo hata ziko nje ya mamlaka yake kiutendaji hivyo ni mtu anayeogopwa sababu anaingilia na kuchukua maelekezo ya utekelezaji nje ya mipaka yake ya kazi kiutendaji na kiidara.
Hivyo kama kafanyiwa inaweza kuwa nayw kasalitiwa kimkakati ikiwa ni namna ya kumuondolea nguvu na njia ya kuanza kujisafisha hapo policcm ili wapoze joto la mambo ya ICC kwani hata MO29 huyu mtu uhusika wake ni mkubwa sana na viapo vyao vya kazi huwa wanapofika kuona mtu wanataka kumuondoa ndio wanatengenezewa ajali au kifo kisichoeleweka.
Hivyo Mafwele kufanyiwa chochote inawezekana kabisa kwani 2012 , RPC wa Mwanza Liberatus Barlow alipigwa risasi na majambazi na kufariki dunia, hivyo hao wanaosema Mafwele sijui ana ulinzi mkubwa wakae wafahamu hakuna ulinzi mkubwa kwani hata Maduro licha ya kujua anafuatiliwa muda mrefu alinyakuliwa kwa kamba chumbani kwake.
Pili, suala la Polepole na Mdude kuwa hai hapa ninatofautiana na bw Augustino Polepole kwanini ,jibu ni jepesi tu Polepole alikua tishio sana kwa watu wawili walioweka CCM kwapani ambao ni mafisadi wawili Rostam Aziz na Kikwete , hata leo hii tunapoongea jukwaa hili liko kifungoni tangu September 6 sababu ya Polepole kuibua kashfa kule kwenye mgodi wa makaa ya mawe.
Polepole ndio alifanya hata Rostam kustage interview na Tindo Mhando na nyingine kumleta mtu anayedai ni mwalimu wake wa shule ya msingi huko Igunga, hizi interview zote zilifanyika katika kipindi kashfa hii imewaka na sikumbuki lini mara ya mwisho Rostam alitoka mafichoni kufanya interview pengine ni zaidi ya miaka 15+ nyuma tena akiwa katika siasa za majukwaani , kitendo hata cha interview ya kwanza kutofanyika ils mara ya kwanza walipopanga kinatupa jibu namna gani alikua katika hofu baada ya kutosikika kwenye media miaka mingi kwa ufisadi wake sasa Polepole alimrudisha kutoka mafichoni , hata tukishuhudia Rostam akijibizana na Polepole kwa kusema ni "wakuja" kwenye chama hii ikupe picha ni namna gani alikua ni target namba 1 na ya muhimu, bila kusahau Kikwete naye alimjibu jukwaani na kutumia machawa hata kupunguza kasi ya mtandao akiwa anafanya zile live zake.
Hadi hapo utajua tu baada ya pesa nyingi kutumika hatimaye Polepole aliuzwa na waliojua alipo na kazi ilikua ni moja tu kuingia alipo kuchukua taarifa muhimu na mipango yake au waliokuwa naye kisha kummaliza.
Hivyo napingana 100% na Augustino Polepole kuwa mdogo wake yuko hai bado , mimi ninaamini kwa damu zile ni aidha walimuua palepale katika mpambano wa kukataa kutekwa , na kama alipona basi waliondoka nae na kukaa nae huko mafichoni kwa siku kadhaa wakimhoji kwa kina na awape mipango yake na vifaa vyake vya kielektroniki vyote na credentials zake kisha wakamuua.
Huyo kaka yake kama amedhamiria kutekeleza kisasi kama alivyodai akitekeleze huku akiamini kabisa ni kisasi juu ya mdogo wake aliyeuwawa na sio mateka tena.