Salaam, sijapita hapa siku nyingi sana. Jamaa zangu kina
Aleyn GUI1 PNC na wengine. Baada ya mimi kuhamishia mapenzi kule anfied napitaga tu hapa na kucheki wadau mnasemaje.
Nimepokea kwa mstuko mkubwa kwa taarifa kuwa Luis Suarez anaondoka na kwenda kujiunga na mabingwa wa italia juventus. Leo alionekana mjini perugia alikoenda kwa ajili ya kufanya mazungumzo na uongozi wa juve kuhusu yeye kujiunga nao.
Tukubaliane, kutokubaliana. Zama zetu kwa sasa zimefikia mwisho. Ile baecelona iliyojengwa miaka kumi iliyopita ndio imefikia mwisho. Inatakiwa barcelona mpya. Ile aliyorithi Guandiola toka kwa Ridjikaard amebakia Messi pekeake bado anacheza. Wengine wote wamesha staafu au wanamalizia soka lao vilabu vingine vya madaraja ya chini.
Wachezaji aliokuwa nao Guandiola na,Tito Villanova, first 11 yao kwa sasa wamebaki wa3. Pique, Busquet na Messi. Wengine wote wameondoka,
So, tunahitaji barceloa mpya. Kuanzia bench la ufundi, hili lifumuliwe lote, hadi wachezaji. Tuanze mdogo mdogo. Tuangalie wapi pa kurekebisha. Na kwa maoni yangu backline ndio mbovu na ndio panye udhaifu mkubwa. Hapa apatikane watu kama Upamecano na Mathijs de Ligt. Then wapandishwe wawili toka kule timu B.
Mabeki wa pembeni/flank upande wa kulia hapajapwaya. Yupo Semedo na Sergi Roberto. Kule kwa alba kina Firpo wameshindwa kuonyesha uwezo wao. Atafutwe mmoja wa kiwango cha Hakimi asaidiane na Alba. Firpo auzwe.
tuna stoke kubwa ta viungo. hapa kocha ndio ana mtihani mgumu. Wapunguzwe wabakie wachache haswa waliotokea pale la masia. Hawa wanaelewa falsafa ya barcelona vizuri. Rakitic, Aigizwe sokoni.
Pale mbele. Goal geter mmoja wa viwango vya Suarez, grezmann kashindwa kuonyesha thamani yake. Kina breithwe hawafai kuchezea barcelona aondoke hata kwa free poa tu.
Mwisho makocha wa aina ya Quique Sitien na huyu wa sasa bado hawana uwezo wa kuifudisha barcelona. Tunahitaji makocha wenye ujuzi na ubora. Hivi walishindwa nini kumpa timu pocchetino aliyekuwa spurs? Yule kacheza spain na analijua soka la spain nje ndani.
Huu msimu utakuwa mgumu na wwnye fesheha nyingi sana. jiandaeni kisaikolojia maana mlizoea kupata raha ila sasa ni kinyume chake.