FC Barcelona (Barça or Blaugrana) | Special Thread

Koeman pimbi sana lime muuza hadi semedo wolves
Hivi huyu kocha kwanini kapewa timu kipindi kigumu kama hiki???
Hatuna kocha kabisa
 
Ushuhudi wa alichokisema Messi kwa board ya Barcelona upo na bado unaendelea :Kama kuku aliekatwa shingo


Another saga ya kuchanganyikiwa board ya Barcelona wamemuuza semedo so hatuna natural RB

Yaani mchezaji anakubali kuondoka team kubwa kama Barcelona anaenda Wolves -team ndogo ya wa portuguese kwa sababu anaona kabisa Barcelona hakuna bright future

Enyi watu nawaambia tuanze kuzoea ,Messi Barcelona huu ni msimu wake wa mwisho

Hata Kama Suarez kachoka huwezi kufanya replacement yake eti awe Depay ,unamkosea heshima El Pisterero (top 5 goal scorers wa Barca ame make history no matter what),na laana yake haitakosa kututafuna ,hivi niwaulizeni Paco Alcacer na Depay nani ni mzuri?au umeshawahi kujiuuliza kwanini wanahangaika usiku na mchana ili aletwe muholanzi Depay ,kwani Griezman aliletwa kwa kazi gani?hawamuamini tena?mbona waliunguza fedha nyingi sana kuletwa pale hadi ,financial status ya team ikakosa nafasi ya kumrudisha Neymar?The board is confused ,nani anajua sababu aliuzwa sub ya Suarez Paco Alcacer akaenda aka perform sana Borrusia Dortmond hadi alipokimbizwa na Halaand na kuamua kurudi zake Villarreal na kuacha kumbukumbu kule mwaka juzi?

Acha hilo mwezi uliopita wamefanya kituko kingine wamemuuza kijana wa miaka 23 kutoka America ya kusini team ya Gremio straight to Barcelona alikuja msimu wa 2018, Arthur Mello na wakamchukua Pjanic Milarem ambaye ana miaka 32 ,muda huo huo wakilalamika kua midfileder za Barcelona umri umekwenda (Sergio Busquets ,Ivan Rakitic ,Artulo Vidal),Hivi mnakumbuka ujio wa Paulinho 2017?msinichekeshe

Hivi mnakumbuka Barca mwezi February walimnunua striker Martin Braithwaite kwa pound mil 24 tena kutoka leganes ya Spain ambae alitetwa kwa mkopo kutoka Middlesbroug ya Germany??kulikua na sababu gani ya kumuuza Carlez Perez kwenda AC Roma(natural striker wa lamasia ambaye alikaririwa nchini Italy baada ya kuuzwa akisema pale Barcelona watoto wachanga board haina uvumilivu na sisi wa Lamasia )?

Je Messi anaposema Barcelona hamna project yoyote ,wala mpango wa kuitumia Lamasia kujenga team, wanafukia tu kashimo anakua amekosea?actions za board ya Barcelona speaks more than their promises

Tumeona kwa watoto waliopotezewa ramani na dira ya kuchezea team yao ya ndoto hii ni baadhi tu ya mifano Carlez Arena ,Riqui Puig huyo ametiwa depression recently ,tumeona kwa akina Miranda ,Dennis Suarez ,Munir El hadaad ,Deleofeu ,Sergi Samper ,Fundi Marc Cucurella eti unamuuza then unamnunua Junior Firpo eti ndio replacement ya Jordi Alba?

Hivi mnajua Thiago Alcantara bado mdogo wake Rafinha Alcantara yuko bado Barcelona anakopeshwa tu kila mwaka mara Inter Milan ,mara Celta Virgo ,kaka aliji offer tena kwa Barcelona sio chini ya mara tatu kuanzia 2016 baada ya kuuzwa kwa bei ya kutupwa mwaka 2015 akaelekea Buyern?Yeye wakati anakua pale Lamasia Cantera watoto wenzake walikua Wana brand na kumuita Kama the next Andrew Iniesta ,usishangae yeye kuongoza kupiga key passes na pass acuuracy ya 95% plus kwa sababu alikulia hivyo Lamasia na Barcelona ndio home hadi mzee wake Mazinho Alcantara ana card ya trusted legend wa Barcelona ,je unajua board walisema nini ?eti bora tumchukue Wijnaldum wa Liverpool

Hapo sitaki kupigilia msumari wa deal la usajili wa Dembele na Coutinho,wala saga la Neymar alivyoenda PSG na kutamani kwake mara moja kurudi Barcelona jinsi walivyolishughulikia

Nina wasiwasi Ansu Fatti ,chini ya menager wake mpenda fedha Mendez, team itakayo muhitaji ikifikia tu dau la kutosha ,Barcelona hawatajishauri mara mbili watamuuza na kumuacha Dembele [emoji23],kwani si tumeona kwa mtoto mdogo Xavi Simons (the next Xavi ) alivyouzwa PSG mwaka 2018?

Hatuna future pale ,let's begin from the scratch ,namtabiria mabaya sana huyu mzee wa kiholanzi
 
Mkuu umeongea mambo ya msingi kabisa. Kinachofanyika barca kwenye msimu wa usajili unaweza kudhani hakuna benchi la ufundi. Miaka minne mfululizo timu inaondolewa Ucl kwa makosa ya ulinzi lkn ikifika wakati wa usajili timu inahangaika na washambuliaji. Timu iliyokua inawekeza katika vijana wa lamasia sasa hivi iko busy na wazee? Makosa ya usajili yaliyofanyika ndani ya miaka minne hii inaweza kuchukua miaka zaidi ya mitatu kuyarekebisha.
 
Barca liwalo na liwe...
Hata kama humtaki mchezaji unamfurumusha lakini sio mchezaji hadhi ya Suarez.

Yaani timu haieleweki inatoka wapi au inakwenda wapi.
 
Hili jinga Bartomeo nadhani limepandikizwa pale kuua timu. Maana toka liingie pale ni maamuzi tu ya kipuuzi linafanya. Toka liingie halijafanikiwa chochote katika usajili. Kwanza mzungu gani unaanzisha project inafail miserably ila bado unakomaa tu kwenye cheo chako! Hiki kidingi kitakuwa kichawi sio bure
 
Suarez is third top all scorer of barcelona
 
Timu yetu bado siiamini lakin madrid ndo bomu kabisaa
 
Ni ukweli uliowazi mkuu, hatuna timu ya kupambana na Bayern na Juventus, tunahitaji kuondoa timu nzima ya zamani na kusuka upya.

Pia hakuna zama zinazokaa milele, tukubali tu kuwa zama zetu zilishaisha, sasa hivi tunahitaji kusuka timu ya zama nyingine.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…