Nimefuatilia kwa kina jinsi wadau mnavyochangia mada na nimegundua kuwa kuna kitu ambacho kinakuwa kinaleta utata katika kujua timu bora, hili ni jambo ambalo kikawaida linatokana na mitazamo tofauti tuliyonayo binadamu katika kuchanganua jambo lolote.
Kuna mdau kagusia kwa kusema kuwa timu bora ni timu inayocheza complete football, yaani ni timu iliyokamilika katika idara zote, huyu ndio naungana naye. Timu bora ni timu ambayo unapoiangalia inacheza unapata radha halisi ya mpira, hauoni mapungufu katika idara yoyote, pia ina wachezaji wakali, wenye uwezo mkubwa huku ikiwa na uwezo mkubwa wa kushinda game lolote bila kujali mazingira. Unapotaka kulinganisha uwezo wa timu bora kutoka ligi tofauti, pamoja na kuangalia uwezo katika hiyo ligi yake lakini ni lazima uzingatie michuano inayowakutanisha.
Wanapokutana wataalamu katika kujua ni timu gani bora kwa kawaida wanaangalia uwezo wa timu hiyo kwa wakati huo na si kwa kuangalia historia pekee. Timu bora ya 2010 haiwezi kuwa ni timu iliyochukua vikombe miaka ya sabini, ila unapotaka kuangalia timu bora all the time ndio inabidi uanze kuchanganua timu bora katika kila mwaka na baada ya hapo unalinganisha sasa, kwamba ubora wa Barca 2010/2011 ni sawa na ubora wa Madrid 2001/2002, sio kufanya majumuisho ya kwamba kwa kuwa Barca amechukua vikombe vichache kuliko Madrid katika historia zao basi haiwezi kuwa bora kuliko Madrid kwa wakati huu. Hapo ndio napenda tutofautishe. Kwa kawaida timu bora ni muhimu iwe inashinda mechi na pia ichukue makombe, lakini si kila timu inayochukua kombe kwa wakati huo ni bora kuliko timu zote.
Kwahiyo wadau, ni vema kuweka bayana kuwa unaweza linganisha uwezo ya timu flani kwa mwaka huu ukilinganisha na timu hiyo hiyo au nyingine kwa mwaka mwingine na ndio maana unaweza kujua uwezo wa soka wa timu fulani au taifa fulani au ligi fulani unapanda, unashuka au uko palepale.