Kila nikiangalia hili sakata la Fei Toto natamani sana kumjua aliyekuwa mshauri wake tangu mwanzo. Yatasemwa mengi lakini pamoja na kuwa na haki ya madai yake lakini kosa kubwa alilofanya ni kuondoka kambini ambako ndio sehemu ya kazi. Wenzake duniani kote huwa wanafanya mgomo baridi lakini mazoezini wanaenda na kwenye mechi wakipangwa wanacheza chini ya kiwango. Ikishafika hali hiyo basi wenye timu wanakuwa hawana ujanja kwani hawwawezi kuthibitisha mahali popote kuwa unacheza chini ya kiwango au unawahujumu basi kwa shingo upande wanakuweka sokoni unaoondoka. Ila hii mbinu aliyotumia Fei Toto ni ya hovyo sana na sidhani hata huko CAS kama atatoboa.
Mfano mdogo tu wa hivi karibuni ni wa mchezaji wa Viper Manzoki. Yeye alifanya mgomo baridi basi Vipers wakamuuza China.
Mfano mdogo tu wa hivi karibuni ni wa mchezaji wa Viper Manzoki. Yeye alifanya mgomo baridi basi Vipers wakamuuza China.