Feisal Salum Feitoto amekosa mzazi

Feisal Salum Feitoto amekosa mzazi

Ni Mchezaji Mzuri Ila waliomzunguka wanamuaminisha kuwa yeye ni zaidi ya Prime Zinedine Zidane
kama ni mchezaji mzuri mbona hanunuliwi hata kwa matimu magalasa tu ya kiarabu huko kama wenzake? bila faitoto yanga hawawezi kushinda mechi? tupa kule. watu hata kabla hawajafanikiwa kwenye maisha wanapanda mabega juuu, umepata kidogo tu mabega juu utafikiri mchungaji kimaro, dawa yake ni kuwaacha waendelee kwenye shimo waliloliendea kina kaseja tu. sasaivi hata timu ya balozi wa mtaani haiwezi kuwaita. mvumilivu hula mbivu. na usiwe na kibri kabla hujafanikiwa.
 
Ongeeni muongeavyo lakini kuanzia viongozi, mashabiki wa utopolo huwa mna roho za kichawi na kimasikini na wengi wenu hamna akili.
Fei toto amesha sema hataki kuendelea kukaa yanga kwa sababu kapata timu iliyo bora kwake kimaslahi lakini mmemgangania tu.

Simba walimuachia Samata kwenda mazembe baada ya kuona kule mazembe atapata maslahi kwa manufaa ya maisha yake lakini nyinyi hamta kumuachia Fei kwa ajili manufaa ya maisha yake badala yake nyinyi mnataka atumike kwa ajili ya maslahi yenu tu.
Ni aibu kwa mazee mazima yanayo jiita masomi kutumia nguvu kubwa kumiharibia ndoto kijana mdogo kama fei eti kwa ajili ya kumkomoa.
Acha kulialia. Mshauri huyo dogo asiye jielewa, afuate utaratibu. Hata huyo Samatta unayemtolea mfano, aliondoka simba kwa kufuata utaratibu;

Hao Tp Mazembe hawakumpa Samatta hela kwa siri, ili avunje mkataba na timu yake.
 
Mbwana Samatta amekulia katika viunga vya Mbagala huko ndiko kuliko mtambulishan katika uga wa kandanda. Historia ya huyu mchezaji haikuwa rahisi kutoboa hadi kufikia hapo alipofikia. Kuna kipindi alikuwa anakosa hata sh. 200 ya nauli ya kumpeleka mazoezi. Waliokuwa karibu yake walimsaidia pesa ya nauli. Sina haja ya kueleza mengi kuhusu mchezaji huyu aliyecheza African Lyon kwa miaka miwili kuanzia 2008 hadi 2010 alipohamia club yake pendwa ya Simba SC. Kila mtu anayefuatilia na asiyefuatilia soka katika nchi hii anamjua Mbwana Samatta.

Ifahamike hapa, lengo sio kumzungumzia Mbwana Samatta, ila tu nataka nikukumbushe au niwakumbushe wachezaji wa Kitanzania njia alizopitia Mbwana Samatta.

Ndio, baada ya kuwika na African Lyon, 2008-2010 Mbwana Samatta alisajiliwa na Simba SC kwa ada ya usajili ambayo ni siri hadi leo lakini moja ya kipendele katika mkataba wake ilikuwa ni lazima Simba SC wampatie gari mpya aina ya Toyota Mark II Grand GX 110.

Siku zikaenda zikarudi lakini team yake ya Simba hawakutimiza ahadi ya kumpatia gari ambayo walimuahidi, Toyota Mark II Grand GX 110. Kumbuka kipindi hicho Samatta alishaanza kuteka mioyo ya wana Msimbazi wa uhodari wake wa kupachika nyavu… nini kilitokea??

Mbwana Samatta, AKAGOMA. Hii ilikuwa ni mwaka 2011 mwanzoni hapo club ya Simba inakabiliwa na mechi ngumu mbeleni dhidi ya TP Mazembe katika ligi ya Mabingwa Afrika.

Hapo ndipo akaibuka Kenny Mwaisabula Maarufu kama “MZAZI’’ huyu ni mmoja katika ya watu walimsaidia Mbwana Samatta katika makuzi ya kisoka. Hata zile mia mbili mia mbili za nauli za kwenda kwenye mazoezi Mbwana Samatta amepatiwa sana na huyu “MZAZI”

Kenny Mwaisabula, ‘’MZAZI’’ kupitia gazeti la Mwanasporti na kupitia ukaribu aliokuwa nao na Mbwana Samatta alimsihi sana kijana wake asigomee mazoezi wala mechi za Simba. Katika Makala yake hiyo ‘’MZAZI’’ alimuomba Mbwana Samatta aendelee tu kucheza mpira ipo siku atapata kile anachotaka kupitia huo mpira, cha msingi asiache mazoezi na aongezee bidii kwenye mechi kwani kwa kufanya hivyo ipo siku atapata na atakuwa na uwezo wa kununua Zaidi gari mia moja kama hiyo aliyoahidiwa na Simba.

Haikuishia hapo, ‘’MZAZI” akakaa na Mbwana Samatta nakumueleza kuwa Simba SC wapo kwenye ligi ya mabingwa Afrika na kama ataendelea kugoma hawezi kupata chance ya kucheza michezo hiyo mikubwa Zaidi kwa upande wa vilabu barani Afrika.

Ndipo Samatta akamsikiliza ‘’MZAZI’’ Kenny Mwaisabula. Akarudi Kambini. Mechi ya kwanza Simba akacheza na TP Mazembe ugenini tarehe 20/03/2011 na Samatta akiwa ndani Simba akafungwa 3-1 pale Lubumbashi.

Mechi ya pili pale taifa Mnyama anakufa tena 3-2 dhidi ya TP Mazembe magoal ya Simba yalifungwa na SHija Mkina dakika ya 58 kwa Assist ya Mbwana Samatta na goal la pili la Simba lilifungwa na Mbwana Samatta mwenyewe dakika ya 70. Hii mechi Mbwana aling’aa sana. Mwingine aliyeng’aa sana kwenye mechi hii ni Mganda Patrick Ochan. TP Mazembe wakaondoka na majina mawili, Patrick Ochan na Mbwana Samatta. Mwaka huo huo 2011, Mbwana Samatta na Patrick Ochan wakatua TP Mazembe.

Bila ushauri wa ‘’MZAZI’’ Mbwana Samatta angeendelea kugoma na angeendelea kugoma sidhani kama TP Mazembe wangemuona akiwa kwao Mbagala alisubiri GX 110 aliyoahidiwa na Simba SC.

Baada ya hapo wazungu wanasema ‘’the rest is history’’ kila mtu anajua ukwasi wa Captain Diego Mbwana Samatta, niliyecheza nae pale Mbeya viwanja vya MBATTA kipindi cha utoto wetu.

Bahati mbaya sana ndugu yetu Feisal Salum Abdallah ‘’FEITOTO’’ amekosa mtu kama ‘’MZAZI’’ katika carrier yake ya kucheza mpira, mtu ambaye anaona mbali na kukitazama mbali kipaji cha FEITOTO. Huyu mtu amekosekana katika maisha ya Feitoto. Watu walionyuma ya Feisal kwasasa ni wale watu ambao wamefikiri leo tu na sio kesho na kesho kutwa na huyu mchezaji.

Ndio, hakuna ubishi ya kuwa FEITOTO ameibeba sana Yanga katika mabega yake na anastahili kupata donge nono katika mshahara wake lakini njia alizotumia ni kama tu zile Hasira za mkizi. Timu yake ya YANGA inakaribia kuanza kucheza michuano ya kimataifa lakini yeye hayupo kikosini. Na bila shaka hii michuano ya Kombe La Shirikisho la Afrika ingekuwa ni Platform kwake kujitangaza kimataifa Zaidi na huenda angepata team nzuri nje ya Nchi ambayo ingekidhi mahitaji yake mara Zaidi ya watu wanaomrubuni kwasasa.

Naamini kabisa FEITOTO angekuwa na ‘’MZAZI’’ angeshauriwa aendelee kucheza huku akiendelea kubargain juu ya maslahi yake mapya kitu ambacho team yake ya YANGA wasingeshindwa kusimsikiliza.

Feisal Amekosa mtu kama Kenny Mwaisabula.

Nawasilisha.

N.B;

FEISAL SALUM FEITOTO RAMADHANI SINGANO A.K.A MESSI ANAOMBA UPOKEE SIMU YAKE ANAKUPIGIA
Mbeya unazungumzia uwanja mpaka uwanja Ngoma? Nimecheza pale na timu ya forest ya kina Hamis Chepelino. Akina Shaban Mtupa.!?
 
Acha kulialia. Mshauri huyo dogo asiye jielewa, afuate utaratibu. Hata huyo Samatta unayemtolea mfano, aliondoka simba kwa kufuata utaratibu;

Hao Tp Mazembe hawakumpa Samatta hela kwa siri, ili avunje mkataba na timu yake.
Sidhani kama atakuelewa jamaa mgumu kuelewa
 
Sahihi Kabisa Kaka ameshimdwa hata kujifunza kwa Luis Miquissone dogo analamba si chini ya 90M pale Club Al Ahly dogo alikiwasha sana hatua ya makundi Hadi akaonwq
90M [emoji3][emoji3][emoji3] sawa.
 
Mbeya unazungumzia uwanja mpaka uwanja Ngoma? Nimecheza pale na timu ya forest ya kina Hamis Chepelino. Akina Shaban Mtupa.!?
Sasa sisi tulikuwa tunacheza pale Mbatta, Samatta alikuwa hapendi kucheza uwanja ngoma... Aisee umenikumbusha mbali enzi za Saitama, Ghana Stars, Redstar, Mwanjelwa, Barcelona Mimi nimecheza na Misango Magae Diego.... Enzi zile tunacheza kaka yake Samatta, Mohamed ndio alikuwa maarufu,.. walikuwa wanakaa pale kota za polisi
 
Fei toto amesha sema hataki kuendelea kukaa yanga kwa sababu kapata timu iliyo bora kwake kimaslahi lakini mmemgangania tu.
Ingekua ni rahisi tu hivi mchezaji kuondoka maana yake mikataba isingekua na maana kwa sababu mchezaji akitaka tu kuondoka anasema anaondoka. Sheria ya mikataba haipo ivyo, yanga sio kwamba wamemzuia feisal kuondoka ila wanachotaka afate utaratibu hao tp mazembe walikaa na simba mezani wakamalizana.. Rage apewe phd ya heshima kwa kweli
 
Sure lazima kuwe Kuna "Mutual Agreement"
 
Sasa sisi tulikuwa tunacheza pale Mbatta, Samatta alikuwa hapendi kucheza uwanja ngoma... Aisee umenikumbusha mbali enzi za Saitama, Ghana Stars, Redstar, Mwanjelwa, Barcelona Mimi nimecheza na Misango Magae Diego.... Enzi zile tunacheza kaka yake Samatta, Mohamed ndio alikuwa maarufu,.. walikuwa wanakaa pale kota za polisi
Aisee safi sana Umecheza na Misango Diego!? very good to know you. Rafiki wa dogo Chale dogo mmoja hv alikuwa anakiwasha balaa. Yule dogo alikuja kuchezea Prison na kina Yona Ndabila nafikiri ni askari magereza sasahivi.
Sasa mimi nimechezea Forest pale uwanja ngoma na kina Hamis Chepe,Robo Mwasalemba, Maja tulikuwa na mzungu pori enzi hizo.
Kwa kifupi Mbeya kulikuwa na vipaji vya hatari sana. Ni vile kulikosekana watu wa kuviendeleza
 
Yes, kaka Misango ni Afande kwa Sasa... That's good memory Yani nikienda Mbeya lazima niende pale kiwanja Ngoma japo siku hizi hawachezi pale... Cheppe what a talent sijui yupo wapi siku hizi
 
Yes, kaka Misango ni Afande kwa Sasa... That's good memory Yani nikienda Mbeya lazima niende pale kiwanja Ngoma japo siku hizi hawachezi pale... Cheppe what a talent sijui yupo wapi siku hizi
Nadhani ni askari somewhere.
Kile kipaji mpaka leo kinaniuma hakikutendewa haki mpaka kimepotea bure.
 
Acha kulialia. Mshauri huyo dogo asiye jielewa, afuate utaratibu. Hata huyo Samatta unayemtolea mfano, aliondoka simba kwa kufuata utaratibu;

Hao Tp Mazembe hawakumpa Samatta hela kwa siri, ili avunje mkataba na timu yake.
Nyinyi utopolo mbona ndo vinara wa uvunjifu wa kanuni za soka hapa nchini na mnafumbiwa macho?
Hili jambo viongozi wa utopolo wangetumia busara tu wakamuachia dogo akaenda na sio kufanya mambo kwa ajili kumkomoa ili wamuharibie kijana mdogo kama huyo , maana hata utopolo imekuwa ikivunja kanuni za soka lakini wamekuwa TFF imekuwa ikitumia busara na kuwastiri.

Kwani hiyo roho ya kichawi mmemfanyia feisal peke yake ,nyinyi wachawi simlisha haribu dili la ngasa kwenda Sudani ambalo linge mpatia pesa kibao ambazo zinge badilisha maisha yake?

Utopolo ni kikundi cha wachawi Mungu atasimama na fei mwisho atakishinda kikundi hichi kiovu cha kichawi na kilicho jaa fikra za kimasikini.
 
Ingekua ni rahisi tu hivi mchezaji kuondoka maana yake mikataba isingekua na maana kwa sababu mchezaji akitaka tu kuondoka anasema anaondoka. Sheria ya mikataba haipo ivyo, yanga sio kwamba wamemzuia feisal kuondoka ila wanachotaka afate utaratibu hao tp mazembe walikaa na simba mezani wakamalizana.. Rage apewe phd ya heshima kwa kweli
Kwa mujibu wa vipengele vya mkataba alicho kifanya Fei ni sawa ila TFF imeliamuwa hili suala kisiasa na sio kikanuni.
 
Back
Top Bottom