rodrick alexander
JF-Expert Member
- Feb 12, 2012
- 16,784
- 23,312
Huyo mzazi unayemtaja hakuhusika kumrudisha Sammata Simba bali alirudi baada ya Simba kumtimizia ahadi yake ya gariUongo uko wapi Sasa!?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Huyo mzazi unayemtaja hakuhusika kumrudisha Sammata Simba bali alirudi baada ya Simba kumtimizia ahadi yake ya gariUongo uko wapi Sasa!?
Wewe huna akili pole sana na sijui unateseka ukiwa wapi!.Nyinyi utopolo mna roho za kichawi sana hata ngasa mlisha kuharibia dili la kwenda sudani ambalo linge mpatia pesa kibao hivyo nyinyi hatuwashangai.
We mbona ndo mwongo "inasemekana" hauna ushahidiPointi zako zimejaa uongo Sammata aliposajiliwa Simba aliweka masharti ya gari lakini Simba hawakutimiza na yeye hakuchezea Simba inasemekana alienda ureno baada ya Simba kufanya vibaya ikabidi wamfate wampe gari walilomwahidi hovyo akajiunga Simba baada ya miezi sita mechi yake ya kwanza ilikuwa na Mazembe akafanya vizuri yeye na Ochan , Mazembe walipoleta ofa Simba wakamruhusu
Umeongea ukweli mchungu muda utaamuaFeisal au fei toto ni mchezaji wa kawaida sana. Nawaza huyu kijana angekuwa anafanya mambo anayofanya chama ingekuwaje!!!
Watanzania sisi huwa tunaamua tu kumpaisha mtu na fei tumeamua tu kumpaisha ila hana tofauti na viungo wengi wazawa nchini.
Ww angalia mtu kama mandonga, piere, dokta shika na wengineo tuliwapaisha bila sababu za msingi, hata Fei anapitia eneo hili ila sema yeye yupo kwenye football.
Nimemuangalia sana huyu dogo ila sijaona ana kitu cha tofauti na wachezaji wengi wazawa nafikiri ni upepo wa kupaishwa tu umeamuangukia .
Ni taarifa ambayo sijathibitisha uwongo ni kama ningesema alienda kumbe hakwenda.We mbona ndo mwongo "inasemekana" hauna ushahidi
Pambana kwa hoja na sio mtoa hojaNi taarifa ambayo sijathibitisha uwongo ni kama ningesema alienda kumbe hakwenda.
Kama kiswahili lugha ya taifa unashindwa kuelewa inaonyesha walimu wako walikuwa na kazi kubwa
Soma uelewePambana kwa hoja na sio mtoa hoja
Kwani Fei hii ndio itakuwa mara ya kwanza kucheza hiyo michuano akiwa na Yanga?Sahihi Kabisa Kaka ameshimdwa hata kujifunza kwa Luis Miquissone dogo analamba si chini ya 90M pale Club Al Ahly dogo alikiwasha sana hatua ya makundi Hadi akaonwq
Feisal Salum (25) sio mtoto ana maamuzi yake binafsi habari za kila muda kusema wanaomshawishi inaonyesha wazi namna unavyoishi wewe kwa kupangiwa maamuzi na kushawishiwa na watu kwa kila jambo lako ndio unahisi Fei nae yupo hivyoKinachomsumbua Fei Toto ni utoto tu aliokuwa nao.
Angekuwa amekomaa kiakili, asingekubali kushawishiwa kirahisi na hao matapeli wa mpira wa miguu.
Fei hana mpango wa kuichezea tena Yanga na wala hajasema kuna timu inamtaka nashangaa Yanga wamekomaa kuwa hiyo timu inayomtaka ije mezani what if kama Fei anataka kuvunja mkataba ili aachane na masuala ya soka afanye mambo mengine sasa unapomshinikiza alete timu na wakati Yeye mchezaji yupo tayari kuuvunja kwa kuununua mkataba wake why msimpe hizo gharama za kuvunja mkataba awe free kijana wa watu kufanya anachopendaIngekua ni rahisi tu hivi mchezaji kuondoka maana yake mikataba isingekua na maana kwa sababu mchezaji akitaka tu kuondoka anasema anaondoka. Sheria ya mikataba haipo ivyo, yanga sio kwamba wamemzuia feisal kuondoka ila wanachotaka afate utaratibu hao tp mazembe walikaa na simba mezani wakamalizana.. Rage apewe phd ya heshima kwa kweli
Kwann wewe usiwe mzazi? Umeongea fact 100%Mbwana Samatta amekulia katika viunga vya Mbagala huko ndiko kuliko mtambulishan katika uga wa kandanda. Historia ya huyu mchezaji haikuwa rahisi kutoboa hadi kufikia hapo alipofikia. Kuna kipindi alikuwa anakosa hata sh. 200 ya nauli ya kumpeleka mazoezi. Waliokuwa karibu yake walimsaidia pesa ya nauli. Sina haja ya kueleza mengi kuhusu mchezaji huyu aliyecheza African Lyon kwa miaka miwili kuanzia 2008 hadi 2010 alipohamia club yake pendwa ya Simba SC. Kila mtu anayefuatilia na asiyefuatilia soka katika nchi hii anamjua Mbwana Samatta.
Ifahamike hapa, lengo sio kumzungumzia Mbwana Samatta, ila tu nataka nikukumbushe au niwakumbushe wachezaji wa Kitanzania njia alizopitia Mbwana Samatta.
Ndio, baada ya kuwika na African Lyon, 2008-2010 Mbwana Samatta alisajiliwa na Simba SC kwa ada ya usajili ambayo ni siri hadi leo lakini moja ya kipendele katika mkataba wake ilikuwa ni lazima Simba SC wampatie gari mpya aina ya Toyota Mark II Grand GX 110.
Siku zikaenda zikarudi lakini team yake ya Simba hawakutimiza ahadi ya kumpatia gari ambayo walimuahidi, Toyota Mark II Grand GX 110. Kumbuka kipindi hicho Samatta alishaanza kuteka mioyo ya wana Msimbazi wa uhodari wake wa kupachika nyavu… nini kilitokea??
Mbwana Samatta, AKAGOMA. Hii ilikuwa ni mwaka 2011 mwanzoni hapo club ya Simba inakabiliwa na mechi ngumu mbeleni dhidi ya TP Mazembe katika ligi ya Mabingwa Afrika.
Hapo ndipo akaibuka Kenny Mwaisabula Maarufu kama “MZAZI’’ huyu ni mmoja katika ya watu walimsaidia Mbwana Samatta katika makuzi ya kisoka. Hata zile mia mbili mia mbili za nauli za kwenda kwenye mazoezi Mbwana Samatta amepatiwa sana na huyu “MZAZI”
Kenny Mwaisabula, ‘’MZAZI’’ kupitia gazeti la Mwanasporti na kupitia ukaribu aliokuwa nao na Mbwana Samatta alimsihi sana kijana wake asigomee mazoezi wala mechi za Simba. Katika Makala yake hiyo ‘’MZAZI’’ alimuomba Mbwana Samatta aendelee tu kucheza mpira ipo siku atapata kile anachotaka kupitia huo mpira, cha msingi asiache mazoezi na aongezee bidii kwenye mechi kwani kwa kufanya hivyo ipo siku atapata na atakuwa na uwezo wa kununua Zaidi gari mia moja kama hiyo aliyoahidiwa na Simba.
Haikuishia hapo, ‘’MZAZI” akakaa na Mbwana Samatta nakumueleza kuwa Simba SC wapo kwenye ligi ya mabingwa Afrika na kama ataendelea kugoma hawezi kupata chance ya kucheza michezo hiyo mikubwa Zaidi kwa upande wa vilabu barani Afrika.
Ndipo Samatta akamsikiliza ‘’MZAZI’’ Kenny Mwaisabula. Akarudi Kambini. Mechi ya kwanza Simba akacheza na TP Mazembe ugenini tarehe 20/03/2011 na Samatta akiwa ndani Simba akafungwa 3-1 pale Lubumbashi.
Mechi ya pili pale taifa Mnyama anakufa tena 3-2 dhidi ya TP Mazembe magoal ya Simba yalifungwa na SHija Mkina dakika ya 58 kwa Assist ya Mbwana Samatta na goal la pili la Simba lilifungwa na Mbwana Samatta mwenyewe dakika ya 70. Hii mechi Mbwana aling’aa sana. Mwingine aliyeng’aa sana kwenye mechi hii ni Mganda Patrick Ochan. TP Mazembe wakaondoka na majina mawili, Patrick Ochan na Mbwana Samatta. Mwaka huo huo 2011, Mbwana Samatta na Patrick Ochan wakatua TP Mazembe.
Bila ushauri wa ‘’MZAZI’’ Mbwana Samatta angeendelea kugoma na angeendelea kugoma sidhani kama TP Mazembe wangemuona akiwa kwao Mbagala alisubiri GX 110 aliyoahidiwa na Simba SC.
Baada ya hapo wazungu wanasema ‘’the rest is history’’ kila mtu anajua ukwasi wa Captain Diego Mbwana Samatta, niliyecheza nae pale Mbeya viwanja vya MBATTA kipindi cha utoto wetu.
Bahati mbaya sana ndugu yetu Feisal Salum Abdallah ‘’FEITOTO’’ amekosa mtu kama ‘’MZAZI’’ katika carrier yake ya kucheza mpira, mtu ambaye anaona mbali na kukitazama mbali kipaji cha FEITOTO. Huyu mtu amekosekana katika maisha ya Feitoto. Watu walionyuma ya Feisal kwasasa ni wale watu ambao wamefikiri leo tu na sio kesho na kesho kutwa na huyu mchezaji.
Ndio, hakuna ubishi ya kuwa FEITOTO ameibeba sana Yanga katika mabega yake na anastahili kupata donge nono katika mshahara wake lakini njia alizotumia ni kama tu zile Hasira za mkizi. Timu yake ya YANGA inakaribia kuanza kucheza michuano ya kimataifa lakini yeye hayupo kikosini. Na bila shaka hii michuano ya Kombe La Shirikisho la Afrika ingekuwa ni Platform kwake kujitangaza kimataifa Zaidi na huenda angepata team nzuri nje ya Nchi ambayo ingekidhi mahitaji yake mara Zaidi ya watu wanaomrubuni kwasasa.
Naamini kabisa FEITOTO angekuwa na ‘’MZAZI’’ angeshauriwa aendelee kucheza huku akiendelea kubargain juu ya maslahi yake mapya kitu ambacho team yake ya YANGA wasingeshindwa kusimsikiliza.
Feisal Amekosa mtu kama Kenny Mwaisabula.
Nawasilisha.
N.B;
FEISAL SALUM FEITOTO RAMADHANI SINGANO A.K.A MESSI ANAOMBA UPOKEE SIMU YAKE ANAKUPIGIA
Endeleeni kumvimbisha kichwa, halafu tuone matokeo yake. Na aendelee hivyo hivyo na hayo maamuzi yake.Feisal Salum (25) sio mtoto ana maamuzi yake binafsi habari za kila muda kusema wanaomshawishi inaonyesha wazi namna unavyoishi wewe kwa kupangiwa maamuzi na kushawishiwa watu kwa kila jambo lako ndio unahisi Fei nae yupo hivyo
Fei ni mtu mzima ameshafanya maamuzi yake na unao waona nyuma yake ikiwemo wanasheria na wazazi wanasimamia maamuzi ya Fei
kibaya zaidi Feitoto anadhani hawa Externalities wanamtakia memaEndeleeni kumvimbisha kichwa, halafu tuone matokeo yake. Na aendelee hivyo hivyo na hayo maamuzi yake.
Maana hayana athari zozote zile kwa timu kubwa kama Yanga.
Samatta aliondoka kama Feisal? unasema watu hawana akili kumbe wewe ndio chizi kabisaOngeeni muongeavyo lakini kuanzia viongozi, mashabiki wa utopolo huwa mna roho za kichawi na kimasikini na wengi wenu hamna akili.
Fei toto amesha sema hataki kuendelea kukaa yanga kwa sababu kapata timu iliyo bora kwake kimaslahi lakini mmemgangania tu.
Simba walimuachia Samata kwenda mazembe baada ya kuona kule mazembe atapata maslahi kwa manufaa ya maisha yake lakini nyinyi hamta kumuachia Fei kwa ajili manufaa ya maisha yake badala yake nyinyi mnataka atumike kwa ajili ya maslahi yenu tu.
Ni aibu kwa mazee mazima yanayo jiita masomi kutumia nguvu kubwa kumiharibia ndoto kijana mdogo kama fei eti kwa ajili ya kumkomoa.
Mpeleke ChamaFeisal atafute team hata uarabuni atalipwa vizuri kuliko yanga wanamlisha mihogo tu
Sawa Samatta alikua anadai , Feisal anadai nini?Pointi zako zimejaa uongo Sammata aliposajiliwa Simba aliweka masharti ya gari lakini Simba hawakutimiza na yeye hakuchezea Simba inasemekana alienda ureno baada ya Simba kufanya vibaya ikabidi wamfate wampe gari walilomwahidi hovyo akajiunga Simba baada ya miezi sita mechi yake ya kwanza ilikuwa na Mazembe akafanya vizuri yeye na Ochan , Mazembe walipoleta ofa Simba wakamruhusu
Ungefatilia mada toka mwanzoni ungeelewa nini tunajadiliSawa Samatta alikua anadai , Feisal anadai nini?
Maelezo yako umesema Samatta aligoma mpka alivyo pewa gari swali langu ni Fei anadai nini mpka aanzishe mgomo?Ungefatilia mada toka mwanzoni ungeelewa nini tunajadili
Naona hutumii akili katika kufikiri simba walimuuza samatha na hawakumuachia na kama fei kapata timu aimbie iende mezani kuongea na yanga and dat's professionalism sio ngonjera zako Mpira ni biasharaOngeeni muongeavyo lakini kuanzia viongozi, mashabiki wa utopolo huwa mna roho za kichawi na kimasikini na wengi wenu hamna akili.
Fei toto amesha sema hataki kuendelea kukaa yanga kwa sababu kapata timu iliyo bora kwake kimaslahi lakini mmemgangania tu.
Simba walimuachia Samata kwenda mazembe baada ya kuona kule mazembe atapata maslahi kwa manufaa ya maisha yake lakini nyinyi hamta kumuachia Fei kwa ajili manufaa ya maisha yake badala yake nyinyi mnataka atumike kwa ajili ya maslahi yenu tu.
Ni aibu kwa mazee mazima yanayo jiita masomi kutumia nguvu kubwa kumiharibia ndoto kijana mdogo kama fei eti kwa ajili ya kumkomoa.
Samahani kwa kujibu text yako nimeona kama nuts zako zimefunguka hutafakari bali unajijibia tuuNyinyi utopolo mna roho za kichawi sana hata ngasa mlisha kuharibia dili la kwenda sudani ambalo linge mpatia pesa kibao hivyo nyinyi hatuwashangai.