Feisal Salum Feitoto amekosa mzazi

Hiyo timu mbona haijitokezi mezani kama Mazembe?!!!
 
Kwani ukimpa mtanzania maslahi yake kwa wakati kuna tatizo gani? Kwann lazima avumilie, apate shida? Haiwezekani akapewa fedha za kumwaga mapema tu? Ni lazima ateseke kwanzaaaa?
 
Samatta alivunja mkataba na Simba Kwa njia ya Feisal?
 
Kila mtu ana njia yake., acheni kuwatapeli local talents
 
Feisal atafute team hata uarabuni atalipwa vizuri kuliko yanga wanamlisha mihogo tu
 
Kama ndo hivo Kuna haja gani ya kua na mikataba???
 
Kwa mujibu wa vipengele vya mkataba alicho kifanya Fei ni sawa ila TFF imeliamuwa hili suala kisiasa na sio kikanuni.
Kuna nafasi ya feisal kwenda kwenye vyombo vya juu zaidi kudai haki yake acha tuone itakuaje akifanya ivyo
 
Kama ndo hivo Kuna haja gani ya kua na mikataba???
Ndo hapo sasa ushangae yaani mchezaji akitaka kuondoka wakati wowote timu imuachie sasa kuna haja gani ya kusaini miaka miwili, mitatu, mnne n.k. watu hawaelewi kwamba mchezaji na timu ni pande tofauti kwaiyo kila upande una haki ya kusimamia masilahi yake. Kama mchezaji akitaka kuondoka na timu ikakataa basi mchezaji anawajibika kuendelea kutumikia mkataba wake mfano feisal na yanga au timu ikataka kumtema mchezaji na mchezaji akakataa kuondoka basi timu inawajibika kumlipa mshahara na stahiki zake zote kwa mujibu wa mkataba mfano barcelona na de jong
 

Nimekuwa na jambo la kujifunza!
Nashukuru mno
 
Unapoteza muda wako bure kumuelimisha empty set
 
Yule mpiga kelele aliyeachwa nilisikitika majuzi anasema kwa madaha. Eti feisal huendi kokote unabaki hapa hapa.

nikaamini alivyosemaga pale yanga wenye akili ni wawili ni kweli maana hata yy kashakosa akili alivyoenda huko.
Mzee Mpili juzi kapeleka watu polisi baada ya kuzidiwa hoja, alikwenda kijiwe chale magomeni mwembechai akasema Feitoto hatacheza mpira akatokea mtu akamjibi hivi wewe huo uwezo unaomtishia feitoto unafikiri ni wewe peke yako unao hebu acha mambo ya akaweka tusi Mzee kakasirika kaenda polisi ila polisi wakaona kesi ya kipuuzi wakampuuzia kurudi wakamwambia kama huwezi matani usiwe unatania
 
Pointi zako zimejaa uongo Sammata aliposajiliwa Simba aliweka masharti ya gari lakini Simba hawakutimiza na yeye hakuchezea Simba inasemekana alienda ureno baada ya Simba kufanya vibaya ikabidi wamfate wampe gari walilomwahidi hovyo akajiunga Simba baada ya miezi sita mechi yake ya kwanza ilikuwa na Mazembe akafanya vizuri yeye na Ochan , Mazembe walipoleta ofa Simba wakamruhusu
 
Hap
Hapo na wewe unajiona binge la mwandishi na mtoa ushauri kumbe yote uliyoandika hapa no uhalo mtupu...
 
Uongo uko wapi Sasa!?
 
Feisal au fei toto ni mchezaji wa kawaida sana. Nawaza huyu kijana angekuwa anafanya mambo anayofanya chama ingekuwaje!!!

Watanzania sisi huwa tunaamua tu kumpaisha mtu na fei tumeamua tu kumpaisha ila hana tofauti na viungo wengi wazawa nchini.

Ww angalia mtu kama mandonga, piere, dokta shika na wengineo tuliwapaisha bila sababu za msingi, hata Fei anapitia eneo hili ila sema yeye yupo kwenye football.

Nimemuangalia sana huyu dogo ila sijaona ana kitu cha tofauti na wachezaji wengi wazawa nafikiri ni upepo wa kupaishwa tu umeamuangukia .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…