Feisal Salum kakosa Elimu na Akili

Feisal Salum kakosa Elimu na Akili

Wataomchangia hizo pesa nao hamnazo. Ila acha aende CAS, aangukie pua ndio arudi chini kujipanga na upya.

Namuonea huruma kwani atavyoshindwa case CAS, itambidi alipe gharama Yanga atazotumia kwenye case.
Wanasheria wanavyomdanganya ni kuwa, ni kweli atashindwa kesi CAS, ila kwa vile Mchezaji hana furaha na Team yake, Watavunja Mkataba wake kwa yy kupigwa Fine, then hiyo Team inayomtaka itamlipia fine basi.
 
Unaamini Mtu aliepeleka milioni 115 kuvunja mkataba anakosa millioni 57 ?

Unaamini atashindwa vipi endapo atashinda?
Una amini akitoa hiyo 57M kwenye ile 112M akafungua jalada halafu CAS wakaamua kuwa mkataba uvunjwe na Feisali arejeshe hizo 112M, bado ile 112 itakuwepo?

Ni mahesabu gani haya ambayo mnapiga nyinyi ambao mnamkosoa Feisali kuhusu akili?
 
Labda wewe ndio haujui taratibu za kuvunja mkataba wa mchezaji, mtu kaambiwa aende klabuni kwake au apeleke barua apewe gharama za kuvunja mkataba au timu unayo mtaka ipekele offer anazurula hapo TFF anapoteza mda, hata huko CAS anaenda kupoteza mda wake
Yanga haina taarifa kuwa Fei anataka kuvunja mkataba?
 
Wanasheria wanavyomdanganya ni kuwa, ni kweli atashindwa kesi CAS, ila kwa vile Mchezaji hana furaha na Team yake, Watavunja Mkataba wake kwa yy kupigwa Fine, then hiyo Team inayomtaka itamlipia fine basi.
Kwani CAS yeye anaenda kushtaki kuwa nini kimetokea?
 
Hoja hapa ni mkataba halali aliosaini kwa hiari...ckuiz hakuna mambo ya kupenda timu wala sio takwa la mkataba.....
Hoja sio mkataba halali tu, Hoja pia ni iwapo huo mkataba una kipengele kinachomruhusu kununua mkataba wake au la. Na kama kipo kwa taratibu zipi.
 
Hakika elimu ni ukombozi wa maisha. Ukiwa umeelimika inakuwa sio rahisi mtu kukushikia akili, ukiwa na elimu sio rahisi kuendeshwa kama gari bovu, ukiwa na elimu sio rahisi kutumiwa kwa maslahi ya mtu bila wewe kujua.

Hata hivyo:

Unaweza kukosa Elimu ya kutosha lakini ukajaaliwa kuwa na Akili kubwa kuliko hata ya mwenye Elimu ,mfano mzuri ni kwa mchaga, mkinga na mpemba aliyeishia la nne ana akili kubwa ya biashara kuliko professor wa UDSM.
Na ndio maana wapo walioishia std 7 lakini wana akili kubwa sana na sio rahisi kushikiwa akili, sio rahisi kudanganywa, sio rahisi kuendeshwa.

Feisal yeye amekosa vyote, AKILI na ELIMU, ameshikiwa tu akili kwa maslahi ya hao waliomshikia akili. Nadhani angekuwa anacheza soka Ulaya angekuwa kama yule mchezaji nadhani anaitwa Eboue aliyefilisiwa mali na Mke. Eboue alikosa akili ya kujua dhamira ya ndani ya mke anayemuoa. Lakini tunashuhudia akili kubwa ya Hakhim jinsi alivyompiga chenga mke tapeli.

Kukosa Elimu ni bora kuliko Kukosa AKILI
Mkuu, maelezo yako

Mkuu, huenda maelezo yako ni mazuri, lakini umekosea kitu kimoja; kutoa mfano hasi kwa kuwapoint watu (kikundi). Ulitakiwa tu kuishia maprofessor, lakini sio maprofessor wa chuo fulani. Hakuna mtu ambaye lingemgusa moja kwa moja. Hilo ni shambulio la maneno, na kama humu id zetu zingekuwa halisi, huenda ungetafutwa na kufunguliwa mashitaka!
 
Yanga taarifa hiyo wataipata wapi!? Mchezaji haonekani kambini!? anakiuka masharti ya mkataba wa kuutumikia timu....

Anaandikiwa barua hajibu .....anazurula TFF....TFF wanamrudisha Klabuni akafuate TARATIBU ..,atekelezi...

Yanga sio wajinga.
Hapo Yanga taratibu za kudeal na mchezaji mtoro wa muda mrefu ni zipi?
 
Dogo ana kipaji cha kucheza mpira! Halafu amenyimwa akili ya kuchanganua mambo. Kweli inasikitisha na kuhuzunisha sana.

Yaani mkataba ulikuwa unaisha mwakani tu 2024, na hivyo angeweza kuondoka kama free agent! Alikuwa ana uwezo wa kukaa mezani na timu yake, ili kuboreshewa mkataba wake! Ila ndiyo hivyo tena. Ameamua kuchagua njia ya mkato.
Unajua kinachokuja kufurahisha hapa kwenye huu uzi ni kuona mashabiki wa Yanga wanavyo nyoosheana vidole kuhusu mwenzao wakimtilia mashaka uwezo wake wa akili.

Mashabiki ambao nahakika miongoni mwao hakuna Sunday Manara wala Kikwete

Hivi nyie mko serious kweli?
 
Hoja sio mkataba halali tu, Hoja pia ni iwapo huo mkataba una kipengele kinachomruhusu kununua mkataba wake au la. Na kama kipo kwa taratibu zipi.
Taratibu ziko ndani ya huo Mkataba halali....vipengele vya mkata dhidi yake vimewahi kiukwa...au kutokutekelezwa?!

Hoja ni Mkataba kwanza....Haki za wawili hawa ktk mkataba zimelindwa!?
 
Hapo Yanga taratibu za kudeal na mchezaji mtoro wa muda mrefu ni zipi?
Si ndio wanamshitaki ktk kamati ya Yanga ya nidhamu na Hadhi za wachezaji...

Subirini huko ndiko maumivu yanaanza kutengenezwa [emoji16]
 
Taratibu ziko ndani ya huo Mkataba halali....vipengele vya mkata dhidi yake vimewahi kiukwa...au kutokutekelezwa?!

Hoja ni Mkataba kwanza....Haki za wawili hawa ktk mkataba zimelindwa!?
Na ndo maana nikasema kuna jambo Yanga na Fei hawasemi.

Fei hajasema ametumia vipengele vipi vya mkataba kuvunja mkataba wake. Na Yanga hawasemi ni taratibu zipi anazokiuka Fei ambazo zipo kwenye mkataba wake.
 
Si ndio wanamshitaki ktk kamati ya Yanga ya nidhamu na Hadhi za wachezaji...

Subirini huko ndiko maumivu yanaanza kutengenezwa [emoji16]
Haya ngoja tuone watakuja na adhabu gani ambayo mwisho wake si kumwachia huru Fei.
 
Na ndo maana nikasema kuna jambo Yanga na Fei hawasemi.

Fei hajasema ametumia vipengele vipi vya mkataba kuvunja mkataba wake. Na Yanga hawasemi ni taratibu zipi anazokiuka Fei ambazo zipo kwenye mkataba wake.
Yanga si wamemuita Klabuni na kumuelekeza Nini anatakiwa kufanya ...au!?
 
Tatizo ni kukosa Akili ya kujua kuwa waliomshauri walikuwa na jambo lao lingine . Kimsingi ni baadhi ya wa Nazi wa Simba waliotaka kuiletea Yanga Frustration ili isisonge mbele na bahati nzuri wamepata aibu kubwa sana Makolo na Feisal
Id yako umenikumbusha mistari ya Dizasta

Muite shosti bitozi, muite mpoki na joti...

Muite poti na soja.....(muite, muite, muite)

Muite vina kikosi, muite bwana misosi tujumuike pamoja....
 
Back
Top Bottom