Feisal Salumu: Nimeondoka Yanga kutokana na manyanyaso, nilizungumza na Rais wa Yanga kwa saa 6, nikamwambia nataka kuondoka

Feisal Salumu: Nimeondoka Yanga kutokana na manyanyaso, nilizungumza na Rais wa Yanga kwa saa 6, nikamwambia nataka kuondoka

Yaani honestly kipo kinafichwa kikubwa tu kustiri utu wa hao wawili ila twende tu ..tutajua tuu kwani Yana muda baasi!!!
Si rahisi kukataa kurudi yanga na fei sikutegemea km ataondoka Yanga miongoni mwa wachezaji wenye mapenzi na Yanga ni naweza sema anaongoza..
Na mzanzibar akisema noooo....amemaanisha NOOO Tena kubwaa
Jamaa ana msimamo haswa. Naskia alipewa ofa mpaka ya 30m kaigomea. Anasema Hersi hajui kamuandalia nn kambini.
 
👉Nimenyanyaswa sana nikiwa Yanga,nimeambiwa nauza mechi na viongozi.

👉Nimekaa na Hersi na Makamu wake masaa 6 nikamwambia yanayonisibu dhidi yake akaniomba radhi akasema tusameheane nikamwambia nimekusamehe lakini nataka kuondoka.

Akasema sisi bado tunakuhitaji, nikamwambia mimi siwezi tena kuendelea na Yanga, naomba niondoke.

Akasisitiza nibaki nikamwambia basi wanipe siku 3 niongee na familia yangu.

👉Mkataba huu nilio nao wakati nasaini mama aliniambia nitasaini mkataba wa miaka 2 lakini Hersi akaniongezea ikawa 3 bila mimi kujua.

👉Mkataba uliandikwa Kingereza na mimi Kingereza sijui na nilikuwa pekeyangu. Wao walikuwa Saimon, Hersi, Arafat na Mdhamini.

👉Mama yangu ni mpenzi mkubwa sana wa Yanga na yeye ndiye aliyenipambania wakati Yanga mambo yakiwa mabaya alikuwa ananipa pesa yake mwenyewe.

👉Nimekula Ugali na Sukari wakati Yanga ikiwa na hali mbaya sio sasahivi.

👉Wanamtukana na kunyanayasa pepo yangu, mama yangu ndiyo pepo yangu mimi halafu anafananishwa na andazi kweli?

👉Nawapenda sana mashabiki wa Yanga na najua wananipenda pia, hawajui niliyopitia wanaambiwa uongo wanamtukana mama yangu na mimi mwenyewe.

👉 Simkimbii Hersi nimkimbie ili iweje Kwani Mimi nimeua? Nimekaa nae yeye na Makamu wake masaa 6

My Take
Msimamo wangu ni kwamba Yanga sio club ya kwenda mtu makini. Imejaa uhuni na wahuni
YANGA na MAKOLO ni club za ujanjaujanja!
 
Hivi huyu dogo ana elimu gani?
Ama kweli huyu ni bora angezaliwa mwanamke. Kuna faida gani kuzaliwa mwanaume halafu akili ni ya mama? Kila saa mama !
Aondoe ubin wa baba aweke wa mamake!
Amesomea Hakimiology...
 
Hapa lazima kuna Jambo nyuma ya pazia ambalo linashindwa kuwekwa hadharani.
Haiwezekani Mchezaji aamue kugoma tu bila sababu yoyote kuifanya kazi yake.
Kufikia hii hatua lazima Fei yalimpata makubwa.
 
Ndio najikuliza kama umemuajiri mtu na hatimizi majukumu uliyompa, ww kama mwajiri kwanini usivunje mkataba nae, na akulipe kufidia hasara aliyokuletea.
Na fei kujua hilo karudisha pesa ya signing fee na mshahara wa miezi 3, lakini waajiri hawatakii eti. [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kwahiyo CR7 na Achraf Hakim hawana akili?
Mkuu, Hakimi hakuwahi kudeka kwa mama yake. Hakimi aliona namna anavyo enda kunasa kwenye tego la mshangazi ndipo akaamua kumrithisha mama yake kila kilicho chake
 
Yani Hersi atume watu wamtukane Feisail na Mama?!

Nitakua wa mwisho kuamini hii. Kuhusu mkataba naweza kuamini, Bongo magumashi mengi.

Tusubiri upande wa pili kama wataona inafaa kujibu.
Mimi nitakuwa wa pili kutoka mwisho, maana wa mwisho si umeshawahi nafasi wewe
 
Timu inakunyanyasa wakati huo huo inakupa offer ya million 30 hivi mbona nyie watu hamtumii akili?
Fei Yanga haimnyanyasi ananyanyaswa na Hersi. Ana matatizo na Hersi. Ni mambo binafsi ila Hersi anatumia nafasi yake kumtandika na amevumilia kachoka hataki tena. Hata huko alipoenda anajua kisheria anaweza shindwa ila anafikiri maelekezo ya adhabu atakayopewa yana nafuu kuliko anachotaka Hersi sababu Hersi hataki kumuachia anataka kumnyoosha ndo maana hataji pesa yoyote anayotaka kutoka kwa Fei anataka aripoti kambini na timu inayomtaka ije, yeye anasema hakuna timu inamtaka.

Weka Uyanga pembeni, mtazame Fei na Hersi.
 
"niliambiwa na viongozi wa Yanga kuwa nauza mechi iliniuma sana na nikipokuwa nawapigia simu hao viongozi waliokuwa wanatamka hayo maneno hawapokei simu yangu.

"Viongozi walikua wanamtukana mama yangu na kutoa matusi ya kumnyanyasa hata ingekua ni wewe ndugu mwandishi usingekubali kutukaniwa mzazi"

"Kula ugali kwa sukari sikula saivi nilikula kipindi kile timu bado ilikua ipo chini kiuchumi na kuna muda tulicheleweshewa mishahara lakini Mama aliniambia vumilia mwanangu maana alikua ni mpenzi wa mkubwa wa Yanga.

"Mama kuna muda mwingine alinipa pesa yake tulipokua tumecheleweshewa mshahara."

Mwandishi: Tueleze umepitia manyanyaso gani?

"Naambiwa nauza mechi, viongozi wananitukana na nikiwaambia familia wanasema nivumilie.

"Mama yangu alikuja Dar wakamtukana na kuanza kumpa maneno ya kejeli."

"Huyo huyo Raisi anatuma watu wamtukane mama yangu wanamuita mama yangu andazi "

Wanitukane Mimi lakini siyo mama yangu maana mama yangu ni pepo yangu"

"Nimekaa masaa sita na Engineer Hersi kuwa hapa nilipofikia nataka niachane na Yanga na Hers alisema kuwa bado anahitaji huduma yangu"

Raisi: anampigia simu mama na mama aliniambia niende kusaini mkataba na mama alimwambia mpe Fei mkataba wa miaka miwili"

Hers aliongeza mwaka mmoja badala ya miaka miwili"

"Mimi sijui kiingereza walinipa mkataba wa miaka mitatu"

"Signing fee sijapewa kwa wakati nilipewa kidogo kidogo tena kwa kutumiana meseji za vitisho"

"Nataka kukusanya milioni 60 niende CAS na watanzania wengi wananichangia na utaratibu umeanza tunasubiri invoice"

"Unajua yanga ni taasisi kubwa na Mimi ninawapenda wanayanga nilimwambia hers ata Kama alinikosea Ila nilimwambia tukae chini tumalizane na hers alikili makosa yake lakini Mimi nilitaka tuachane nikatafute maisha sehemu nyingine"

"Nilimwambia eng Hers bmkubwa alikuambia Miaka miwili lakini ukanipa mitatu lakini hers hakunijibu"

"Familia yangu wanaipenda Yanga lakini kilichonitoa Yanga ni manyanyaso"

"Hakuna timu inayonitaka na ndiyo maana nilitaka kuvunja mkataba niende kutafuta maisha yangu pengine"

"Tumekaa na familia yangu niliona Bora tuvunje mkataba na niliwaomba viongozi tuachane nilichangiwa pesa na familia"

"Mimi siwezi kula dhuluma siwezi kula pesa ambayo siifanyii kazi na ndiyo maana wakituma pesa zinarudi"

"Mimi sipendi hizi kelele nataka hili Jambo liishe na nafsi yangu haitaki kucheza Yanga na ndiyo maana nilikaa nao chini viongozi chini tuyamalize nikatafute maisha sehemu nyingine"

",Kama Jambo litakua haliishi ni bora nikae nyumbani maana ndiyo mwenyezimung atakua amepanga hivyo" kipaji kuisha.

"Hers anasema nauza mechi kun pass moja nilimpa Mayele aongeze magoli mbele ya kipa lakini Mayele alikosa hapo Hers akaanza kusema kuwa nauza mechi"

"Nilimtafuta GSM aje kutafuta suluhu lakini hakupokea simu zangu lakini aliposikia sakata Hili ndiyo akaanza kunitafuta na Mimi sikupokea simu yake"

"Nilikutana Hers akasema kuwa anataka nirudi Yanga nilikataa basi akaniambia niende CAS"

"Hers anadharau kubwa sana na Msolwa alikua ni mkarimu sana"

"Watu hawajiulizi ni kwa nini Fei hajaondoka katika kipindi kile Cha Yanga ngumu lakini nimeondoka kipindi hiki kizuri".

"Mimi nina matatizo na Raisi wa club Sina Tatizo na club Ila hers ndiyo Raisi wa club ndiyo Nina tatizo nae"

"Mpaka Sasa hela haijatosha Ila nashukuru Watanzania wameshanichangia kiasi cha shilingi milioni tisa (9)

"Mimi Nina rafiki na ndugu na wengine wapo humo humo ndani ya klabu ya yanga ndiyo walinichangia kurudisha pesa ili nivunje mkataba."

"Naitakia kila la heri Yanga katika fainali yake huko Algeria na nitaiombea Dua mungu ifanye vizuri"

"Mimi nimeongea yote lakini nafsi yangu haitaki kurudi kabisa Yanga sc"
AENDE TUU ASITUCHOSHE!YANGA IPO NA ITAENDELEA KUWEPO!WALIONDOKA KINA SUNDAY MANARA,OMAR MWAMBA KAPERA,GIBSON SEMBULI,KITWANA MANARA POPAT, WAKAJA KUONDOKA KINA LUNYA,KIZOTA,MAMCHINGA ETC!NA YANGA BADO IPO!SEMBUSE HUYU FEISAL!FEISAL NANI BANA MBELE YA YANGA!!!YANGA IMEANZISHWA 1935 NA IPO HADI LEO!WAMEPITA WACHEZAJI GANI WAZURI PALE??ASITUTISHE SISI
 
Kitendo cha feisal kusema amesaini mkataba kwa lugha ya kiingereza wakati yeye hajui lugha hyo hapo tayari feisal ameshinda kesi tayari hata Simon msuva alishinda kesi yake kwasababu alisaini mkataba ambao hajui ndani kumeandikwa nn na hakuwa na shahidi wala mwanasheria na nikinyume na utaratibu unavyotakiwa feisal kashinda kesi tayari mwanasheria wa yanga ni miongoni mwa wanasheria vilaza kuwahi kutokea Tanzania hajawahi shinda kesi yoyote.
 
Back
Top Bottom