[emoji117]Nimenyanyaswa sana nikiwa Yanga,nimeambiwa nauza mechi na viongozi.
[emoji117]Nimekaa na Hersi na Makamu wake masaa 6 nikamwambia yanayonisibu dhidi yake akaniomba radhi akasema tusameheane nikamwambia nimekusamehe lakini nataka kuondoka.
Akasema sisi bado tunakuhitaji, nikamwambia mimi siwezi tena kuendelea na Yanga, naomba niondoke.
Akasisitiza nibaki nikamwambia basi wanipe siku 3 niongee na familia yangu.
[emoji117]Mkataba huu nilio nao wakati nasaini mama aliniambia nitasaini mkataba wa miaka 2 lakini Hersi akaniongezea ikawa 3 bila mimi kujua.
[emoji117]Mkataba uliandikwa Kingereza na mimi Kingereza sijui na nilikuwa pekeyangu. Wao walikuwa Saimon, Hersi, Arafat na Mdhamini.
[emoji117]Mama yangu ni mpenzi mkubwa sana wa Yanga na yeye ndiye aliyenipambania wakati Yanga mambo yakiwa mabaya alikuwa ananipa pesa yake mwenyewe.
[emoji117]Nimekula Ugali na Sukari wakati Yanga ikiwa na hali mbaya sio sasahivi.
[emoji117]Wanamtukana na kunyanayasa pepo yangu, mama yangu ndiyo pepo yangu mimi halafu anafananishwa na andazi kweli?
[emoji117]Nawapenda sana mashabiki wa Yanga na najua wananipenda pia, hawajui niliyopitia wanaambiwa uongo wanamtukana mama yangu na mimi mwenyewe.
[emoji117] Simkimbii Hersi nimkimbie ili iweje Kwani Mimi nimeua? Nimekaa nae yeye na Makamu wake masaa 6
My Take
Msimamo wangu ni kwamba Yanga sio club ya kwenda mtu makini. Imejaa uhuni na wahuni