Feisal Salumu: Nimeondoka Yanga kutokana na manyanyaso, nilizungumza na Rais wa Yanga kwa saa 6, nikamwambia nataka kuondoka

Jamaa ana msimamo haswa. Naskia alipewa ofa mpaka ya 30m kaigomea. Anasema Hersi hajui kamuandalia nn kambini.
 
YANGA na MAKOLO ni club za ujanjaujanja!
 
Hivi huyu dogo ana elimu gani?
Ama kweli huyu ni bora angezaliwa mwanamke. Kuna faida gani kuzaliwa mwanaume halafu akili ni ya mama? Kila saa mama !
Aondoe ubin wa baba aweke wa mamake!
Amesomea Hakimiology...
 
Hapa lazima kuna Jambo nyuma ya pazia ambalo linashindwa kuwekwa hadharani.
Haiwezekani Mchezaji aamue kugoma tu bila sababu yoyote kuifanya kazi yake.
Kufikia hii hatua lazima Fei yalimpata makubwa.
 
Ndio najikuliza kama umemuajiri mtu na hatimizi majukumu uliyompa, ww kama mwajiri kwanini usivunje mkataba nae, na akulipe kufidia hasara aliyokuletea.
Na fei kujua hilo karudisha pesa ya signing fee na mshahara wa miezi 3, lakini waajiri hawatakii eti. [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kwahiyo CR7 na Achraf Hakim hawana akili?
Mkuu, Hakimi hakuwahi kudeka kwa mama yake. Hakimi aliona namna anavyo enda kunasa kwenye tego la mshangazi ndipo akaamua kumrithisha mama yake kila kilicho chake
 
Yani Hersi atume watu wamtukane Feisail na Mama?!

Nitakua wa mwisho kuamini hii. Kuhusu mkataba naweza kuamini, Bongo magumashi mengi.

Tusubiri upande wa pili kama wataona inafaa kujibu.
Mimi nitakuwa wa pili kutoka mwisho, maana wa mwisho si umeshawahi nafasi wewe
 
Timu inakunyanyasa wakati huo huo inakupa offer ya million 30 hivi mbona nyie watu hamtumii akili?
Fei Yanga haimnyanyasi ananyanyaswa na Hersi. Ana matatizo na Hersi. Ni mambo binafsi ila Hersi anatumia nafasi yake kumtandika na amevumilia kachoka hataki tena. Hata huko alipoenda anajua kisheria anaweza shindwa ila anafikiri maelekezo ya adhabu atakayopewa yana nafuu kuliko anachotaka Hersi sababu Hersi hataki kumuachia anataka kumnyoosha ndo maana hataji pesa yoyote anayotaka kutoka kwa Fei anataka aripoti kambini na timu inayomtaka ije, yeye anasema hakuna timu inamtaka.

Weka Uyanga pembeni, mtazame Fei na Hersi.
 
AENDE TUU ASITUCHOSHE!YANGA IPO NA ITAENDELEA KUWEPO!WALIONDOKA KINA SUNDAY MANARA,OMAR MWAMBA KAPERA,GIBSON SEMBULI,KITWANA MANARA POPAT, WAKAJA KUONDOKA KINA LUNYA,KIZOTA,MAMCHINGA ETC!NA YANGA BADO IPO!SEMBUSE HUYU FEISAL!FEISAL NANI BANA MBELE YA YANGA!!!YANGA IMEANZISHWA 1935 NA IPO HADI LEO!WAMEPITA WACHEZAJI GANI WAZURI PALE??ASITUTISHE SISI
 
Kitendo cha feisal kusema amesaini mkataba kwa lugha ya kiingereza wakati yeye hajui lugha hyo hapo tayari feisal ameshinda kesi tayari hata Simon msuva alishinda kesi yake kwasababu alisaini mkataba ambao hajui ndani kumeandikwa nn na hakuwa na shahidi wala mwanasheria na nikinyume na utaratibu unavyotakiwa feisal kashinda kesi tayari mwanasheria wa yanga ni miongoni mwa wanasheria vilaza kuwahi kutokea Tanzania hajawahi shinda kesi yoyote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…