Feisal Salumu: Nimeondoka Yanga kutokana na manyanyaso, nilizungumza na Rais wa Yanga kwa saa 6, nikamwambia nataka kuondoka

watu wengi ambao mnauelewa mdogo wa kufikiri mnarukia kwenye cheap issues lakini hamtizami tatizo kuu. wachezaji wengi hasa wa kitanzania wana changamoto ya elimu kutokana na mfumo uliopo wa maisha yetu kwamba shule ikikushinda unakimbilia mpira na kipaombele ni kupata pesa tu bira kutizama mustakabari mzima wa maisha.

maana yake mpira haukua kama ajira rasmi. na hapo TFF na baraza la michezo liliunda sheria na kanuni za kulinda haki za wachezaji na vilabu. Lakini kwakua soka letu limeshakua TFF na baraza la michezo linatakiwa liunde chombo rasmi kinachojitegemea kwaajili ya kusikiliza kesi zinazowahusu wachezaji na vilabu vya mpira.

hilo halijafanyika hivyo ni kasoro kwasababu wachezaji wetu wandani hawana uwezo wa kumudu gharama za kwenda CAS badala yake wangeweza kufungua kesi katika mahakama za michezo hapahapa Tanzania.

wapo wachezaji wengi tu wanachangamoto kama alizonazo Feisal lakini kwasababu ya ukubwa wa Jina alilonalo Feisal ndio maana linatizamwa kwa ukubwa lakini ukweli wapo wengi.

so ni muda muafaka sasa wa Rais wa TFF kushirikiana na Waziri wa michezo kuanzisha mchakato wa mahakama ya michezo.

Sent from my TECNO KB7j using JamiiForums mobile app
 
Feisal laani inamuandama.

Timu za Yanga na Simba si za kuzichezea, angeondoka kwa kufuata taratibu na si kwa kujifanya mjuwaji.




Bandiko alihusiani na hii thread.
 
Tusi NI neno ambalo litamkera mtu, Kama Hersi alijibu neno la hovyo yeye akidhani ni jepesi basi limemkera mama na mtoto. Na Kama hakutukana kwa nini Fei anasema Eng. alimuomba msamaha? Kuwa wa mwisho ni hiari ya mtu mkuu.
Kwa hiyo ni kweli Hersi alimtukana Mama Fei akamuita andazi na ndio maana akamuomba msamaha?! Andazi?! Andazi?! Andazi?!
 
Nakazia asikilizweeee [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Safi sana Feisal kwa kupigania haki yako... inshaallah utawashinda hawa watesi wako.
 
Naunganaa na wee. Uko sahihi
 
Feisal laani inamuandama.

Timu za Yanga na Simba si za kuzichezea, angeondoka kwa kufuata taratibu na si kwa kujifanya mjuwaji.

View attachment 2642385


Bandiko alihusiani na hii thread.
Ushabiki bana. Fei ameshasema hana tatizo na Yanga ana tatizo na Hersi, ila bado unaiingiza Yanga. Au Hersi ndo Yanga? Mnasahau kuwa kunaweza kuwa na tabia binafsi za viongozi ambazo sio tabia za club. Hapa Hersi anatakiwa aulizwe una tatizo gani binafsi na Fei? Maana anasema ana shida na wewe sio Yanga.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…