Feisal Salumu: Nimeondoka Yanga kutokana na manyanyaso, nilizungumza na Rais wa Yanga kwa saa 6, nikamwambia nataka kuondoka

Feisal Salumu: Nimeondoka Yanga kutokana na manyanyaso, nilizungumza na Rais wa Yanga kwa saa 6, nikamwambia nataka kuondoka

Kwahiyo Hersi kamzunguka kijana ama??!!
Haya Sasa ndio madhira wanayokutana nayo wachezaji wa ndani, wengi wao shule imepita mbali. Wengi hutumia wapambe kama wanasheria, mpambe mwenyewe naye hakwenda shule. Inasikitisha sana mtu tunaye amini ni professional kuongea vitu kama hivi.

Hawa watoto wetu tuwasisitize kupenda michezo na shule pia. Sio kumwambia mtoto mbona wachezaji Wana fedha zaidi ya wasomi
 
Nilichogundua jamaaa Hana msimamo, ameshikiwa akili na familia
 
Kama haya ndiyo mambo yanayopelekea aende CAS ili wavunje mkataba,ameula wa chuya.

1.Mama yangu ametukanwa
2.Viongozi waliniambia nimeuza mechi
3.Mama yangu anaitwa andazi.

Dogo ameulizwa ishu za kimkataba zilizofanya asitishe mkataba amebaki kujing'ata ng'ata tu.

ELIMU,ELIMU,ELIMU,ELIMU,ELIMU
 
Kama haya ndiyo mambo yanayopelekea aende CAS ili wavunje mkataba,ameula wa chuya.

1.Mama yangu ametukanwa
2.Viongozi waliniambia nimeuza mechi
3.Mama yangu anaitwa andazi.

Dogo ameulizwa ishu za kimkataba zilizofanya asitishe mkataba amebaki kujing'ata ng'ata tu.

ELIMU,ELIMU,ELIMU,ELIMU,ELIMU
Hizo pointi unazichukulia poa? Hapo maana yake hakuna mazingira Bora ktk utekelezaji wa mkataba husika Mtu Hana elimu ya kutosha, ulitegemea aongee vipi
 
Amijei anajichanganya tu ,kama ana tatizo na Rais wa Club na siyo Yanga ,sasa si adili na huyo rais direct?
 
Hakuna kipengele kilichopo kwenye mkataba kilichovunjwa,CAS wataangalia mkataba unasemaje na unatekelezwaje
Nimeongelea mazingira ya utekelezaji wa mkataba. Je mazingira yalikua favorable Kwa pande zote mbili.
 
Sitatoa coment ya maana mpaka mahojiano na ya Feisal na Clouds yatakapo isha ila mpaka hapo mahojiano yalipo fik.

Engineer Hersi ni TAPELI na ni mtu mbaya sana kwa alicho mfanyia mchezaji na kwa namana inavyo onekana huenda kuna wachezaji wengine wanayapitia haya kimya kimya hawaja taka kujitokeza tu.

Alitumia udhaifu wa Fei kuto kujua kingereza na kutokua na wakala wala mwanasheria kumkandamiza hii ni mbaya sana.
 
Nimeongelea mazingira ya utekelezaji wa mkataba. Je mazingira yalikua favorable Kwa pande zote mbili
Kama mazingira hayakuwa favorable watamwambia harudi wakae chini na Yanga wavunje mkataba,hilo ndilo Yanga wanamtaka lakini yeye hataki.

Hata kama mazingira hayakuwa favourable huwezi kuvunja mkataba kihuni,ingekuwa hivyo kila siku tungekuwa tunaona wachezaji wanavunja mikataba wanaondoka kiholela,yeye anachopaswa ni kwenda kwenye uongozi wa Yanga na kukaa chini na kukubaliana wavunje mkataba kila mtu ashike hamsini zake.
 
Nipo upande wake lakini hapo kwenye kutokujua mkataba unasemaje sababu ni wa kingeleza namlaumu. Kwanini asaini dili kubwa kama hii bila kuwa na mtalamu wa hata mambo
Hili limefanya hata hayo mengine nisimuamini
 
Chuki za kishamba hizi,
Huyu dogo Kuna watu wanampotosha kwa maslahi Yao BINAFSI[emoji3525]
Hizo chuki unazo wewe mkuu, hayo ni maisha ya mchezaji hauwezi kunyanyaswa mahali pako pa kazi miaka yote na ukawa una vumilia wakati una options za kufanya kuwa salama na maslahi yako jamaa ali taka kuvunja mkataba kwa kufuata yale yaliyo andikwa kwenye mkataba. Enheee hizo chuki unazo zi sema wewe zina toka wapi?
 
"Baada ya kuwasumbua sana ndio wakaniongezea Million 20 zingine baaae."
Mazungumzo yalikua nilipwe signing fees million 100 Kwa mkupuo, baada ya kusaini wananiambia kua mkataba unasema nitalipwa Kwa mafungu. Mkataba ni wa Kingereza na mi sikijui".
Ndiyo ujinga wenyewe huo. Sheria haina jutokujuwa, angetafuta wanasheria kabla hajasaini mkataba.

Huyo masikini ya Mungu alikuwa haijuwi dunia na hajapata washauri wazuri, ni wakuhurumiwa tu.

Salama yake huyo kijana amuombe GSM tu kama ataweza, maana nasikia siku hizi kumuona GSM ni vigumu kuliko hata kumuona Rais wa nchi.

CAS huko hawahukumu kihuruma, hana kesi huyo.

Yanga waliwekeza kwa matumaini wavune faida, alikuwa hafahamu kama mpira ni biashara?

Huwezi kuwarudishia million 100 ya kusaini useme ndiyo umemalizana nao. Hapo ilitakiwa awalipe gharama zao zote na faida juu, kwa uchache nahisi kama 1b.

Ushirikina uliopo kwenye mpira anafikiri kuna huruna huko? Maawe.

Awaambie viongozi wa timu anayotaka kuhamia wa "negotiate" na viongozi wa Yanga. Simpo.
 
Back
Top Bottom