Feisala Salum Shtuka Mapema Mdogo wangu!

Feisala Salum Shtuka Mapema Mdogo wangu!

Yanga SC wameshika mpini hivi sasa.

Dogo mkataba wake unaisha May 2024.


Mtoto wa Bakhresa anaona kama mbali sana.


Pesa yote ya usajili msimu ujao inaishia kwa Mawakili na Wanasheria. Wanampiga pesa za kutosha hivi sasa. Mpaka akija kuamka atagundua kumekucha.

Yanga leaders want to set a good example right here!
Kwenye kesi feisal halipi chochote pale kuna watu wanalipa na kumsimamia mpaka sakata linaisha mshahara wa million nne unaweza ukapata hela za kumlipa jasmine abdulrazak kweli hapo wanamsaidia tu.
 
Kutokuwepo kambini miezi 3 ni sababu tosha ya kumfukuza mchezaji, ila kwa Fei hali imekuwa tofauti sababu anahitajika.

Sheria hii imeandikwa wappi?

Hebu weka picha ya ushahidi hapa...wanajanvi wajifunze.[emoji23]
 
Acha uongo anatakiwa alipe mshahara wake mpaka mkataba unaisha hela yenyewe million nne hyo pesa ndogo kwa AZAM safari hii mmeyakanyaga.
Kama anatakiwa alipe iyo milioni 4 kuvunja mkataba si aende sasa afanye ivyo asepe, mbona anawakwepa yanga shida yake nini?
 
Hiyo miezi 3 kulikuwa na kesi zinaendelea hivo sio rahisi kufanyakazi kwasasa.
Wanasema miezi 3 kutokuwa kazini inatosha kumfanya afukuzwe.

Inafaa adhabu ya faini. PSG hawawezi kumfukuza Mbappe eti kwa sababbu hajahudhuria ofisini siku 3.
 
Simba waliihandle vzr sana ile ishu na haikuwa na mjadala. Huenda sababu hawakumhitaji sana. Imagine Simba ingekimbilia TFF kama Yanga.
Ilikuwa ni Simba Vs Dejan.

Ingekuwa Simba Vs Chama ingekuwa issue nyingine.[emoji23]
 
Kosa la viongozi ni moja tu, kuruhusu mkataba wa mchezaji aina ya fei kuwa na udhaifu na thamani ndogo.

Kama kweli mkataba una udhaifu basi tulitegemea Azam FC wamtangaze dirisha lile dogo.

Kwanini hawakumtangaza ikiwa mkataba unasema Fei akilipa Milion 100 tu anaruhusiwa kuondoka?

Azam FC sio wajinga.

Mara 2 mfululizo TFF wametoa hukumu ya kuwa mkaataba wa mchezaji na klabu yake ni halali. Tunapata vipi uhalali wa kubishana na TFF na kusema mkataba una mapungufu?
 
Njia ipi? Kwa kawaida usipoonekana eneo la kazi yako kwa miezi 3 si unafukuzwa tu? Ila huyu imekuwa tofauti sababu anahitajika.
Sheria ipi ya TFF au ya CLUB imedema hivyo?

Au unatumiaa sheria za TAMISEMI?[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kama anatakiwa alipe iyo milioni 4 kuvunja mkataba si aende sasa afanye ivyo asepe, mbona anawakwepa yanga shida yake nini?
Jiongeze mbona unadandia treni kwa mbele million times remaining contract period hivi shule ulikuwa unaingia kweli kipindi cha hesabu
 
Ficha ujinga wako kama ujui kitu funga kabati lako, uyo sure boy yanga walifata utaratibu wa kutaka kumsajili kwa kuwaandikia azam officialy but azam walikataa katakata kumuachia ikabidi Sure boy asubili mkataba wake uliokuwa umebakiza miezi 6 uishe ili aondoke bure na ndicho kilichotokea, yanga aikufanya uhuni kama huu aliotaka kufanya fei toto
Kwa ramadhani kessi na buswita mlifuata utaratibu upi.
 
Hivi kwanza hujashtuka tu mara zote hizo kukimbiwa na wanasheria wako?

Ulianza na wale wa Bernard Morrison.

Ukaja na Shangazi Mwanasheria Mwanasiasa.

Na sasa Umefika kwa Mwanasheria wa msuva.

Shtuka mdogo wangu, hao wote wanatambua kuwa hutoboi dhidi ya Yanga SC na ndio maana mwanasheria wako wa sasa hivi amekushauri ukavunje mkataba baada ya kusoma tu shauri lako na klabu yako. Ulikosea sana kufuata ushauri wa watu wasio fahamu mpira. Ona sasa hata hao nao wamekukimbia, wamebaki kukuungumza tu mitandaoni.

Kila mwenye akili anafamahu kabisa hauna msimamo bali una kiburi, hata viongozi wa klabu yako wanafahamu hilo. Ndio maana wanataka watoe fundisho kupitia wewe. Sio kwamba wana uhitaji na wewe sana bali hapana. Na viongozi wako pia wanafahamu kuwa wewe si wa kurudi pale hata wakamsajili Mudathir.

Kimsingi mwanasheria wako ndiye aliyekushauri ukaulizie gharama ya kuvunja mkataba na Yanga, na kwasababu ya jeuri yako ukaamua mupeleke maombi hayo kupitia TFF. Mdogo wangu viongozi wako wamepanga wavune Milioni 500 kutokana na kuvunja mkataba wako na wao. Wanafahamu wazi kuwa Azam FC ndio mabosi wako watarajiwa, wanafahamu kuwa boss wako atakusaidia tu.

Hata kama ikishindana wanakuvizia miezi 3 kabla ya mkataba wako na wao kutamatima, ili wakakufungulie kesi ya madai ya kwanini walikuwa wakikulipa mshahara na kazini hukuwa unaripoti. Wamepanga kuwa hawakuachi uondoke free (bure) hata kama ukiamua kukaa gheto ungoje tamati ya mkataba wako.

Kuna hati hati pia hata dirisha lijalo la usajili usisajiliwe na timu yeyote kwa kuwa bado utakuwa kwenye kesi ya madai na klabu yako.

Mdogo wangu hakuna mchezaji anayeweza kuvunja mkataba na klabu yake pasi na klabu kunufaika. Inawezekana tu kama ungekuwa Juma Makapu, Telela au crispin ngushi.

Waambie tu hao matajiri wa juisi wapeleke pesa tu pale avic town ili ucheze mpira msimu ujao.
Wachezaji wetu tatizo elimu. Kwa akili ya kawaida tu mkataba umebaki mfupi Kuna ugumu gani wa kuvumilia uishe aondoke bure hasa ukizingatia umri bado. Kiburi kisichokuwa na maana.
 
kwa wanasheria wenu wale vilaza pale yanga mapema tu mnapigwa knockouts

Ukitumia akili kidogo utagundua kuwa Feisal na Wanasheria wake wote wamepigwa Knockouts za kutosha.


Ona sasa wamekuja wakipiga magoti kuomba wavunjiwe mkataba.

Mwanasheria wa kwanza kamkimbia.


Mwanasheria wa pili kamkimbia.


Huyi wa tatu atamkimbia nayeye...
 
Jiongeze mbona unadandia treni kwa mbele million times remaining contract period hivi shule ulikuwa unaingia kweli kipindi cha hesabu
Wanaojua thamani ya mkataba wa mchezaji ni yanga wenyewe, izo blah blah unazoandika hapo mnazijua wenyewe madunduka, Thamani ya mkataba wake ataijua siku akienda kutajiwa dau la kuvunja mkataba full stop
 
Kama kweli mkataba una udhaifu basi tulitegemea Azam FC wamtangaze dirisha lile dogo.

Kwanini hawakumtangaza ikiwa mkataba unasema Fei akilipa Milion 100 tu anaruhusiwa kuondoka?

Azam FC sio wajinga.

Mara 2 mfululizo TFF wametoa hukumu ya kuwa mkaataba wa mchezaji na klabu yake ni halali. Tunapata vipi uhalali wa kubishana na TFF na kusema mkataba una mapungufu?
Azam kwann unawaingiza hapa? Kwani wao ndo wamesema wanahusika na muamala?
 
Hujajibu swali la kwanza. Kwann Yanga baada ya aliyoyafanya Fei wapo tayari kuboresha maslahi yake sasa? Unadhani hawaoni tatizo limeanzia kwenye mkataba usio fanana na thamani ya mchezaji?

Hayo ya kukaa mezani na Yanga ndicho anachofanya sasa hivi kupitia TFF, Amepeleka barua ya kuomba kuvunja mkataba. Iwapo TFF itaruhusu, Yanga itakuwa kwenye mtego wa kusema alete kiasi gani na kwanini na hapo ndipo udhaifu ulipo. TFF isipo ruhusu itahalalisha sasa mchezaji kuwa na sababu ya kulalamika iwapo vipengele vya kuvunja mkataba vipo. Mwanzoni tatizo lilikuwa ni utaratibu, hajapeleka maombi, hajakaa na viongozi. Sasa kayapeleka.

Mkataba umebaki muda mfupi uishe ila Yanga imechelewa kumpa mkataba mpya mpaka hao wanaomrubuni wakamfata na kumpa ofa yao na Fei kuikubali.

Haya, ngoja tusubiri Yanga watasemaje kuhusu ombi la mchezaji la kuvunja mkataba maana mpaka sasa walichofanya ni kumwandikia barua wakimtaka arudi kambini.
Yanga wanamtega pia Fei, asiwe na hoja hata CAS, ataenda kusema nini? anavunja mkataba kwa shida gani?
 
kwa hiyo ukiwa mchezaji unapotea tu miezi mitatu ufukuzwe ili uhamie timu ingine ,we kashabikie vitu vingine mpira huulewi!
Akipotea miezi 3 unafanyaje? 6 je?
 
Acha uongo anatakiwa alipe mshahara wake mpaka mkataba unaisha hela yenyewe million nne hyo pesa ndogo kwa AZAM safari hii mmeyakanyaga.
Mkuu unaelewa maswala ya mikataba? Hatukatai anaweza kulipa ila Unataka kuhama nyumba unayoishi si uongee na mwenye nyumba Sasa unaenda kushtaki kwa mwenyekiti inakaaje hiyo , kuweni waungwana asaidike afanikiwe acheni chuki na club

Hata kama anaweza kulipa Kuna taratibu za kulipa mkuu
 
Back
Top Bottom