Feminism imewaongezea Wanawake mzigo mzito zaidi kuliko walivyotarajia

Kwa hili la feminist nakupinga na hapo nawatetea wanawake na mabinti, siyo kwamba feminist ndo imesabibisha wanawake kubeba laana mbili zote za kuzaa kwa uchungu na kula kwa jasho ila kilichosabisha haya yote ni malezi na maandalizi ya kuwaandaa watoto kuwa mama Bora na watoto wa kiume kuwa baba Bora, Sasa wote wa kiume na wakike kizazi hiki wameambulia kupata makoroma, kwani mwanaume gani atapenda kuishi Malaya? Mke asiyejiheshimu, koroma au jamvi la wageni? Kama hakuna basi inaumiza kuwa na jamii inayotia kichefuchefu, Sasa basi lawama zinarudi kwa baba kwa kushindwa majukumu yake ya kulea familia Bora, kuoa mke mwema wa kulea watoto wake maana vijana wote wakike na kiume hawapaswi kukosa maadili mpaka tushabikie mapenzi njenje kama wanyama yaani kutongozana hovyohovyo kama wanyama hiyo kwa binadamu inaondoa thamani yetu hata zamani watu wa hivyo walionekana mafataki na wanawake walionekana Malaya na kutengwa na jamii maana umalaya ni uchafu na dhambi kubwa kwa Mungu.

Sasa basi wewe Taikon kama baba hebu acha kuwaponda wanawake kama ulivyosema wengine ni dada zako au watoto wako, hebu Anza kufundisha ubaba Bora uliobeba jukumu la kulinda watoto au kizazi alicholeta dunia ahakikishe kiwe Bora na kama siyo Bora yaani familia yoyote itakayotoa watoto Malaya na vijana barubaru basi itengwe, kikubwa nikuomba serikali itunge Sheria za malezi Bora Kila baba Kila mwaka aonyeshe jamii watoto wake wapo katika viwango gani vya malezi Bora kama serikali inavyoonyesha imefanya nini basi na wababa iwe hivyo hivyo, waonyeshe jinsi walivyothaminisha watoto wao, kielimu, malezi Bora na hata uchumi wa familia yake, mbona zamani walifanya hivyo kwa kutoa hesabu na kama familia ilitoa Malaya basi ilijulikana ni familia ya nani, imagine baba huna malazi ya kulelea watoto na watoto wakikua kidogo hasa wa kike wanaruhusiwa kutoka nyumbani kwenda kujiunga na umalaya Ili waje wamtunze baba na kizazi chake na bado tunaona sawa tu na vijana wa kiume hivyo hivyo mpaka wengine wanajifunza tabia mbaya kwa kukosa malezi na bado tunaona sawa tu, hatutaki kumuwajibisha baba arudi kwenye mstari alee kizazi Bora akipe mahitaji yake na kama hawezi basi ahasiwe maana huwezi kuwa baba unaleta jamii inatia kichefuchefu maana yake uzao wako ni mchafu, tena maandiko yamemsisitiza baba kwamba asipoweza kutunza familia huyo amemkana Mungu tayari tena achukuliwe kama mchawi yaani yeye ndo mchawi wa jamii na mchawi adhabu yake ni kifo.

Sasa basi hao wanawake Malaya tukiwarudisha kwa baba zao na mizigo yao ya watoto baba zao wawalele kwa kushindwa kuleta kizazi chenye maadili huo upuuzi utaondokwa kwenye jamii na Yale majimama mashankupe yaliyozaa watoto bila familia au mpango maalumu nayo yataona aibu baada ya kuthaminisha Hawa mabinti wadogo kwa kuwarudisha kwa baba zao, lawama zitabaki kwa mwanaume kwasababu ndiye aliyepewa majukumu ya ulinzi wa kizazi chake, kuinua uchumi wa kizazi chake na mengine mengi ya uongozi na usimamizi wa familia, tena basi haikuishia hapo bado akaonywa juu ya kulinda moyo wake usitekwe na mwanamke Malaya na mbinu za mwanamke Malaya zipo kwenye maandiko na bado akaonyeshwa madhara ya kuwa na mwanamke Malaya Sasa wababa tumekwama wapi? Mpaka tunatengeneza jamii ovu kiasi hiki, baba huna hata Binti mwema wa kujisifia bado unatamba kwamba ungekuwa wewe ni Adamu basi Hawa asingekutapeli!!!, Mbona bado tulichopewa na Mungu tumeshindwa mapema sana yaani uongozi umetishindwa tumekubali wanawake wabebe majukumu yetu kwa kulea vizazi vyetu bila uchumi kitu kinachofanya wawalee kwa umalaya na baba upo tu ukiangalia jinsi unavyotengwa na Mungu kwa kufanya kizazi chako kiwe chukizo kwa Mungu hasahasa wewe Taikon sijui watoto wako wapo upande upi? Maana unachekelea tu wanawake kuwa Malaya na kusingizia feminist hiyo feminist maana yake ni usawa wa kijinsia yaaani ukiweza kusomesha Binti zako na vijana wako wa kiume na ukawapa uchumi mzuri basi wakijaliwa kupata waume hao wake waweze kujihudumia kwenye mambo yao ya msingi na isiwe kama zamani watoto wa kike walipata shida kusubiri huduma za msingi na kusababisha kunyanyisika sana na hiyo yote ilisababisha bado na kujisahau kwa baba kwamba hayo ni majukumu yake na siyo adhabu kwake, na bado mabinti wazuri na wema wapo na wanaume wanaojielewa wanajisifu kupata kitu chema na wanalinda kwelikweli.
 

Kama Mwanamke hataki kumheshimu mume wake unategemea Mume atafanya wajibu wake?

Nakupa mfano,
Kwa upande wa Kidini, Mungu ni Kama Baba, binadamu ni Kama Mke/Mwanamke.

Unategemea Mungu afanye majukumu yake Kwa binadamu asiye na utii aliyeamua kumuasi?

Familia inajengwa Kwa kanuni mbili;
1. MWANAUME ampende Mkewe
2. Mwanamke amheshimu na kumtii Mumewe.

Siku hizi wanawake wanataka tuwapende na hapohapo tuwatii. Huo upuuzi uliona wapi?

Yaani Sisi tuwasikilize wao, wao wenyewe wanaita Masikilizano😂😂
 
Siyo kweli.........Wanawake ndiyo wanapata taabu kwenye suala la mahusiano...amini nakumabia....kama huamini nenda kwa waganga, manabii uone wateja wengi ni wa fungu gani
 
Sina la kuongezea ila hii ni kuntu kabisa,
Ubarikiwe kwa andiko zuri lenye fasihi na falsafa ndani yake.
 
Ili usinielewe itakupasa uwe na akili ndogo Sana, au uwe na akili za kike zilizoumizwa.

Wengi hunielewa mwishoni, ninachofanya hapa ni kwaajili ya Vijana wadogo ambao wengi hamkupelekwa jando, na hamna akili za Kiume
Dogo ulikosa malezi ya mama ndio maana una kisasi na wanawake. Mara nyingi unaleta ujuaji na upumbavu mwingi na kutumia neno la Mungu vibaya.
 
Binadamu pale anapoenda kinyume na asili ndo matatizo mengi yanakuja mfano kukata miti ovyo ili kupata makzi ndo matatizo ya tabia nchi na majanga kibao ynakuja.

Tuje sasa sasa!! Haiwezekani hata siku moja mwanamke we juu ya mwanaume no matter how ata awe na degree mia 700 kwa asili anaweza kuolewa na Tena kumtii hata mpiga debe kama akimuoa ..
Sasa ivi usanii na mambo ya mitandaoni ni mengi sana watu kuleta ujuaji usisema elimu bongo hamna elimu zaidi ya kujua mambo ya kizungu na kingereza....Hakuna mwanaume bwege anaweza pelekeshwa na mwanamke kwa namna yeyote ile mara nyingi ni Bora kutulia tu na kuepusha Shari kama unaelewa tafuta yule mawazo yako yanalenga kwa kufanya assessment kabla ya kuingia kweny mahusiano na ndoa kwa ujumla.

Nina hakika kama sijakosea kiburi cha mwanamke kinaanza pale atakapozaa hata ubinafis na roho mbaya zinaanza hapo akijumlisha kipato ,Mara nyingi naona status hapa wale waliozaa washawatoa mapenzini wanaume wao wamebaki kujifanya wanawekeza kwa watoto hapa naongelea weny kipato Mara akipost mto "We ndo kila kitu kwang" means hapo kamaliza hana time na mume na anajua anaweza kujitegemea ila umri sio rafiki unashangaa puuuh!! Miaka 41 sura inaanza kupoteza Nuru tumbo nalo limekushuka kama kunyonga ile miruzi unapigiwa na wanaume ukipita barabara inapungua na kuisha kabisa hauna mvuto Tena ...kumbuka katika umri huu wanaume wengi wanakuwa wametulia na wanakuwa kweny moto wanaweza hata kupata mtoto kwa miaka 40 hata 45 fresh kwa mwanaume ila mwanamke game lishamtupa mkono sehemu za Siri hazina mvuto kitambi tayar alama za stretch mark kibao kile kiburi hauna Tena labda utafute viben 10 ..
Hela Haina thamani Tena utajua hujui.
 
Nakuelewa. Ila umesahau kuweka maana ya feminism

Ufemnist Kwa wengi ni ule mtazamo wa mwanamke awe Sawa na Mwanaume tena ikiwezekana zaidi yake. Sio ajabu ukisikia watu wakisema Nani Kama Mama.
Ufemnist upo wa Aina mbili kulingana na Visakale vya Kidini.
1. Ufeminist wa Lilith
2. Ufeminist wa Eva/Hawa.

1. Ufeminist wa Lilith
Ni ule wa moja Kwa moja(wa dhahiri) wa mwanamke kukataa kutawaliwa na Mwanamke kabisa.

2. Ufeminist wa Eve/Hawa.
Ni ule ambao upo Kwa kificho, indirect way.
Yaani mwanamke anaratibu mambo yake kisiri huko ili ampindue mwanaume alafu ikishindikana ndio anakuletea matatizo yake.
Mfano, Mwanamke anaweza kuingia kwenye mchezo Fulani wa vikoba Kwa Siri au akawa anafanya biashara Kwa Siri bila kukushirkisha alafu yakimshinda ndio anakuletea matatizo Kwa namna ya kujiliza Liza.

Hawa/ Eva wakati anakula mchongo wa kufanana na Mungu akiwa na Nyoka ilikuwa ni Siri. Alitaka kumzidi mpaka Adamu mumewe, alivyokula tunda akaona hakuna matokeo mazuri ndio akaona ule sasa ni msala.
Akarudi Kwa mumewe na kumbembeleza wale Yale matunda waliokatazwa wasiyale,
Wakati anamuambia hivyo Adamu kumbuka hakumuambia kilichotokea kuwa amedanganywa na nyoka huko bustanini.

Adamu Kwa upendo akaamua kusikiliza sauti ya mkewe. Yaani Akauza mamlaka yake kisa upendo alionao Kwa mkewe.
Bila kujua mkewe alikuwa anataka kumpindua.

Ufeminist agenda yake ya nje ni kupigania haki za wanawake Jambo ambalo ni sahihi Kabisa.
Lakini agenda ya ndani ndio mbaya zaidi ambayo ni kumpoka Mwanaume Mamlaka yake.

Na Hilo kamwe halitowezekana,
Kwa sababu Dunia hii inaongozwa na Wanaume, na falme za kiroho zinaongozwa Kwa character ya kiume.
Lusifa pamoja na Mungu Wana Character ya Kiume.

Hivyo Lusifa anatumia ufeminist kama alivyoutumia zamani kuzidi kuutawala ulimwengu.

Kwa kifupi ni kuwa Mwanamke anatumika kama toilet paper kutimiza majukumu ya Mfumo dume WA kishetani na kuuacha mfumo dume wa kiungu
 
Dogo ulikosa malezi ya mama ndio maana una kisasi na wanawake. Mara nyingi unaleta ujuaji na upumbavu mwingi na kutumia neno la Mungu vibaya.

Kwa bahati nzuri nimelelewa na Mama, lakini hainifanyi ni mtetee hata Yeye endapo akikengeuka na kujiingiza katika mambo ya kishetani.

Ungeleta hoja kuliko kuonyesha kuwa huna akili ya kujadili mambo madogo Kama haya.
 

Chain of command baadaye ndio inawaathiri. Kwa maana Wale watoto aliokuwa anawategemea ndio haohao watamdharau
 
Sasa hapo mwenye kosa bado ni mwanaume, hivi unaoaje gubegube lisilokuheshimu? Au na wewe ni gubegube? Hayo maandiko yamesema uoe mke mwema Sasa unakuta mwanaume anaoa gubegube kwa tamaa zake mwenyewe, na kingine unasema Mungu usipomuheshimu anakaa mbali na wewe lakini husemi Kwanza Mungu alitunga Sheria zake na kutoa uhuru kama huzifati basi anakuacha uende zako, Sasa kwanini mwanaume anaoa bila kuwa na Sheria zake na azinadi kabla ya kuoa huyo mke mwema Ili afanye uchaguzi mwema maana ukitoa hizo Sheria atakaye kubali kuzifata ndo oa na masomo ya uchumba yapo kabla hujaoa tafuta mtu wa Imani yako atoe SoMo la mke mwema na mume mwema kama ukiona huyo mke hafai au hata kuheshimu vunja uchumba tafuta hata nchi za mbali mpaka utakapopata wa kufanana na wewe, ila mtu anaona gubegube kwa pupa zake bila Sheria yoyote Wala kujua wataendana alafu yakimushindwa anaanza kulalamika Sasa si apambane na Hali yake ya kukurupuka, wanaume warudi kwenye mstari na jambo la kuoa lisiwe la pupa lizingatie vigezo ikiwemo hilo la kuheshimiwa lakini napo huko kuheshiwa kuwe kwenye Sheria ulizoweka kabla ya kuoa na ulimjulisha huyo mke mapema kama muda wa kurudi nyumbani na ratiba zingine siyo mke akuheshimu kama anavyomuheshimu baba yake yaani akuogope hata kukusogelea hapo ndo tunavuka mipaka, mke siyo mtoto wa mume ni mpenzi wa mume wataheshimiana kwa kulinda Sheria za mume na siyo kuogopana na hata hapo unaposema wanataka tukisikilizane hapo mbona sawa tu Kwa mtu na mpenzi wake? Au tuwafundishe jando hamjaenda? Mke na mume wanapaswa kuelewana na kuzungumza hata Mungu Anaita watu waende wakatoe hoja zao kwake azisikilize na ndo umesema ni mfano wa mume hivyo mke na mume wanapaswa kukaa pamoja na kuambiana makwazo yao na matamanio yao na ndo maana Kuna sehemu za utulivu za kwenda kusemezana huko na kukumbushia Sheria kama zinafatwa au zimesahaulika ila tu usioe gubegube Bali oa mke mwema na ukae sehemu yako kama mlezi wa nyumba na mke mweleze ukweli yeye ni msaidizi wako yaani anachukua madaraka unapokuwa haupo hivyo ni wajibu wa mume kufumfundisha mke wake ninini anataka afanye akiwa hayupo na nini ajifunze kwa mume tu na ndo maana unatakiwa kuwa baba mwenye maadili hizi kelele za kutokuheshimiana ukichunguza utakuta hukufanya uchaguzi sahihi na ulioa gubegube linalopaswa kuzurula mitaani likifanya ushankupe wake na hakuna mwaume anajielewa ataoa hilo gubegube.
 
Siyo kweli.........Wanawake ndiyo wanapata taabu kwenye suala la mahusiano...amini nakumabia....kama huamini nenda kwa waganga, manabii uone wateja wengi ni wa fungu gani
Wengi hao wanawake siyo tabu Bali nikuteka mioyo ya hao waume wasiojiombea na kusimama kwa Mungu.
 
Wanawake wanakutesa sana kijana
Kama umesoma katikati ya mistari main post na reply za mleta mada utakuta kuna maneno kama feminist wa kiume,marioo kiben ten etc

Sasa wewe ndiye FEMINIST WA KIUME aliowataja.

Mkuu ROBERT HERIEL nakusoma na nakuelewa sana hao waliopigwa kishoka na kaka zao goi goi ipo siku watakuja humu kuzitafuta post zako na watakuwa wameshachelewa sana.
 

Rejea post yangu ya juzi

Hii hapa👉👉 Mwanamke ukiishi naye bila ndoa anakuheshimu zaidi kuliko ukifunga naye ndoa, kwa sisi Wakristo

Wanawake baadhi Yao hukupa rangi unayoitaka ili umuoe ukishamuoa ndio wanakuonyesha rangi yao halisi
 


Hawa hawataturudisha nyuma Kuwafunza Vijana wanaohitaji Mafunzo kufundishwa.
 
Haaaa Sasa hivi si vichambo jamani, uzee si DNA tu za mtu zilivyo Kuna mwingine amezaa bado anaoneka yupo vizuri, pia jamani mapenzi kitu kinaitwa mapenzi naomba tukitofautishe na kushindwana na magubegube yenu, na ndoa ijulikane ilikuja kwa lengo gani na siyo wote wanapaswa kuoa au kuolewa tulijue hilo, ndoa kama ndoa ilikuja Ili mume aoe na apate msaidizi Ili asiwe mpweke akirudi nyumbani apate wa kusemezana naye na watunzane mpaka uzeeni hata kama hawana watoto cha Kwanza iliangaliwa mke kama rafiki wa kuaminiwa na mume wake, haya ya kuanza kudhalilishana sijui atazeeka atachoka na mashavu kushuka hayapo kwenye ndoa, maana rafiki yako aliyekuvumilia na kujua Siri zako kwa miaka mingi ndiyo rafiki unayeweza kumuamini kuliko rafiki mpya anayeweza kukuchukia au kutokuvumilia kwa udhaifu mdogo tu, hebu tuipe ndoa heshima yake isiusishwe na mabadiliko ya mwili maana wote wanabadilika tena wanaume wanavyokuwa ukuni unalegea hata kama anazalisha bado hawezi kuwa kama kijana Sasa kwanini tusilindiane heshima ya miili yetu na ndoa ibaki kwa mke na mume kuishi kwa kuelewana yaaani mtu utakaye muamini kutunza Siri zako na rafiki yako kwenye shida awe na wewe, na wanaume hebu tuoe kulingana na mpango wa Mungu Ili tusipate haya maumivu, Adam alipewa Kila kitu ndo akaja kupewa Hawa Sasa kwanini huna kitu ukachukue huyo boss au CEO wa kazi gani? Kwanini ushushe heshima yako hivyo Mimi nasema bila kupepesa macho oa size yako mke afate Sheria zako ndo kukuheshimu huko na siyo kuoa CEO eti akikuona anakuogopa kama swala kamuona Simba hapo nikudanganywa kweupe au kujidanyana, heshima ya mume ni Sheria za nyumba yake na huwezi kuweka Sheria na zikafatwa na mtu anayekuchukulia duni kwake yaaani anakuhandle mbele ya safari itakuwa vikwazo na haya madhalilisho ya uzee wakati ni mfumo wa viumbe hai wote kukua na kuzeeka hakuna kuchekana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…