Kwa hili la feminist nakupinga na hapo nawatetea wanawake na mabinti, siyo kwamba feminist ndo imesabibisha wanawake kubeba laana mbili zote za kuzaa kwa uchungu na kula kwa jasho ila kilichosabisha haya yote ni malezi na maandalizi ya kuwaandaa watoto kuwa mama Bora na watoto wa kiume kuwa baba Bora, Sasa wote wa kiume na wakike kizazi hiki wameambulia kupata makoroma, kwani mwanaume gani atapenda kuishi Malaya? Mke asiyejiheshimu, koroma au jamvi la wageni? Kama hakuna basi inaumiza kuwa na jamii inayotia kichefuchefu, Sasa basi lawama zinarudi kwa baba kwa kushindwa majukumu yake ya kulea familia Bora, kuoa mke mwema wa kulea watoto wake maana vijana wote wakike na kiume hawapaswi kukosa maadili mpaka tushabikie mapenzi njenje kama wanyama yaani kutongozana hovyohovyo kama wanyama hiyo kwa binadamu inaondoa thamani yetu hata zamani watu wa hivyo walionekana mafataki na wanawake walionekana Malaya na kutengwa na jamii maana umalaya ni uchafu na dhambi kubwa kwa Mungu.Anaandika, Robert Heriel
Angalizo; lugha itakayotumika inaweza isiwe nzuri. Hivyo Kama ni mwepesi WA mihemko basi unashauriwa kuishia hapahapa. Endapo utaendelea kusoma, na ukapata madhara yoyote ya kihisia au kisaikolojia basi sitakuwa sehemu ya lawama.
Nafahamu ili familia ianguke basi Mama ndiye atakuwa wa Kwanza kuiangusha familia, najua jamii na taifa ili iaungike basi wanawake watakuwa wakwanza kuwa chanzo cha anguko Hilo.
Dini na vitabu vya dini kubwa vinaeleza namna Mwanamke alivyokuwa chanzo kikuu cha anguko la Dunia.
Mtu ni masikini alafu unaiga ufeminist Kama sio kutaka kujiingiza kwenye umalaya ni kitu gani. Kama sio kutaka kuzaazaa hovyo na wanaume wengi pasipo adabu ya kike ni nini.
Kuangalia filamu za Hollywood ndio udhani uyaonayo ni kweli?
Kupata hako kadegree Kako kamoja ndio ufikiri usomi ndio kutaka mambo ya kipuuzi?
Kwa mujibu Biblia, Feminist wa Kwanza kabisa alikuwa Eva/Hawa ambaye alitamani kufanana na MUNGU, yaani alitaka kumpiku mpaka Adamu mumewe. Shetani alitumia tamaa ya Hawa ya kutaka kumpindua Adamu tena ikiwezekana kufanana na Mungu, na ndipo Shetani anamuambia Hawa/Eva.
Mwanzo 3:4
Nyoka akamwambia mwanamke, Hakika hamtakufa,
Mwanzo 3:5
kwa maana Mungu anajua ya kwamba siku mtakayokula matunda ya mti huo, mtafumbuliwa macho, nanyi mtakuwa kama Mungu, mkijua mema na mabaya.
Shetani kamwe hawezi kukujaribu Kwa kitu ambacho sio tamaa yako. Hata Biblia inasema; Mtu hujaribiwa Kwa tamaa yake MWENYEWE.
Hata hivyo, Shida au changamoto Fulani inayokusibu huweza kutumiwa na Shetani kukujaribu.
Hawa/ Eva alikuwa amezidiwa Kwa mambo mengi na Adamu. Kumbuka Adamu ni mfano wa MUNGU, wakati Eva ni mfano wa Adamu.
Ufeminist wa Eva Kwa kutaka kumzidi Adamu tena ikiwezekana afanane na Mungu unageuka kuwa mzigo tofauti na vile alivyotarajia.
Kwanza haitokuja kuwezekana Mwanamke akawa Sawa na Mwanaume dunia ingalipo.
Hata huyo Lusifa aliyekuwa anamdanganya Eva ni ana-character ya kiume, huyo Mungu Mkuu ana-character ya kiume. Hivyo ni kusema vyovyote mwanamke atakavyochagua iwe upande wa Shetani au Mungu bado atajikuta anaongozwa na mfumo Dume.
Madhara ya ufeminist ndio yalifanya Adamu akafukuzwa pale Bustani ya Edeni.
Moja ya Madai ya ufeminizimu(feminism) ni mwanamke KUSIKILIZWA. Wakati kiroho hakuna kitu Kama hicho.
Mwanaume ndiye anasikilizwa anataka nini? Na sio mwanamke.
Kumsikiliza mwanamke ni kutaka maanguko tuu. Kwanza mwanamke akili yake haioni mbali, yeye anachotaka ni kutatua tatizo lililopo mbele yake tu.
Wanawake ni vipofu ambao kiongozi wao ni mwanaume.
Mungu anamshangaa Adamu Kwa kumsikiliza Mkewe, wakati Mungu alimuachia maagizo Adamu kuwa yeye ndiye kiongozi hivyo Oda zote zinatakiwa azitiishe kwenye Ile Bustani akiwepo huyo mwanamke. Yaani mwanamke naye amtii Adamu.
Mwanzo 3:17
Akamwambia Adamu, Kwa kuwa umeisikiliza sauti ya mke wako, ukala matunda ya mti ambao nalikuagiza, nikisema, Usiyale; ardhi imelaaniwa kwa ajili yako; kwa uchungu utakula mazao yake siku zote za maisha yako;
Mwanamke hapaswi kusikilizwa, wengi mtapinga Kwa sababu hamna upeo wa kuona mbele, mnaongozwa na Mapenzi na hisia za kipuuzi mtadhani Taikon ninataka kukandamiza Dada na Mama zangu Jambo ambalo sio Kweli.
Ufeminist umeongezeka maradufu katika Zama hizi.
Wanawake wanataka kusikilizwa,
Wanawake wanataka utawala na mamlaka,
Wanawake wanataka kuongoza familia,
Wanawake wanataka kuvuja Kwa jasho,
Wanawake wanataka kuolewa na wanaume zaidi ya mmoja,
Matokeo ya ufeminist ni mwanamke kuzaa Kwa uchungu, na sio kuzaa tuu Kule Kwa kuzaa watoto, Hasha Bali kupata matatizo yanayotia maumivu mioyo Yao.
Ufeminist umekuwa mzigo Kwa wanawake Kwa sababu
1. Kwa sasa Wanawake kuwapata ni rahisi yaani thamani Yao imeshuka
Yaani Kwa sasa unaweza hangaika kupata mayai ya Kuku WA kienyeji lakini kamwe huwezi hangaika kupata mwanamke WA kulala naye.
Hii inafanya wanawake wasiwe na laziada Kwa wanaume.
Zingatia kitu pekee ambacho mwanamke atamringishia Mwanaume ni Uchi wake tuu! Vingine vyote wanaume wanavyo tena kwa mbali na ubora maradufu.
2. Wanawake siku hizi wanamzigo wa Kulea watoto na familia
Ufeminist umeleta matokeo mabaya Kwa wanawake, kwani Kwa sasa baadhi Yao ndio wanahangaika wenyewe kutunza familia, jasho linawatoka hasa, wajibu ambao haukuwa wao.
Wanaume wengi Kwa Kupenda bwerere wanapigania Kwa makusudi ufeminist Kwa maslahi Yao hasa ya kibiashara huku wanawake wakimenyeka.
3. Ufeminist unadhalilisha uanamke
Siku hizi ni ngumu kuuona uchi wa Kondoo kuliko kuuona uchi wa Mwanamke. Yaani mwanaume kila ukikatiza unaona uchi ule pale, ukipita mitandaoni ule pale. Ufeminist umekuwa mzigo Kwa Dada zetu. Wanadhalilika hasa.
Ukipiga marufuku na kutoa adhabu Kwa wakala uchi, feminist watajitokeza kuwa unawanyima haki zao. Yaani haki ya mtu kujidhalilisha. Matokeo yake ni wanawake kutokuwa na mvuto Kwa wanaume, umalaya kuongezeka, single mother kuwa wengi n.k.
4. Wanawake kuzaa na Kulea watoto na mababa wengi Kama wanyama wengine.
Huenda isiwe lugha nzuri kwani labda ndugu au watu wangu wa karibu au hata binti zangu wanaweza kujikuta katika Hali hii. Lakini ukweli lazima tuuseme. Ufeminist umeongeza Kasi ya wanawake kuzaa na wanaume wengi. Sio ajabu kukuta Mwanamke kila mtoto anababa yake.
Huo ni mzigo na aibu Kwa mwanamke yeyote anayejua thamani ya mwanamke. Zingatia, thamani ya mwanamke ipo katika kujifunza. Yaani kile ambacho anacho ambacho anaweza kukitumia kama silaha Kwa mwanaume.
5. Mzigo wa kujitongozesha
Ufeminist umepelekea hatua wanawake wanapishana Kwa Masheikhe, waganga, wachungaji na manabii uchwara kisa kutafuta wanaume wa kuwaoa au hata kuishi nao. Kitu cha thamani hakiwezi kuhangaika hivyo, Bali Sisi wanaume ndio tulipaswa kwenda Kwa waganga kisa wanawake.
Kwa zamani mwanamke kamwe hawezi kwenda Kwa mganga ati kutafuta mvuto wa kupendwa na Wanaume. Labda akienda Kwa mganga ni kumuweka mumewe aliyemuoa kiganjani kuwa asione wanawake wengine.
6. Wanawake ku-share mapenzi pamoja na binti zao
Ufeminist umechangia pakubwa Wamama wengi ku-share penzi na binti yake Kwa mwanaume Fulani.
Mfano, Kwa mwanamke anayejitambua na Mwanamke kweli, kamwe hawezi kutoka kimapenzi na kijana aliyemzidi umri zaidi ya mitano au kumi. Achilia mbali mmama kutoka na kijana Mdogo Jambo ambalo mara nyingi husababisha Kijana kutoka na binti, Hali iñayopelekea mtu Kula kuku na mayai.
Mwanaume ndiye anauwezo wa kuoa mwanamke hata kama amemzidi miaka arobaini. Ni Sawa tuu.
7. Wanawake kujikuta katika biashara ya umalaya Jambo ambalo linaathiri thamani Yao
Kadiri biashara ya umalaya inavyoshamiri ndivyo umuhimu wa Ndoa unakosekana.
Kwa sehemu kubwa ndoa Kwa mwanaume ni tendo lenyewe. Mwanaume Kama anauhakika wa kupata tendo la ndoa muda autakao Kwa gharama nafuu hawezi kuona umuhimu wa Ndoa.
Nachelea kusema, Kama wanawake wakiamua Kwa pamoj kuweka mgomo wa miezi mitatu mfululizo wa kutokuwapa wanaume tendo la ndoa Kwa ambao hawajao basi ndoa nyingi zitatangazwa na wengi wataolewa. Hata hivyo kesi za ubakaji zitaripotiwa mahali mahali pia.
Niliwahi kusema mwanamke wakati mwingine kujiingiza katika utafutaji wa kubangaiza na kusaka tonge kunaweza kumuingiza kwenye umalaya.
Nipumzike sasa.
Nitacheza na yeyote kadiri anavyotaka tucheze.
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Sasa basi wewe Taikon kama baba hebu acha kuwaponda wanawake kama ulivyosema wengine ni dada zako au watoto wako, hebu Anza kufundisha ubaba Bora uliobeba jukumu la kulinda watoto au kizazi alicholeta dunia ahakikishe kiwe Bora na kama siyo Bora yaani familia yoyote itakayotoa watoto Malaya na vijana barubaru basi itengwe, kikubwa nikuomba serikali itunge Sheria za malezi Bora Kila baba Kila mwaka aonyeshe jamii watoto wake wapo katika viwango gani vya malezi Bora kama serikali inavyoonyesha imefanya nini basi na wababa iwe hivyo hivyo, waonyeshe jinsi walivyothaminisha watoto wao, kielimu, malezi Bora na hata uchumi wa familia yake, mbona zamani walifanya hivyo kwa kutoa hesabu na kama familia ilitoa Malaya basi ilijulikana ni familia ya nani, imagine baba huna malazi ya kulelea watoto na watoto wakikua kidogo hasa wa kike wanaruhusiwa kutoka nyumbani kwenda kujiunga na umalaya Ili waje wamtunze baba na kizazi chake na bado tunaona sawa tu na vijana wa kiume hivyo hivyo mpaka wengine wanajifunza tabia mbaya kwa kukosa malezi na bado tunaona sawa tu, hatutaki kumuwajibisha baba arudi kwenye mstari alee kizazi Bora akipe mahitaji yake na kama hawezi basi ahasiwe maana huwezi kuwa baba unaleta jamii inatia kichefuchefu maana yake uzao wako ni mchafu, tena maandiko yamemsisitiza baba kwamba asipoweza kutunza familia huyo amemkana Mungu tayari tena achukuliwe kama mchawi yaani yeye ndo mchawi wa jamii na mchawi adhabu yake ni kifo.
Sasa basi hao wanawake Malaya tukiwarudisha kwa baba zao na mizigo yao ya watoto baba zao wawalele kwa kushindwa kuleta kizazi chenye maadili huo upuuzi utaondokwa kwenye jamii na Yale majimama mashankupe yaliyozaa watoto bila familia au mpango maalumu nayo yataona aibu baada ya kuthaminisha Hawa mabinti wadogo kwa kuwarudisha kwa baba zao, lawama zitabaki kwa mwanaume kwasababu ndiye aliyepewa majukumu ya ulinzi wa kizazi chake, kuinua uchumi wa kizazi chake na mengine mengi ya uongozi na usimamizi wa familia, tena basi haikuishia hapo bado akaonywa juu ya kulinda moyo wake usitekwe na mwanamke Malaya na mbinu za mwanamke Malaya zipo kwenye maandiko na bado akaonyeshwa madhara ya kuwa na mwanamke Malaya Sasa wababa tumekwama wapi? Mpaka tunatengeneza jamii ovu kiasi hiki, baba huna hata Binti mwema wa kujisifia bado unatamba kwamba ungekuwa wewe ni Adamu basi Hawa asingekutapeli!!!, Mbona bado tulichopewa na Mungu tumeshindwa mapema sana yaani uongozi umetishindwa tumekubali wanawake wabebe majukumu yetu kwa kulea vizazi vyetu bila uchumi kitu kinachofanya wawalee kwa umalaya na baba upo tu ukiangalia jinsi unavyotengwa na Mungu kwa kufanya kizazi chako kiwe chukizo kwa Mungu hasahasa wewe Taikon sijui watoto wako wapo upande upi? Maana unachekelea tu wanawake kuwa Malaya na kusingizia feminist hiyo feminist maana yake ni usawa wa kijinsia yaaani ukiweza kusomesha Binti zako na vijana wako wa kiume na ukawapa uchumi mzuri basi wakijaliwa kupata waume hao wake waweze kujihudumia kwenye mambo yao ya msingi na isiwe kama zamani watoto wa kike walipata shida kusubiri huduma za msingi na kusababisha kunyanyisika sana na hiyo yote ilisababisha bado na kujisahau kwa baba kwamba hayo ni majukumu yake na siyo adhabu kwake, na bado mabinti wazuri na wema wapo na wanaume wanaojielewa wanajisifu kupata kitu chema na wanalinda kwelikweli.