Kuna nyakati Binadamu wanaishi kwa kutegemea hope. Unalala ukihope utaamka, unasafiri ukihope utafika, Unaoa ukihope utafanya kazi na kuihudumia familia. Kuna nyakati hope inafeli, unalala huamki, unasafiri hufiki, unaoa unashindwa kuihudumia familia.
Kwa kawaida mwanaume anapofeli mwanamke anashika usukani kwa muda huku akili yake akiielekeza kumrudisha mwanaume wake kwenye nafasi yake. Tatizo la siku hizi ni either:
1. wanawake hawafikirii kuwarudisha wanaume zao kwenye nafasi zao wanafikiria kuchukua nafasi zao ili wawapeleke na kuwacontrol watakavyo. Au
2. Kuna wanaume wamekuwa wavivu, watu wa kuhonga michepuko, wakwepa majukumu, akili ndogo, kuwa na ndoto zisizotekelezeka hivyo mwanamke anaona si salama kuweka imani kwa mwanaume wa aina hiyo.