Festo Sanga: Ndani ya Ligi Kuu Bara kuna Wachezaji wanalipwa Laki 2 wengine wanalipwa Milioni 50

Festo Sanga: Ndani ya Ligi Kuu Bara kuna Wachezaji wanalipwa Laki 2 wengine wanalipwa Milioni 50

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876

Mbunge wa Makete, Festo Sanga ameshauri Wizara ya michezo kupitia BMT wapitie na wapendekeze kima cha chini cha mishahara ya wachezaji kwenye Ligi mbalimbali nchini hususani Ligi kuu.

Amesema "Kuna baadhi ya Wachezaji wanapokea laki 4 , laki 3, Million 1 na wengine wanapokea Milioni 10, 20 hadi Milioni 50. Sasa vyema kuweka kima cha chini chenye kuzingatia maslahi ya Wachezaji ili wasinyonywe, lakini angalau kuleta unafuu kwenye majukumu yao. Hii itasaidia kuondoa rushwa na upangaji wa matokeo kwenye michezo".

Ameyasema hayo wakati anachangia Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Mei 4, 2026
 
Unalipwa kwa kiwango chako na jinsi unavyoweza kunegotiate kwenye meza ya makubaliano.
Ulaya huko kuna watu wanalipwa dola 250k kwa wiki na wengine dola 10k kwa wiki timu ni moja..

Salah na mane mshahara ulikuwa tofauti sana, mane alizidiwa hadi na henderson
 
Kobie Mainoo wa Man U alikuwa analipwa Paundi elfu ngapi tu kwa wiki, huku magarasa anayoyaweka benchi yakilipwa Paundi laki kadhaa kwa wiki. Hivi ndivyo dunia ilivyo. Hakuna haki.

Fikiria mimi mwenyewe hapa nikijitathmini, najiona nina sifa ya kuwa kiongozi mkubwa kabisa ndani ya hii nchi! Lakini hapa nilipo ninawafungulia mageti watu wenye elimu ya hapa na pale kupita na ma V8 yao.
 
Kama uwezo wake n wa hapa na pale katika kulisakata kabumbu haki yake kulipwa hvyo

Atafute wakala aka winga mZur kwenye majadiliano ya kimkataba si unamuona samia ELIMU yake ni ya hapa na pale lakn anaye winga aka wakala mkal naye n jakaya kikwete anampambania kwa watanganyika
 
[emoji23][emoji23][emoji23] nimecheka km mwehu hapa. Lol
 
Unalipwa kwa kiwango chako na jinsi unavyoweza kunegotiate kwenye meza ya makubaliano.
Ulaya huko kuna watu wanalipwa dola 250k kwa wiki na wengine dola 10k kwa wiki timu ni moja..

Salah na mane mshahara ulikuwa tofauti sana, mane alizidiwa hadi na henderson
Kawaida mkataba wa kwanza hulipwi pesa nyingi. Hata kina saka walishalipwa paund elfu 30 lakini Sasa?
 
Utakuta timu inalipa mishahara minono💰 wachezaji wake, likini wananunua 💼mechi kwa timu inayolipa mishahara ya laki laki ili kujihami wasifungwe.
Injinia acha huo ujinga🙄🚶‍♂️🚶‍♂️
 
Hao wabunge feki sasa hivi wanalipwa mishahara mikubwa shilingi milioni 25 kwa mwezi na posho za vikao laki tatu kila siku kwa kazi gani ya maana wanayofanya.

Kisha watumishi wanaosota wanalipwa laki tatu tu kwa mwezi, hilo mbona halisemi mnafiki mkubwa huyo.
 
Back
Top Bottom