Fid Q : The King of Plagiarism of all the time

Likud niaje, nyingine hii hapa ukishindwa kujiandaa jiandae kushindwa amekopi ile quote inayosema if you fail to plan you plan to faol
 
We makuzi kweli Wewe.Yani ulirepresent kitaa cha weusi kwa kutumia mawazo ya wazungu..Listen to urself b4 u post ur container of nonsense and call it explanations
 

Huu Uzi ni mkubwa kuliko ufahamu wako asol. am talking about kucopy mashairi ya MTU,kuyatafsiri na kuya present kama utunzi wako.Sizungumzik kuhusu kukarabati wimbo au kufanya sampling
 
Umekosea kumshutuma fid hivyo,watu ambao tumetoa mziki huu kwao bs ndo mabingwa wa plagiarism.

Rejea nyimbo ya dmx,slipping,anaanza na intro anasema "to live is to suffer but to survive is to find meaning in the suffering" msemo huo sio wake bali wa mtu anaitwa Friedrich nietzsche

Huo ni mfano tu lkn ni kawaida ya rappers kufind inspiration kwny vitabu au misemo na sio plagiarism.


 
Umewahi kusikia wapi hiyo quote?
Misemo ni jambo la kawaida ebu leta mfano mwingine wa copy zake kama mbili.
Niki mbishi wimbo wa nyakati za mashaka kuna sehemu anasema Life is like a dice game....
Mstari full ka copy kwenye wimbo wa Nas unaitwa hivyo so na yeye tumuite mkali wa plagiarism??
Ukifuatilia hakuna mtu ambaye ana 100% uandishi kwa kila nyimbo.
Na wasomi uongea kwa reference hivyo fid Q kama anaweza soma vitabu na mawazo aka ya summerize kwenye nyimbo basi ni kwamba ana akili kubwa.
 
Unadhani basi hajui anajua sana watu wanaomsema Fid Q sijui uwa ana copy sijui nini uwa hawana hoja za msingi ni chuki tu.
 
Huu Uzi ni mkubwa kuliko ufahamu wako asol. am talking about kucopy mashairi ya MTU,kuyatafsiri na kuya present kama utunzi wako.Sizungumzik kuhusu kukarabati wimbo au kufanya sampling
Awali ulisema kuwa Fid-Q anakopi 'aidia' kutoka katika misemo (quotes) na sasa unasema anakopi nyimbo za watu wengine. Uone aibu, hujui hata unachosisitiza.

Kadhalika, umetoa mfano mmoja tu wa 'quote' ambayo Fid-Q alikopi na kuweka katika mashairi ya muziki wake, na ninavyofahamu Fid-Q ana nyimbo nyingi sana.

Hebu tuambie, ikiwezekana kwa orodha na mifano hai, kuhusu nyimbo zote za Fid-Q unazodai aliiba 'aidia.'
 
Kwahiyo hiyo nukuu ya mstari mmoja tu ndo imekufanya umuanzishie thread?[emoji56]
 
Makuzi
 
Kwa iyo apo kwenye beat ilitakiwa asemaje sasa ili kum acknowledge uyo jamaa

The script wa USA wana nyimbo moja hivi inaitwa "the energy never dies" hawaja-mu acknowledge mtu yeyote mle ndan

Uandishi wa music ni tofauti na uandishi wa thesis, majarida na vitabu

Kuna baadhi ya misemo ni maarufu tu huwezi kum acknowledge mtu, inawezekana ww ukawa ndo mara ya kwanza kusoma icho kitabu na kukuta huo msemo lakini kumbe kwa jamii ya muandishi ni common term tu isiyohitaji acknowledgment
 
hebu tuwekee hayo mashairi aliyotafsiri,kwenye ngoma yake yoyote ile uijuayo..na isiwe msemo mmoja
He is just a Copy Cat watu wa Hip Hop watanielewa namaanisha nini. Sina haja ya kuweka hapa kila kitu...huu mchezo wa kucopy mistari na concepts za nyimbo za nje hajaanza yeye hata wakongwe wamefanya hiyo kitu..Mfano Balozi Dola kwenye Ngoma yake moja anasema "Ma Mc wanakweenda Wanaruudi" Wengi walikuwepo Lakini mimi Nitabaki" hapa aliiga Mashairi ya wimbo Wa Freddie Fox a.k.a Bumpy Knuckles (Huyu sidhani kama unamfahamu) wimbo unaitwa Mc'z Go Mc'z Come.
 
Hizi ndio tunaita Chuki binafsi huku uswahilini
 
Reactions: Pep
Anafanya makosa .huo ni wizi kama wizi mwingine. Atoe mawazo yake binafsi hayo ya kwenye vitabu awe anayazungumzia wakati wa interview au awe na yeye aandike vitabu then awe ana wa quote humo kwa sababu ni rahisi
Siyo kweli Mkuu.
Hakuna plagiarism ya aina hiyo ktk sanaa hasa kuimba.
 
Reactions: Pep
Sijaona tatizo lolote lile kwa yeye kusoma vitabu na kurahisisha yale anayoyapata humo kwa njia ya mistari, nilishawahi kumsikia kwenye interview moja akisema yeye anapenda sana kusoma vitabu, ningeshauri na wasanii wengine wajisomee vitabu ili waimbe vitu vinavyoeleweka, pia nikukumbushe mdau, kusoma kitabu au vitabu ni jambo moja na ule ufundi wa kuunganisha hayo mawazo katika mtitiriko unaoeleweka na yakaimbika ni jambo jingine, hivyo tusiwabembeze wasanii wanaojisomea kaka, sijajua pia kama ulitaka kila mwisho wa wimbo pawe na references na ziwekweje.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…