Fid Q : The King of Plagiarism of all the time

Fid Q : The King of Plagiarism of all the time

Nakumbuka kuna msemo mmoja alikuwa anaupenda sana mwalimu wangu wa kishwahili naye aliutoa kwenye kitabu nimekisahau s "akupigae ngumi ya jicho nawe mpige ya sikio" nikaja kuukuta kwenye ngoma ya Fid Q ile ya kwanza kabisa...watoto wadogo naonutawaskia fid q....
Tell them bro
 
Hata yeye Mtoa mada amecop hii mada,maana fid hajaanza shutumiwa Leo kuhusu Hilo jambo kwa hyo alete shutuma mpya au ataje amemquot nan
Once again I'm telling you this chief, nothing new in this universe, kazi ya sanaa ni pamoja na kutafsiri maneno magumu kwa lugha rahisi ili yaeleweke kwa wanaotaka kuelewa.

Fid Q anafanya vizuri kwenye game ndo maana yupo kitambo, hii ni kutokana na kusoma machapisho na kupata maarifa zaidi. Wangapi walikuepo na pengine walivuma pamoja na akina Fid Q toka enzi hizo ya zaidi ya 15 good years na huwasikii tena? Mfano Lucky Dube once said in one his song; “Not every BLACK MAN IS MY BROTHER and not every WHITE MAN IS AN ENEMY ” si kila mmoja wetu ataelewa haya, na haya maneno yalikuepo toka enzi na enzi, sasa Fid Q akitaka kuyatumia na kusema hivi; “Si kila mtu mweusi/muafrika ni ndugu yangu na Si kila mtu mweupe/mzungu ni adui” ungependa am-acknowledge nani hapo?
 
Huo msemo mbona upo kitambo hata kabla fid ajautoa, ko tuseme wasanii wote watumiao nahau, methali na vitendawili na misemo ya wahenga kwenye nyimbo zao nao wana kesi ya kuiba mawazo ya wahenga.

shida si maneno shida ni kipaji cha kufanya yale maneno yavutie huku yakiendelea toa elimu/mafunzo kwa jamii

sioni kosa kwa ngosha
Ndo nlitaka nimuone yeye akitoa ngoma zake kisimpo simpo km anavyodhan kua rahis C n P huyu jmaa[emoji38]
 
Hakuna kazi rahisi kama kufanya muziki anao ufanya Fid Q. Anacho kifanya Fid Q ni kutafuta best quotes kuhusu mada anayo taka kuiandikia wimbo au kusoma kitabu halafu akipata wazo zuri ndani ya kitabu hicho anacho kifanya ni kulitafsiri na kulifanya kama wazo lake.


Mfano kwenye wimbo mmoja wa Fid kuna mstari anasema " Maisha ni kama kioo ukiyachekea na yenyewe yanakuchekea'

Hii amecopy kwa MTU mmoja anaitwa Peace Pilgrim ambae nukuu yake inasema " Life is like a mirror if you smile at it it smiles back at you'

Nyimbo nyingi za huyu jamaa ni tafsiri ya mawazo ya watu wengine

Jambo linalo mfanya kuwa mfalme wa plagiarism Tanzania

Plagiarism ni kitendo cha kuchukua wazo la mwandishi mwingine.na kulipresent kana kwamba ni wazo lako bila kumu acknowledge muasisi wa wazo hilo.

Kwa nchi za wenzetu ambao wanalinda na kuthamini kazi za fasihi, Fid angekuwa ana rot in jail this time cause wahusika lazima wange msue na kwa kiwango cha idadi ya mistari aliyo iba kwa waandishi wengine sidhani kama angeweza kuwalipa, mwisho wa siku angeishia kuwa civil prisoner.

Katika ulimwengu wa kiroho anacho kifanya fid q ni kutembelea nyota za watu.

Kwa sababu nyota ya MTU INA include akili yake pia.

MTU amebuni wazo lake Wewe umelichukua na kulifanya wazo lako na ukapewa sifa na watu wengine wakiamini kwamba Wewe ndio uliw toa wazo hilo. Hapo maana yake ni kwamba unakuwa unatembelea nyota ya Huyo ambae umeiba wazo lake.

USHAURI WANGU KWA FID Q

Its high time now uanze kutumia mawazo yako Wewe mwenyewe ili tuweze kukutofautisha na kukushindanisha na artist wengine ambao wanafanya muziki kama Wewe.

Siwezi kukushindanisha na MTU kama Joh Makini au Nilki Mbishi kwa sababu wenzako wapo real na Wewe unatumia mawazo ya watu wengine . Yaani ntakuwa nawashindanisha na hao watu ambao una wa copy something which is not fair.

JUST BE REAL LIKE OTHER HIP HOP ARTISTS :
Mfano Babuu kwenye ngoma yake Kimbia kuna sehemu anasema

" POLISI NI MSHKAJI UKIWA NAE KITAANI, UKIFIKA KITUONI ANAKUACHA KAMA HAKUONI" Huu ni mstari ambao unarelate na uhalisia, ni filosofi na ufundisha. Hata mtoto atakae zaliiwa mwaka 2050 akiusikia huo mstari atauelewa na utamuhusu.

Anaweza kuwa ameimba kitu cha kawaida sana ( kwa viwango vyako ) lakini ni wazo lake mwenyewe.

Hujawahi kumsikia Chindo Man kwenye wimbo wa JCB feat Arusha All Stars akisema " TORATI YA STREET INASEMA USIWE FALA" Kwanini na Wewe usianze kuandika track zinazo tokana na utunzi wako mwenyewe?
Matter fact hiyo line ya Chindo hata Wewe inakuhusu kwa sababu kilichosemw na Babu Tale na Fella juzi kama ni kweli basi Wewe ni fala kweli coz kutokuwa na hela ni ufala kama alivyosema Mzee Upako.

Leave Mzee wa Upako aside Mzee upo kwenye game kwa miaka kumi na tano and huna hata gari na unalelewa? Kama ni kweli bro ufanyie kazi huo mstari wa Chindo

Mifano IPO mingi sana. Badilika and be real.

WATZ SIKU HIZI WAMEANZA KUSOMA VITABU..DONT THINK THEY DONT UNDERSTAND
Huyu jamaa hadi maisha yake mwenyewe ni ya Kucopy...binafsi simkubali Fid sababu hiyo. Kwa sisi tuliosikiliza Hip Hop tangu 80,s hana jipya zaidi ya kutafsiri mashairi ya watu. Kiukweli FiD he is not Real MC. He's just a "Wanna Be".
 
Nilijuaga jamaa anijiamini sana ila kwa hili la vs wasafi nikagundua jamaa nae kumbe ni wale wale wakukunjia mkia nyuma
 
Kuna thread ipo humu jf inaonyesha jinsi Fid Q anavyo iba nyimbo za wasanii wa zamani wa Marekani na kuzi translate kwa kiswahili, huo uzi unamchambua vibaya sana mshkaji, sina mb ningewaweeken link, Fid yule ni mzee wa kucopy, kuna mashairi aliya copy hadi aibu, link naitafuta nitaiweka baadae
 
Sanaa ni Ubunifu,sanaa yaweza kua kama asali/kachumbali,ni mchanyato wa vitu vingi,ndio maana kupitia kazi za sanaa tunapata ladha/burudani na pia tunapata ujumbe.
Ukifikiria kuiba ubunifu wa mwenzio omba lidhaa yake kwanza/au acknowledge wazo uliloliiba ndio uungwana katika sanaa..
 
Kuna thread ipo humu jf inaonyesha jinsi Fid Q anavyo iba nyimbo za wasanii wa zamani wa Marekani na kuzi translate kwa kiswahili, huo uzi unamchambua vibaya sana mshkaji, sina mb ningewaweeken link, Fid yule ni mzee wa kucopy, kuna mashairi aliya copy hadi aibu, link naitafuta nitaiweka baadae
mnahangaika nae!!..hebu wekeni hit tracks za fid tuone alikokopi..anzeni na propaganda
 
Huyu jamaa hadi maisha yake mwenyewe ni ya Kucopy...binafsi simkubali Fid sababu hiyo. Kwa sisi tuliosikiliza Hip Hop tangu 80,s hana jipya zaidi ya kutafsiri mashairi ya watu. Kiukweli FiD he is not Real MC. He's just a "Wanna Be".
hebu tuwekee hayo mashairi aliyotafsiri,kwenye ngoma yake yoyote ile uijuayo..na isiwe msemo mmoja
 
Umenena vyema mkuu vichwa maji watakubishia...

Nakumbuka hata ule wimbo wa classic material aligoma kuweka verse zake kwasababu alikua hajajipanga pakucopy Punch, akaona kabisa moko wa miujiza,unju bin unuki na singa singa watamwaibisha akabaki kupiga chorus tu
mpaka tunakwenda mitamboni Fid Q pamoja na uzuri wake ktk mistari hajamfikia Moko wa Miujiza hata kwa mita 200. Fid aliwai kutoka na Kuwait kupewa heshima na nyimbo zake huzitoa kwa muda mrefu kutengeneza public demand lakini miujiza ya uandishi ipo kwa Moko na flow ipo Stereo
 
Back
Top Bottom