Fid Q : The King of Plagiarism of all the time

Fid Q : The King of Plagiarism of all the time

Fid Q ni mwizi wa kazi za watu kweli. Niliwahi kujaribu kuwaonyesha watu humu jinsi jamaa alivyoiba wimbo wa KRS-1 mpaka baadhi ya bars na puns kama zilivyo na kujifanya ni mawazo yake. Ila uzi wako umelenga kumshambulia jamaa personally, na sio sanaa yake.
 
Once again I'm telling you this chief, nothing new in this universe, kazi ya sanaa ni pamoja na kutafsiri maneno magumu kwa lugha rahisi ili yaeleweke kwa wanaotaka kuelewa.

Fid Q anafanya vizuri kwenye game ndo maana yupo kitambo, hii ni kutokana na kusoma machapisho na kupata maarifa zaidi. Wangapi walikuepo na pengine walivuma pamoja na akina Fid Q toka enzi hizo ya zaidi ya 15 good years na huwasikii tena? Mfano Lucky Dube once said in one his song; “Not every BLACK MAN IS MY BROTHER and not every WHITE MAN IS AN ENEMY ” si kila mmoja wetu ataelewa haya, na haya maneno yalikuepo toka enzi na enzi, sasa Fid Q akitaka kuyatumia na kusema hivi; “Si kila mtu mweusi/muafrika ni ndugu yangu na Si kila mtu mweupe/mzungu ni adui” ungependa am-acknowledge nani hapo?
Akili ndogo, we c umemkopi Luck dube naye itabidi afanye hivyo
 
Hakuna kazi rahisi kama kufanya muziki anao ufanya Fid Q. Anacho kifanya Fid Q ni kutafuta best quotes kuhusu mada anayo taka kuiandikia wimbo au kusoma kitabu halafu akipata wazo zuri ndani ya kitabu hicho anacho kifanya ni kulitafsiri na kulifanya kama wazo lake.


Mfano kwenye wimbo mmoja wa Fid kuna mstari anasema " Maisha ni kama kioo ukiyachekea na yenyewe yanakuchekea'

Hii amecopy kwa MTU mmoja anaitwa Peace Pilgrim ambae nukuu yake inasema " Life is like a mirror if you smile at it it smiles back at you'

Nyimbo nyingi za huyu jamaa ni tafsiri ya mawazo ya watu wengine

Jambo linalo mfanya kuwa mfalme wa plagiarism Tanzania

Plagiarism ni kitendo cha kuchukua wazo la mwandishi mwingine.na kulipresent kana kwamba ni wazo lako bila kumu acknowledge muasisi wa wazo hilo.

Kwa nchi za wenzetu ambao wanalinda na kuthamini kazi za fasihi, Fid angekuwa ana rot in jail this time cause wahusika lazima wange msue na kwa kiwango cha idadi ya mistari aliyo iba kwa waandishi wengine sidhani kama angeweza kuwalipa, mwisho wa siku angeishia kuwa civil prisoner.

Katika ulimwengu wa kiroho anacho kifanya fid q ni kutembelea nyota za watu.

Kwa sababu nyota ya MTU INA include akili yake pia.

MTU amebuni wazo lake Wewe umelichukua na kulifanya wazo lako na ukapewa sifa na watu wengine wakiamini kwamba Wewe ndio uliw toa wazo hilo. Hapo maana yake ni kwamba unakuwa unatembelea nyota ya Huyo ambae umeiba wazo lake.

USHAURI WANGU KWA FID Q

Its high time now uanze kutumia mawazo yako Wewe mwenyewe ili tuweze kukutofautisha na kukushindanisha na artist wengine ambao wanafanya muziki kama Wewe.

Siwezi kukushindanisha na MTU kama Joh Makini au Nilki Mbishi kwa sababu wenzako wapo real na Wewe unatumia mawazo ya watu wengine . Yaani ntakuwa nawashindanisha na hao watu ambao una wa copy something which is not fair.

JUST BE REAL LIKE OTHER HIP HOP ARTISTS :
Mfano Babuu kwenye ngoma yake Kimbia kuna sehemu anasema

" POLISI NI MSHKAJI UKIWA NAE KITAANI, UKIFIKA KITUONI ANAKUACHA KAMA HAKUONI" Huu ni mstari ambao unarelate na uhalisia, ni filosofi na ufundisha. Hata mtoto atakae zaliiwa mwaka 2050 akiusikia huo mstari atauelewa na utamuhusu.

Anaweza kuwa ameimba kitu cha kawaida sana ( kwa viwango vyako ) lakini ni wazo lake mwenyewe.

Hujawahi kumsikia Chindo Man kwenye wimbo wa JCB feat Arusha All Stars akisema " TORATI YA STREET INASEMA USIWE FALA" Kwanini na Wewe usianze kuandika track zinazo tokana na utunzi wako mwenyewe?
Matter fact hiyo line ya Chindo hata Wewe inakuhusu kwa sababu kilichosemw na Babu Tale na Fella juzi kama ni kweli basi Wewe ni fala kweli coz kutokuwa na hela ni ufala kama alivyosema Mzee Upako.

Leave Mzee wa Upako aside Mzee upo kwenye game kwa miaka kumi na tano and huna hata gari na unalelewa? Kama ni kweli bro ufanyie kazi huo mstari wa Chindo

Mifano IPO mingi sana. Badilika and be real.

WATZ SIKU HIZI WAMEANZA KUSOMA VITABU..DONT THINK THEY DONT UNDERSTAND
Mkuu umesema ukweli kwa sehemu kubwa, lakini swali la kujiuliza je kati ya wasanii ni Did Q peke yake anaye iba mistari au idea za watu wengine bila kuwatambua (acknowledge)?

I know I can (Nas), idea yake imetumiwa na wasanii wengi tu akiwemo Kala Jeremiah (Wana Ndoto), Jikubali (Ben Pol) n.k

My Gal (R Kelly na Usher), Ngwea (RIP) na ........) idea imetumiwa kwenye wimbo wao wa Demu huyu ni wa kwangu

Nikumbushe lini Diamond amewa acknowledge wasanii anao wa copy, wa bongo na wa nje, mfano Zilipendwa

Ney wa Mitego anaingiza vikorombwezo vingi tu vya Wasanii wenzake, mfano kwenye wimbo wake wa Moto. Kibwagizo cha Wengi walikuwepo ......., pia ameingiza kibwagizo cha hili game hili ....... Je kuna sehemu ame wa appreciate Balozi na Sir Nature?

Huyo Joe Makini mwenyewe, ana m copy sana Nas, Mase na wengine

Hiyo ni mifano ya wasanii wa mziki wachache kati ya wengi wanao copy sehemu za mashairi ya wengine, je ni wangapi wanao copy kazi nyingine (sio mashairi) ikiwemo Vitabu na Misemo?
 
Fid Q ni mwizi wa kazi za watu kweli. Niliwahi kujaribu kuwaonyesha watu humu jinsi jamaa alivyoiba wimbo wa KRS-1 mpaka baadhi ya bars na puns kama zilivyo na kujifanya ni mawazo yake. Ila uzi wako umelenga kumshambulia jamaa personally, na sio sanaa yake.
Wimbo upi wa krs
 
He is just a Copy Cat watu wa Hip Hop watanielewa namaanisha nini. Sina haja ya kuweka hapa kila kitu...huu mchezo wa kucopy mistari na concepts za nyimbo za nje hajaanza yeye hata wakongwe wamefanya hiyo kitu..Mfano Balozi Dola kwenye Ngoma yake moja anasema "Ma Mc wanakweenda Wanaruudi" Wengi walikuwepo Lakini mimi Nitabaki" hapa aliiga Mashairi ya wimbo Wa Freddie Fox a.k.a Bumpy Knuckles (Huyu sidhani kama unamfahamu) wimbo unaitwa Mc'z Go Mc'z Come.
thats just the way it is,things will never be the same...huyo tupac,wale madem wakaimba na "thingd will never be the same again".. hapo wameiga au ni sentensi ya kawaida tu!!?..tukiwaambia muweke ngoma alizokopi mnarukaruka tu
 
  • Thanks
Reactions: Pep
thats just the way it is,things will never be the same...huyo tupac,wale madem wakaimba na "thingd will never be the same again".. hapo wameiga au ni sentensi ya kawaida tu!!?..tukiwaambia muweke ngoma alizokopi mnarukaruka tu
Hakuna unachokijua katika HipHop...HipHop ni Culture...FiD ni Big Failure katika Culture ya HipHop pamoja na Nguzo zake!
 
Hakuna unachokijua katika HipHop...HipHop ni Culture...FiD ni Big Failure katika Culture ya HipHop pamoja na Nguzo zake!
mi nipo na hiphop bongo tangu sele jabir anaiba beat za watu..kipindi hicho mama yako bdo msichana na maziwa yamemsimama..jibu ulichoulizwa
 
huyo gosha wenu mchovu fid q huwa namfananisha na pdiddy kwa kupeleka mambo kiujanja ujanja!
 
Huo msemo mbona upo kitambo hata kabla fid ajautoa, ko tuseme wasanii wote watumiao nahau, methali na vitendawili na misemo ya wahenga kwenye nyimbo zao nao wana kesi ya kuiba mawazo ya wahenga.

shida si maneno shida ni kipaji cha kufanya yale maneno yavutie huku yakiendelea toa elimu/mafunzo kwa jamii

sioni kosa kwa ngosha
achana nae huyo katumwa
 
Wewe sio kichwa, wewe unaweza fichwa

huo ni mstari kwenye ngoma yake ya Kiberiti alofanya na Saida Karoli na ilikua ni moja ya Diss alizopata kutoka kwa mashabiki wa timKiba baada ya kufanya Fresh remix na Mond

Jamaa anauwezo mkubwa sana lakini haya mambo ya kuingilia kati kati ya pande mbili zinazoshindana yamemkuta yakimcost siku za hivi karibuni, hii hali inawezachangia kushuka kwa heshima yake.
 
Back
Top Bottom