Tetesi: FIFA kuifungia Tanzania kufutia saga la mechi ya Simba na Yanga

Tetesi: FIFA kuifungia Tanzania kufutia saga la mechi ya Simba na Yanga

Mimi napenda sana football especially timu yangu ya simba ila natamani Fifa watufungie ili tuanze ku~focus na mambo ya no reforms no election maana ndio mambo ya msingi zaidi kwa kizazi hiki na kijacho kuliko upumbavu huu wa mpira utafiki tumekua taifa la matahira...
 
Akienda uwanjani kaingilia? Alitoa pesa kaingilia? Akiwashauri wakae vizuri ndio kaingilia?? Chuki isipitilize hadi mtu akifanyia wema mnalalamika
 
Mimi napenda sana football especially timu yangu ya simba ila natamani Fifa watufungie ili tuanze ku~focus na mambo ya no reforms no election maana ndio mambo ya msingi zaidi kwa kizazi hiki na kijacho kuliko upumbavu huu wa mpira utafiki tumekua taifa la matahira...

wewe ndani ya akili yako unaamini kabisa kila mtanzania anawazo huo upuuzi wenu?
 
Mkishaanza kupuuza, kutojali, kuzikanyaga na kufanya mambo yenu nje ya taratibu, kanuni na sheria zinazosimamia mambo ktk Jumuiya, jamii au taifa au vyama vya michezo ikiwemo TFF, basi tambueni kuwa mnakwenda kuwa kama Banana Republic...

Kosa lililosabisha haya yote ni ile siku ya kwanza tu Simba walipogoma kuja kucheza mechi yao wakati ratiba/fixture za mechi zao, muda wa mchezo na uwanja wa kuchezra walikuwa wanajua tangu awali, lakini TFF kupitia Bodi ya Ligi badala ya kusimamia sheria, waka entertain mazungumzo wakati timu imevunja kanuni/sheria ya mchezo...

Kilichopasawa kufanyika siku ileile ilikuwa ni kuangalia tu kanuni zitasemaje kwa timu kutofika uwanjani kucheza mchezo wake...

Bila shaka ni referee ku - assume kuwa mchezo umechezwa, timu ambayo imefika uwanjani inapewa pointi 3 na magoli 2 na baadaye adhabu zingine za kikanuni na kisheria zitolewe ikiwemo timu kupigwa faini na kulipia hasara ya maandalizi ya mchezo na kama gravity ya kosa ni kubwa, wafungiwe kushiriki ligi au washushwe daraja kabisa..

Shida ya soka la Bongo ni u - Simba na u - Yanga kusumbua. Utadhani timu Tanzania ni hizi tu wakati Kuna timu zingine 16 za ligi kuu zinaxotaka zitendewe haki pia...

Lakini kuanza kubembelazana kwa sbb eti ya Simba na Yanga tu na kuweka sheria pembeni, huo inakuwa ni ujinga na uwendawazimu ambao unaua soka letu..

Kwa kilichofanyika kwa mgogoro wa mpira wa miguu (football) kwenda kuamuliwa ikulu ya Rais (ofisi ya kisiasa), obvious FIFA/CAF watachukua hatua stahiki...

Hakuna mahali popote ktk sheria au kanuni za mpira wa miguu, ofisi ya Rais wa nchi fulani anatajwa kuwa sehemu ya chombo cha rufaa ya kufanya maamuzi ya mgogoro wa mchezo wa mpira wa miguu..
 
EEEeeenHEEEEEnHEE
Huwajui FIFA?
Naona unatumia 'lugha pendwa sana ya STAHA' kujieleza hapa!

Nyinyi watu ni matapeli kwelikweli. Sijui mmeibuka toka sayari gani nynyi?

Ulaghai ndi utamaduni wenu halisi.
😄😄😄😄😄
 
Vigezo ni kiwango cha ushabiki wa Watanzania kwa timu hizi mbili unless huishi Tanzania kuuliza swali hili. Mijadala kwenye media zote, vijiwe vya mitaani hata maofisini, kwenye magroup ya whatsapp nk. Ushabiki wa Simba na Yanga hapa Tanzania ni ugonjwa mbaya sana.
Si kwamba unataka kuwasukumia lawama zote mashabiki wa soka kwa ujinga wa watanzania? Kwamba ionekane watanzania wapo hivi walivyo kisa wanashabikia simba na yanga?
 
Fifa wanataka mpira uchezwe, Serikali imefanikiwa kusuruhisha pande zilizo kuwa kwenye mgogoro na mechi itachezwa, kuna shida hapo?
Rais akitoa ndege msafiri mnachekelea hamsemi anaingilia michezo, akitoa motisha ya goli la mama mnapokea hamsemi kaingilia michezo.
PELEKENI TIMU ACHENI KUTAFUTA PA KUJIFICHA KAMA MARCH 8
Kosa lilianzia hapo mkuu. Asante kwa kutukumbusha.
 
Back
Top Bottom