Mchezo wa leo baina ya Sweden na USA ulikuwa mzuri sana na USA walicheza vizuri sana wakiutawala uwanja. Kwa jumula timu USA waliielemea sana Sweden, ila kama nilivyowahi kuandika huko nyuma, USA haina wafungaji. Baada ya Rose Lavelle kupewa kadi mbili za njano wakati wa makundi hakucheza mchezo huu na kusababisha timu imtegemee Lindsey Horan, na Alex Morgan zaidi has kwa vile Sophia Smith hana uzoefu. Sasa Ingawa wote ni wacheazji wawili, center forwad Alex Morgan hana shabaha langoni tena kama zamani (sijui labda baada ya kujifungua). Timu USA ilipata nafasi nyingi sana lakini zote zikapotea mpaka nikazimia, ndiyo maana nimechelewa kuandika post hii. Ama walikuwa wanapiga nje ya goli au walikuwa wanamlenga golikipa au walikuwa wanachelewa kutoa uamuzi hadi wanabanwa kushindwa kufunga. Hakuna mshambuliaji aliyetoa mashuti kama yale aliyokuwa akipiga Christen Press yanayomfuata kipa halafu yanapiga kona angani.
Baada ya dakika 90 wakaongezewa nyingine 30 nako hawakupata kitu. Zikaja mikwaju ya Penalty ambazo ndizo zilzioamua ubishi.
Sweden walipiga penalty moja nje, na penalty nyingine ikazuiwa na golikipa wa marekani, na hivyo kupata penaly tatu. Lakini sasa marekani ilivurunda sana kwa kutoa penalty mbili nje, yaani moja ya veteran Megan Repinoe ilikwenda nje kabisa, halafu nyingine ya Sophia Smith nayo ilikwenda nje hivyo timu zote zikamaliza penalty kwa 3-3 (utaona kuwa Marekani wafungaji ndio walikuwa pumba kabisa)
Sasa walipoingia kwenye kipindi cha penalty za moja moja, Marekani bado Kelley O'Hara naye alishindwa kufunga penalty moja kwa kugonga mwamba na na kuisababaisha Sweden kupata goli la ushindi lilioamuliwa kwa VAR kwa sababu golikipa Alyssa naeher alidaka mpira ukiwa umeshapita zaidi ya nusu ya msitali kama inavyoonekana picha hii hapa chini. Matokeo ya mwisho yakawapa Sweden ushindi wa 5-4
Ingawa timu ya Merakani niliyokuwa nashabikia imetolewa, ilicheza mpira mzuri sana leo kuliko walivyocheza na Ureno; wanatakiwa kujifunza jinsi ya kufunga kwani ushindi ni kupenyeza magoli nyavuni.
Goli lililoipa ushindi Sweden
Highlights za mchezo huo ni hizi hapa; kwanza ni mchezo wa dakika 120
Halafu mikwaju ya penalty.
Baada ya Banyana Banyana na Team USA kuondolewa, sasa nimebakiza timu nne tu za kushabikia kwa order hii: Nigeria, Jamaica, Morocco, Japan na Australia; usiniulize kwa nini. Mchezo unaofuata ni baina ya Nigeria na Uingereza ambao utachezwa kesho saa 4 na nusu asubuhi (saa za Tanzania)