Spain vs Sweden; kipenga cha kwanza kimepulizwa na mchezo umeanza.
Katika dakika hizi za mwanzo mwanzo Spain wameonekana kuwaelemea Sweden kidogo.
Sina timu ninayoshabikia hapa ila Spain wanaonekana kuwaelemea sana Sweden labda upepo uubadilike huko mbeleni. Sweden walinitoa raha kwa kuiondoa Team USA kwenye mashindano haya kwa technicalities.
Pamoja na Spain kuilemea Sweden, bado timu zote hazishambuliani kabisa. Yaani Spain wanamiliki mpira sana lakini hawashambulii pia.
Mchezo bado haujasisimua kabisa
Umedoda sana. Sweden hawajafika kwenye goli la Spain na Spain nayo imefika golini kwa Sweden labda mara u mbili tu tena kwa udhaifu sana.
Dakika 45 za kwanza zimekwisha sasa tuko kwenye dakika za majeruhi.
Kipindi cha kwanza kimekwisha wala hakikusisimua kabisa. Nia kama walikuwa wanaogopana vile.
Tumeaza kipindi cha pili sasa
Sijaweka updates kwa vile mcehzo umedumaa sana inga ni hivi karibuni tu wameanza kushambuliana lakini siyo kwa nguvu sana.
Spain ilijaribu kusmabulia sana lakini kicks zake zote zilikuwa zinakwenda nje.
Spain wamepata goli la kuongoza. Kuna mcheazji wa Spain anitwa Slam ndiye amefunga bao hilo; watangazaji wanasema ndioye pial aliyewafunga Uholanzi, kwa hiyo anaonekana ni star wa magoli sana.
Sweden wamesawazisha mara moja; haikukuchukua hata dakika tano kwa Sweden kusawazisha.
ndani ya muda mfupi, Spain wameongza bao jingine la kuongoza. Sasa hivi tuko kwenye dakika za mejeruhi. Mpira umependeza sana dakika hizi za mwishoni. Mpaka sasa Spain inaongoza 2-1.
Katika dakika hizi za mejuri, husu Spain ikiongoza, imeamua kuimarisha sana ulinzi langoni mwake. Sweden watapata muda mgumu sana kupenya na zimebaki kama dakika nne tu.
Spain imeshinda; dakika hizi za mwisho mpira ulisismua sana kwani wanwake wa pande zote mbili walianza kushambuliana kwa nguvu sana. Hata hivyo Sweden ambayo nayo ilikuwa mojawapo mwa vigo wa mashindano haya ameatolewa. Sasa hivi amebaki kigogo mmoja tu-England. Wengine wote ni underdogs : Spain, Australia, na kigogo England
View: https://www.youtube.com/watch?v=h7Mlf7chPJs